MJADALA: Jamii ina Uelewa Juu ya Ugonjwa wa Lupus?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
676
1,093
LUPUS MJADALA.jpg
Je, unaufahamu Ugonjwa wa Lupus, Dalili na jinsi ya kushughulikia nao? Je, unafahamu 90% ya Wagonjwa wa Lupus Duniani ni Wanawake?

Kumekuwa na Uzushi kuwa watu wenye Ugonjwa wa Lupus hawawezi kuishi muda mrefu. Mtu mwenye Ugonjwa wa Lupus anaweza kuishi umri mrefu kama watu wengine iwapo atapata Matibabu ya uhakika na uangalizi mzuri.

Jamiiforums ikiwa miongoni mwa Wadau wa muhimu katika kutoa elimu ya afya inashirikiana na Wataalamu mbalimbali wa afya ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa mbalimbali ikiwamo ugonjwa wa Lupus.

Usikose kujiunga nasi katika Twitter Spaces ya Jamiiforums siku ya Jumatano ya Mei 31, 2023, kuanzia Saa 12 Jioni hadi Saa 2 Usiku kuwasilikiliza Wataalamu wa Afya wakifafanua kwa kina yote yahusuyo ugonjwa wa Lupus.

Aidha, mjadala huu utakupa nafasi ya kusikiliza na kuuliza maswali kwa wataalamu kuhusu ugonjwa huo.

Pia unaweza kutoa maoni na kuuliza maswali kupitia uzi huu na yatasomwa siku ya mjadala.

Karibu


=======================

Ugonjwa wa Lupus ni ugonjwa unaoathiri viungo mbalimbali vya mwili kutokana na mashambulizi ya mfumo wa kinga ya mwili kwa viungo hivyo unaosababishwa na hitilafu ya mfumo huo. Kutokana na hitilafu hiyo viungo vya mwili huathirika ikiwa ni pamoja na ngozi, moyo, figo, mapafu, mfumo wa fahamu, damu na misuli. Waathirika wa ugonjwa huu huwa na dalili mbalimbali kutegemea na mfumo wa mwili ulioathiriwa, pia inawezekana mgonjwa akapata athari kwenye mfumo zaidi ya mmoja au mifumo yote ya mwili kuathirika.

Takwimu za kitafiti kutoka nchi zilizoendelea hususani, Ulaya na Marekani zinaonyesha kuna wagonjwa 20-150 kwa kila watu 150,000 mpaka 400,000, na ugonjwa huu hushambulia zaidi watu wenye asili ya Afrika, wakifuatiwa na watu wenye asili ya bara Asia. Pia ugonjwa huu huathiri zaidi wanawake kwa uwiano wa mwanaume mmoja na wanawake tisa katika kila wagonjwa 10. Miongoni mwa dalili zinazotambulisha ugonjwa wa Lupus ni mabaka kwenye mashavu yanayoonekana kama umbo la kipepeo na kutokana na muonekano huu kipepeo hutumika kama nembo ya ugonjwa huu. Dalili nyingine ni homa, uchovu, nywele kulainika na kukatika, viungo kuuma na kuungua sana na jua.

Kutokana na aina ya athari zinazotokea kwa wagonjwa wa Lupus, na kupata dalili katika mifumo mbalimbali, mwili wagonjwa wa Lupus hutibiwa na wataalamu wa afya wa aina mbalimbali kulingana na viungo/mifumo ya mwili iliyoathirika. Miongoni mwa wataalamu hawa ni pamoja na Madaktari wa ngozi, wa figo, wa moyo, wa mfumo wa fahamu, mapafu n.k. Ugonjwa wa Lupus uko katika kundi la magonjwa ya Rheumatism, na wataalamu wa magonjwa haya yanaitwa Rheumatologists, na nchini kwetu wapo Madaktari wapo watatu tu.

Siku ya Lupus duniani iliasisiwa na Lupus Canada ambalo ni shikrikisho la wagonjwa wanaoishi na ugonjwa wa Lupus nchini Canada mwaka 2004, na huadhimishwa kila tarehe 10 Mei kila mwaka huku mwezi wa Mei ukitumika kama mwezi wa kutoa elimu juu ya ugonjwa huu. Nchini Tanzania siku ya Lupus duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 2021 na maadhimisho haya yalifanyika katika Chuo Kikuu Cha Afya Muhimbili (MUHAS) kwa miaka miwili ya awali na maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kama sehemu ya maadhimisho ya mwezi na siku ya Lupus Duniani mwaka 2023, jukwaa la majadiliano limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Lupus Warriors Tanzania (Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoundwa na wagonjwa wa Lupus Tanzania), Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Jamii Forums.
---
Mjadala Umeanza
Baadhi ya hoja zilizotolewa na Wataalamu wa Afya
DKT. FRANCIS FURIA (Daktari bingwa wa magonjwa ya figo na Rheumatism MNH na Profesa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili): Hakuna tafiti za moja kwa moja zilizofanywa na kubaini kwa nini Ugonjwa wa Lupus unaathiri zaidi Wanawake.

Lakini tafiti za awali zinaonesha kuwa hormoni za kike zinaweza kuwa zinachangia kusababisha ugonjwa huo, pia wakati wa ujauzito huwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

DKT. ANGELA MIGOWA: Tafiti kutoka nchi zilizoendelea hususani, Ulaya na Marekani zinaonesha Ugonjwa wa Lupus hushambulia zaidi watu wenye asili ya Afrika, wakifuatiwa na watu wenye asili ya Bara Asia,

Hakuna takwimu kamili zinazotajwa idadi ya Wagonjwa lakini katika Nchi ambazo wanafanya utafiti wa Kisayansi kuhusu Lupus kumekuwa kukibainika waathirika.

DKT. ANGELA MIGOWA: 20% ya Wagonja wa Lupus ni Watoto, nitoe mfano mfano kati ya wagonjwa 300 ninaowahudumia kwa Kenya, kati yao 30% huwa ni wagonjwa wa Lupus, lakini hiyo siyo takwimu kamili kwa maana huo ni mtazamo wangu kuhusu kile ninachokutana nacho.

100% ya Wagonwa wa Lupus ninaowahudumia huwa wanakuwa na athari katika ngozi japokuwa kuna changamoto nyingine kadhaa.

Ugonjwa huo kwa amaye ameathirika katika Ngozi anaweza kusumbuliwa na mwaka wa jua katika sehemu aliyoathirika, kuwashwa, pia kuna kitu kinaweza kutokea kinaitwa ‘shilingi’.

DKT. ANGELA MIGOWA: Athari nyingine ya Ngozi kwa mgonjwa wa Lupus ni pale inapotokea unamtibu mtu ngozi na hapati nafuu basi jua hiyo ni dalili, pia mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri na kusababisha ngozi kuanza kuwa nyeusi.

Takwimu za kitafiti kutoka nchi zilizoendelea hususani, Ulaya na Marekani zinaonyesha kuna Wagonjwa wa Lupus 20-150 kwa kila watu 150,000 mpaka 400,000

Miongoni mwa dalili zinazotambulisha Ugonjwa wa Lupus ni mabaka kwenye mashavu yanayoonekana kama umbo la kipepeo na kutokana na muonekano huu wa kipepeo hutumika kama nembo ya ugonjwa huu

Dalili nyingine ni homa, uchovu, nywele kulainika na kukatika, viungo kuuma na kuungua sana na Jua.

Maureen Manyama (kutoka Lupus Warriors Tanzania): Niligundulika kuwa na Ugonjwa wa Lupus nikiwa na umri wa miaka 19 wakati huo nikiwa chou, nilianza kuwa nachoka sana, Ngozi yangu ikaanz akubabuka pembeni ya pua na kwenye mgongo.

Sikwenda kumuona daktari kwa kuwa nilikuwa katika mitihani, nilikuwa Afrika Kusini, nikabahatika kumuona daktari bingwa, baada ya vipimo ndipo nikabainika nina Lupus.

Kutokana na aina ya athari zinazotokea kwa Wagonjwa wa Lupus, na kupata dalili katika Mifumo mbalimbali, Mwili Wagonjwa wa Lupus hutibiwa na Wataalamu wa Afya wa aina mbalimbali kulingana na Viungo/Mifumo ya Mwili iliyoathirika

Miongoni mwa Wataalamu hawa ni pamoja na Madaktari wa ngozi, wa figo, wa moyo, wa mfumo wa fahamu, mapafu n.k. Ugonjwa wa Lupus uko katika kundi la magonjwa ya Rheumatism, na wataalamu wa magonjwa haya wanaitwa Rheumatologists, na Nchini kwetu wapo Madaktari watatu tu.

Maureen Manyama: Niliporudi Tanzania kulikuwa na changamoto kidogo kwa kutopata wataalam, hali ikaendelea kuwa mbaya, nikavimba mwili mzima, nikashindwa kula baadaye nilipopelekwa Agha Khan nikafanikiwa kukutana na daktari bingwa ambaye alikuwa na ufahamu mzuri wa Lupus

Ninasumbuliwa na Lupus, ilifikia hatua nikawa najaa maji kwenye moyo, nilipoelezwa mwanzo sikuelewa ugonjwa huo kwa kuwa sikuwa naujua na nilijihisi mpweke.

Niliona kama ni ugonjwa ambao unanisumbua mimi mwenyewe, lakini baadaye nikabaini kuwa kuna wagonjwa wengine.

DKT. Beatrice Mkenda (kutoka Lupus Warriors Tanzania): Nilibaini kuwa nina ugonjwa huo baada ya kujifungua, awali sikujua na baada ya vipimo nilivyofanya katika hospitali kubwa nikiwa #Sweden ndipo nikabainika kuwa nina #Lupus, sikuwa naujua kabisa ugonjwa huo.

Daktari akanielezea zaidi kuhusu Lupus na kunipa ushauri kuwa sitakiwi kukaa juani muda mrefu, iliniumiza na ilinichanganya.

Jean Orwa Banda (kutoka Kenya Lupus and Kidney Foundation): Nilibainika nina Lupus wakati nikiwa chuo nasoma, changamoto niliyokutana nayo tangu nilipobainika kuwa figo iliathirika, hali ambayo imesababisha mambo yakabadilika mengi kwenye mwili.

Kabla ya kuanza kuumwa nilikuwa mjamzito lakini bahati mbaya mimba ikatoka, inaonekana ilikuwa ni dalili za mwanzoni ambazo zikujua, changamoto nyingine ni kukosa usingizi.

Elizabeth Achilles (Kutoka Lupus Warriors Tanzania): Ugonjwa wa Lupus kila siku inanibidi ninywe Dawa, changamoto nyingine ni kuwa Mtu akikuona unakunywa Dawa kila Siku anakunyooshea vidole.

Wakati mwingine ugonjwa unaweza kunifanya nichoke, naweza kuwa fiti asubuhi muda mfupi baadaye hali inabadilikaUgonjwa huo umenifanya niwe na changamoto ya kusahau kwa kuwa umeathiri Ubongo wangu.

Ugonjwa huo umenifanya niwe na changamoto ya kusahau kwa kuwa umeathiri ubongo wangu

Maureen Manyama (kutoka Lupus Warriors Tanzania): Ugonjwa wa Lupus umebadilisha Maisha yangu, nilikuwa mwanariadha lakini sikuendelea tena na mchezo huo, muonekano wangu umebadilika kwa kuwa ngozi na nywele vimeathirika sikai juani kwa muda mrefu

Lakini kupitia ugonjwa huu nimepata watu wengi ambao ni mashujaa, wananishauri na wanapambana, pia mimi imebadili fikra zangu tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

Dkt. Beatrice Mkenda (kutoka Lupus Warriors Tanzania): Baada ya kujua nina Lupus changamoto nilizokutana nazo ni kushindwa kufanya kazi ambazo zilihitaji nitumie nguvu.

Lakini imenifanya niujue mwili wangu na kujua nini cha kufanya, hilo ni jambo chanya ambano naweza kusema nimeliona kutokana na ugonjwa huu.

Jean Orwa Banda (kutoka Kenya Lupus and Kidney Foundation): Ni muhimu wagonjwa wa #Lupus kuwa pamoja, kuna wakati ugonjwa unaweza kuathiri hisia za mhusika, watu wengine wanaweza kutoelewa

Umoja na kuwapa Faraja ni jambo zuri linaloweka kusaidia saikolojia ya Mgonjwa, pia taasisi zinatakakiwa kutoa mwamko ili jamii ijue

Mfano JamiiForums wanapoandaa mjadala kama huu ni kitu kizuri na ninapoingeza kwa kuwa inasaidia jamii kujua kuhusu Lupus.

Taasisi zinatakiwa kuwapa nafasi Wagonjwa wa Lupus na kuwasaidia hata kiuchumi, hiyo inaweza kuwasaidia kujikimu kwa kuwa Mgonjwa wa Lupus anapokosa kushikwa mkono anaweza kuathirika.

Jean Orwa Banda: Taasisi zinatakiwa kuwapa nafasi Wagonjwa wa Lupus na kuwasaidia hata kiuchumi, hiyo inaweza kuwasaidia kujikimu kiuchumi kwa kuwa Mgonjwa wa Lupus anapokosa kushikwa mkono anaweza kuathirika.

Madaktari nao wanatakiwa kutoa elimu ya kwanini Wagonjwa wa Lupus wanatakiwa kunywa dawa kila siku, unajua ni jambo gumu kumeza dawa kila siku na wakati mwingine tunakunywa tukia hatuna elimu au uelewa wa umuhimu wa kufanya hivyo.

DKT. Francis Furia: Kuna uwezekano wa kuwa na wagonjwa 20,000 Nchini Tanzania wanaoathiriwa na Lupus. Ugonjwa wa Lupas hauambukizwi, unatokana na hitilafu katika mfumo wa mwili kushambuliwa na kuathiri sehemu mbalimbali za mwili na ndio maana mgonjwa anaweza kusumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
 
Mjadala unaendelea.

Maureen Manyama: Niliporudi Tanzania kulikuwa na changamoto kidogo kwa kutopata wataalam, hali ikaendelea kuwa mbaya, nikavimba mwili mzima, nikashindwa kula baadaye nilipopelekwa Agha Khan nikafanikiwa kukutana na daktari bingwa ambaye alikuwa na ufahamu mzuri wa Lupus

ninasumbuliwa na Lupus, ilifikia hatua nikawa najaa maji kwenye moyo, nilipoelezwa mwanzo sikuelewa ugonjwa huo kwa kuwa sikuwa naujua na nilijihisi mpweke

Niliona kama ni ugonjwa ambao unanisumbua mimi mwenyewe, lakini baadaye nikabaini kuwa kuna wagonjwa wengine.
 
SLE
(Systemic Lupus Erythematosus)
Inflammatory disease caused when an immune system attack its own tissues

it affects ;
-skin, joints, blood cells, brain, kidneys, heart and Lungs

 
Back
Top Bottom