Mjadala: Je, ni kweli Mikopo na Misaada ya China kwa nchi za Afrika imejaa mitego ya Kisheria?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,710
13,462
Je, ni kweli Mikopo na Misaada ya China kwa nchi za Afrika imejaa 'Mitego ya kisheria'?

China inaonesha kwenda kuwa taifa kubwa kiuchumi na kuziondoa nchi za magharibi katika nguvu walizonazo. Je, waafrika wategemee kitu gani?

Ungana nasi katika Mjadala na Wataalamu na Wadau wa Uchumi, kupitia TwitterSpaces ya JamiiForums, leo Ijumaa, Novemba 11, 2022, kuanzia saa 12: 00 jioni hadi Saa 2: 00 usiku.

Mjadala: https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzXgavoRJv

9C926417-3A03-41CB-8CA0-EBE15C9075C7.jpeg

UPDATES:

KAPILA HADJI KAVENUKE

Kuhusu mikopo ya China kama ni kweli imejaa Mitego, kujibu moja kwa moja ni ngumu kwa kuwa kila Mkopo una mtego wake

Mara nyingi Misaada yao huwa siyo moja kwa moja inahusisha Fedha, inawezekana ikawa Miundombinu mbalimbali

Mikopo ya Mataifa mengine huwa ipo wazi, mfano hapa naweza kusema ile ya Wazungu ni tofauti na ile ya Wachina ambayo inakuwa ina usiri sana

Wao wanadai Mikopo yao inasaidia kuboresha uhusiano wa Nchi na Nchi, nadhani ni muhimu kuwa makini

Naishi Zambia, nitoe mfano wakati wa Corona, hapa walikuwa na deni kubwa la China hadi ikafikia hatua Rais wa Zambia akasema wazi kuwa Nchi haiwezi kulipa madeni yaliyokuwa yakidaiwa. Ogopa sana Mtu ambaye anakupa kitu kisha anakwambia tumia tu

CHIEF RUNDOKO
Mikopo haina mitego, ninachojua kabla ya kusaini kuna Jopo la Wataalam wetu wa Sheria mfano Wizara husika, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali n.k.

Kwa hiyo tatizo si China, tatizo ni Watanzania kuwa Wazalendo ili kusaidia nchi yetu!

ANANIA
China imetengeneza miradi mingi ambayo inaweza kuinua uchumi wao, wanaendeleza kile kilichoasisiwa na aliyekuwa kiongozi wao, Mao Zedong akiwataka wazaliane sana ili kuwe na nguvu kazi nyingi

Hiyo wanaitumia kuendelea kusambaa na kuongeza nguvu kazi

Kupata mikataba ambayo wamesaini huwa ni ngumu kwa kuwa mara nyingi inawabeba wao

Mikopo ya China huwa inatengeneza mazingira ya kuunganishwa na vitu, mfano wakijenga barabara wanaweza kutengeneza mazingira ya wao wakusanye ushuru kwa muda mrefu

Mfano kilichotokea Zambia walipojenga Uwanja wa Ndege mkataba ukawa unawapendelea wao Wachina kwa kuwa asilimia kubwa ya kodi zikawa zinaenda kwao, ikawa ni kama vile miundombinu ipo Zambia lakini anayefaidika ni Mchina kutokana na mikataba iliyosainiwa

ZITTO KABWE
Kuhusu utaratibu wa mikopo ya Nchi, Waziri wa Fedha anaomba kibali cha kukopa ndani ya Bunge, Bunge likipitisha inamaanisha limempa kibali

Ndio maana kwenye ripoti ya Mkaguzi wa Serikali huwa anatoa taarifa ya hali ya mikopo kama imezidi kiwango au la

QUANTUSHA
Ni kwanini Serikali zetu za Afrika, huwa hazituambii ama kwanini huwa hawaiweki wazi masharti wanayokutana nayo huko? Ama wao huangalia mafungu yao baada ya kupewa mikopo tu?

Kuna Masharti mengine huigharimu Nchi nzima tunakujaga kusikia mara pap hao ni Wawekezaji

ZITTO KABWE
Niliandika makala JamiiForums, nilieleza kuna maneno mengi sana yamejaa hisia kuliko uhalisia. Nilionesha takwimu za 2018 au 2019 kuwa mikopo mingi haitoki China bali inatoka kwenye Taasisi nyingine za kimataifa kama vile Benki za Dunia

Kumekuwa na propaganda nyingi kuhusu mikopo ya China, kusema kuwa mikopo yao inaukandamizaji siyo sahihi japokuwa mikopo haifanani Mara nyingi mikopo yao wakikujengea kitu lazima katika uendeshaji wafanye wao

Kuna chumvi nyingi kuhusu mikataba ya China, Vyombo vya Magharibi vimekuwa vikizungumza na kufanya propaganda kuhusu China Ni muhimu kuzungumza kwa uhalisia na kwa takwimu, hata hao wanaotajwa Zambia, mikopo yao kutoka China haikuwa katika kiwango hicho

MANFRED MANDA
Viongozi wetu wanakosa Negotiation Power na Uzalendo. Wizara zote zina Wanasheria tena wanasheria wazuri Binafsi sidhani kama kuna mitego ya kisheria bali mitego ni ya kiuchumi, kizalendo na kiakili.

Sera zetu za kiuchumi ziko kwa ajili ya Walanchi ama Wananchi?

ZITTO KABWE
Tatizo siyo Wazungu au Wachina, tatizo ni sisi wakopaji ndio tunatakiwa kujua tunachokitaka Mfano bomba letu la gesi tulilojengewa tunatumia asilimia ndogo, kumbuka tunatakiwa kuanza kulilipia lakini sisi hatutumii hilo bomba inavyotakiwa

Tatizo Nchi nyingi za Afrika tunajenga miradi ambayo hatuitumii Unatakiwa kuchukua mkopo wa kitu ambacho unataka kukitumia, ukichukua mkopo kwa kitu ambacho haukitumii lazima utaona hasara na utaona hauna faida na ndivyo ilivyo kwa Nchi nyingi

MWAURA ROBERT
Mikopo ya China imejaa mitego ya Kisheria, nakubaliana na hilo, Wachina wana malengo fulani, tena wanaangalia miaka 30 hadi 50 mbele, hawaangalii hapa miaka mitano Mfano wakijenga reli basi malighafi zitatoka kwao na zitatumiwa kwa faida yao

Ukipewa mkopo na taasisi nyingine mfano Benki ya Dunia wanakupa masharti na wanataka iwe wazi, lakini China wao wanakupa na hawajali utakavyotumia

Hiyo inaonesha wao siyo marafiki wa Afrika hata kidogo

ZITTO KABWE
Sikubaliani na hoja kuwa China si rafiki wa Afrika, ni muhimu Waafrika tuwe makini kuhusu hoja hiyo

China imesaidia Nchi nyingi, nakumbuka kuwa hatukutawaliwa na Wachina

FADHIL MGAYA
95% ya Viongozi wetu wanajilipua kwenye hii mikataba bila kuifanyia uchambuzi yakinifu wa kiintelinjisia kuhusu thamani ya sasa ya Mikopo hiyo na ya baadaye

Wanakurupushana tu na kukwea pipa

MUCCIFIVE
Mkopo sio tatizo, tatizo unafanyia nini huo mkopo? Lakini Afrika Mikopo inaishia mikononi mwa watu Bora mikopo ya China wanajenga miundombinu kwa namna moja ama nyingine inasaidia Wananchi wa ndani.

Mikopo ya Wazungu wanakuzuia hata baadhi ya miradi usijenge

ZOBOGO
Sasa hivi hakuna nia njema ya kusaidia nchi za Afrika kote kwa mataifa ya Magharibi na China Hii mikataba ni mtego, ni sisi wenyewe tunapaswa kupambana. Tuna Watu wenye 'level' kubwa za elimu lakini hata madaraja madogo tu tunatengenezewa na China
 
Mchina nae anapambania maslahi ya watu wake! No free Lift!! Huwa ni mdhulumati sana, wafanyakazi kwenye kampuni zake ni dhiki kubwa.
 
Debt trap walianzisha wazungu, sasa hivi wanamuonea gere Mchina..
 
Zitto ni mwanasiasa na kwa sasa analamba asali hawezi kuisemea china vibaya labda kwa kushikiwa bunduki.

Kwa kifupi hakuna mtoa mkopo asiyepata faida kutoka kwa anayempa, wachina hata wakitoa mkopo kwa masharti yasiyoonekana ila wanajua huko mbele zitto hatakuwepo wala aliyesaini huo mkataba so wajukuu wataangaika nao.
 
West wanaumia sana wanavyoona mchina anaijenga dunia, 😂,maana wao kazi yao ni kuharibu na sio kujenga, hivyo propaganda dhidi ya china, haziwezi kuisha
 
West wanaumia sana wanavyoona mchina anaijenga dunia, ,maana wao kazi yao ni kuharibu na sio kujenga, hivyo propaganda dhidi ya china, haziwezi kuisha
Huna ujualo mchina anamiliki entebe airport baada ya mda wa kurejesha deni kupita huko zambia ndio mchina kaikamata yote pesa anapeleka kwao hawafanyi kitu kwa hasara hao.
 
Huna ujualo mchina anamiliki entebe airport baada ya mda wa kurejesha deni kupita huko zambia ndio mchina kaikamata yote pesa anapeleka kwao hawafanyi kitu kwa hasara hao.
Wachina ni tatizo kubwa!! Ogopa mtu mwenye watoto kumi Huku akijitia kukusaidia wewe mwenye watoto watatu!! Macho yake yote ni Kwa wanae!! China is highly populated!! Tupambane watanzania chine is not a developing partner
 
Huna ujualo mchina anamiliki entebe airport baada ya mda wa kurejesha deni kupita huko zambia ndio mchina kaikamata yote pesa anapeleka kwao hawafanyi kitu kwa hasara hao.
Hakuna mwekezaji akawekeza kwa hasara, hata wazungu wanakupa msaada kwa masharti wanaume waoane🤷‍♂️
 
Hakuna mwekezaji akawekeza kwa hasara, hata wazungu wanakupa msaada kwa masharti wanaume waoane
Na kuna kitengo maalum cha kushawishi nchi za Africa zikope pesa kama raisi unakataa kukopa yajayo yanafurahisha watukuundia zengwe la kila aina ila ukikopa mara kwa mara watakupa tuzo mpaka basi.
 
Back
Top Bottom