UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,710
- 12,784
Wakuu habari za leo
Bila shaka mnaendelea na ujenzi wa Taifa na kujipatia kipato endelevu,Mungu awatie nguvu sana wapambanaji wote!.
Moja kwa moja kwenye mada.
Sitaki kuandika sana leo!.
Mimi kwa upande wangu natumia sana Jamii forum,Google na YouTube.
Hiyo ndiyo mitandao yangu pendwa kwasababu imenisaidia kujifunza mambo mengi na mengine nayafanyia kazi.
Kupitia Jamii forums nimejifunza udereva na naelekea kumaliza na kujipatia leseni ya udereva hivi karibuni,hii yote ilitokana na kusoma nyuzi fulani humu za kutia moyo vijana na kutaka tupambane,pia kupitia mtandao huu wa Jamii forum nimejipatia Pasipoti ambayo hapo mwanzo sikuona umuhimu wa kuwa nayo.
Pia kuna uzi nimewahi kusoma na naendelea kusoma hapa unahusu maisha ya nje ya nchi na fursa zinazopatikana huko hasa Marekani,Kanada na Uingereza.
Kiukweli baada ya kusoma nyuzi hizo kiukweli nategemea Mwakani nirudi shule kusomea Medical doctor kuanzia ngazi ya cheti mpaka Degree,ingawa inahitaji pesa naamini nitapambana.
Japo kwasasa nimesoma na nina Diploma ya Business Administration niliyoipata pale Kampala University tawi la Da es salaam,lakini lazima nirudi kwenye Elimu ninayo ipenda ya Udokta kwasababu pia nilifaulu vizuri masomo yote ya sayansi,nitaanza ngazi ya cheti kabisa!.
Pia kupitia uzi huu nimepata somo namna ya kununua bidhaa nje ya nchi,na hapo hapo pia nimeweza kufungua sanduku la posta kupitia namba yangu ya simu,hivyo kurahisisha mambo mengi kiukweli,pia nategemea kupata Visa card ya mitandao ya simu(Voda na Airtel) hivi karibuni,hii yote ni faida ya Jamii forum.
Hiyo ni faida niliyoipata hapa Jamii forum kwa muda mfupi na nadhani nitapata faida kadiri nisomavyo nyuzi mbalimbali humu.
Upande wa Google umenisaidia mambo mengi sana ambayo nilikuwa siyafahamu hasa,kujifunza lugha ya kiingereza kwa ufasaha n.k.
Upande wa YouTube huko huwa napenda sana kuangalia documentary mbalimbali zinazo nisaidia sana,pia naangalia mahubiri ili kujilisha kiroho,nyimbo za dini pia naangalia huko,naangalia pia vichekesho vya Joti a.k.a Nishai Kitombangile kitwango ili kuupa ubongo haki yake ya kufurahi wakati mwingine.
Pia mimi ni mpenzi wa nyimbo za Kongo hasa Bolingo,hivyo huwa ni rahisi kuzipata huko,kiukweli huwa sijutii bando langu ninapoingia moja ya mitandao niliyotaja hapo.
Hayo ni mambo baadhi napenda sana kuangalia huko.
Kwenye simu yangu pia ninao mtandao wa Instagram ambao kwangu nataka niufute kwasababu naona hauna faida kwangu,huwa najaribu kupitia mambo kadhaa ya elimu lakini ghafla unakutana na mwanamke kavaa nusu uchi anatikisa mitako,kiukweli huu mtandao kwangu ni changamoto ndo maana naufutilia mbali kabisa.
Facebook,huu ndo sizani kama nitakuja hata kuupakua kwasababu sijaona faida yake.
Twitter,ninayo kwenye simu yangu na nimefollow watu muhimu ambao wana madini sana,nadhani huu ni mzuri kwa uapande wangu.
Tiktok sina kabisa na sijaona umuhimu wa kuupakua.
WhatsApp huu ninao na unanisaidia kunikutanisha na marafiki zangu kwa wepesi zaidi.
Nadhani kwasasa mitandao iliyonisaidia sana kwa upande wangu ni Jamii forum,Google na YouTube.
Huwa nikiweka bando liikisha ninakuwa nimejifunza kitu kipya.