Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 2,965
- 4,577
Mpira au Soka ni moja kati ya michezo ya kipekee sana, ni mchezo ambao umejaa makeke mengi sana na nyakati za huzuni na Furaha, kwa wengi mpira umevunja ndoa za watu kwa wale wenzangu ambao ni mashabiki kindakindaki, wale ambao wapo Tanzania ila wanafuatilia mpaka Ligi kuu ya Brazil ambapo Mechi zake nyingi huchezwa kuanzia saa 8 ama saa 9 usiku.
Sasa mwanamke anaona ni bora aende kwao tu kuliko kulala peke yake huku mumewe yuko anaangalia mechi kali kati ya Flamengo dhidi ya Internationale.
Mpira umewaleta karibu watu, mfano tu kupitia matawi mbalimbali ya vilabu vya soka nchini, watu wengi wamejenga urafiki wa kudumu, na wengine wamepata na nduu zao humo humo.
Lakini pia mpira umejenga chuki na uhasama mkubwa sana baina ya mashabiki wa timu kadhaa. Chuki ambazo huonekana wazi wakati wa mitanange mbalimbali endapo tu timu hizi zikakutana uwanja. Baadhi ya mashabiki hutoleana maneno makali, wengi hupigana na kuchoma wenzao kwa visu huku vifo pia vikitokea.
Leo Nitakupa mechi kali ambazo kwa hakika kabsa ni mechi ambazo duniani zimekuwa kivutio kikubwa sana, ni mechi ambazo zimevuta hisia za mashabiki kwa ukaribu sana na zingine zimeleta mpaka fujo na ugomvi kwa watu na ugomvi mkubwa.
Karibu kwenye sehemu ya kwanza;
1. Borussia Dortmund dhidi ya Schalke 04
Tuanzie huko Ujerumani twende Kaskazini ambapo tunakutana na timu mbili kubwa zenye historia ya kuheshimika sana ndani ya Ujerumani na Ulaya. Nazungumzia klabu za Borussia Dortmund na Schalke 04 ambao hawa ni watani haswa kwani mechi yao ya watani wa jadi ilianza mwaka 1925 huku mashabiki wa timu hizi mbili wakiwa ni maadui haswa, na endapo timu moja ikifungwa basi washindi hutengeneza jezi maalumu kushangilia ushindi wao.
Na wajuzi wameipatia mechi hii jina la The Revierderby, na hii ndio mechi ya kwanza ya watani wa jadi ndani ya Ujerumani.
2. Ugiriki dhidi ya Uturuki
Ugiriki dhidi ya Uturuki ni mechi nyingine kubwa ambayo sio ya kubeza hata kidogo, timu hizi mbili za taifa ni watani wa jadi ambao hata mashabiki wake huishia kuchapana makofi endapo wakikutana uwanjani.
View attachment 2648173
Mwaka 2002 Uturuki alipambana sana mpaka kufikia hatua ya nusu fainali huku Ugiriki akitoka kwa aibu, na mwaka 2008 Ugiriki na Uturuki walipangwa kundi moja kwenye michuano ya EURO huku Uturuki akipata bahati tena ya kuingia hatua ya nusu fainali akimuacha mwenzake Ugiriki mbali sana.
3. Porto dhidi ya Sporting
Twende mpaka Ureno ambapo tunakutana na timu mbili zenye historia na heshima kubwa sana kwenye tasnia ya mpira wa miguu, hawa ni Porto pamoja na Sporting Lisbon. Ukipata nafasi ya kushuhudia mchezo baina ya timu hizi mbili kwenye uwanja wa taifa wa Ureno, Estadio Nacional basi utakubaliana nami kuwa ni vita kubwa sana ndani ya dakika 90 za mchezo. Porto wanaotokea Kaskazini mwa Ureno na Sporting Lisbon wanaotokea Kusini mwa Ureno wamecheza michezo mingi baina yao huku Porto akiwa na historia nzuri kuliko Sporting Lisbon, huku wote hawa wawili wakiwa hawajawahi kuteremka daraja tokea wamepanda kwenye ligi ya Ureno Premeira Liga.
View attachment 2648174
Mtanange huu naufananisha kwa ukaribu zaidi ya ule mtanange wa Minho baina ya Vitória de Guimarães dhidi ya SC Braga.
4. Flamengo dhidi ya Vasco de Gama
View attachment 2648178
Tutoke Ureno na twende Amerika Kusini mpaka Ardhi ya Marehemu Pele, maskani kwa kina Ronaldinho Gaucho, Romario, Ronaldo De Lima,Neymar, Dida na kadhalika. Ardhi iliyobarikiwa mafundi na wasanifu bora sana wa kucheza na mpira wa miguu. Huko tunakutana na mechi moja kali sana baina ya Flamengo dhidi ya Vasco De Gama. Wababe hawa wawili wakikutana uwanjani basi nyasi hutoa cheche kabsa, wameibatiza mechi hii kwa jina la "Clasico dos Milhoes" au Mechi ya Matajiri, huku Flamengo pamoja na Vasco De Gama wakiwa na mashabiki wengi sana kutoka Brazili, na nchi jirani mpaka Amerika ya Kusini kwa ujumla, na kwa kawaida watu takribani milioni 50 hufuatilia mechi hii na hii inachukuliwa ndo mechi kubwa sana ndani ya Brazili.

Ukifika kwenye uwanja wa Maracana, pale kwenye Jiji la Rio de Janeiro ni kawaida kuona mashabiki wakiwasha moto majukwaani na fujo ambazo kwa mara kadhaa zimepelekea ugomvi na hata vifo vya mashabiki.
5. Marseille dhidi ya Lyon
Tuondoke Brazili na twende moja kwa moja mpaka Ulaya na tufikie pale Ufaransa ambapo tunakutana na mechi kubwa sana ndani ya Ufaransa, baina ya Olympique Marseille dhidi ya Olympique Lyon.

Mechi haina uadui sana kiasi cha kutoana roho bali ni mashabiki tu wamekuwa wakiwapatia moto sana wachezaji. Wafaransa wameibatiza mechi hii jina la Choc des Olympiques kwa maana ya Mpambano wa Olimpiki.
6. Partizan dhidi ya Red Star
Tutoe Ufaransa na tusogee mpaka Serbia ambapo tunakutana na mechi kubwa sana ndani ya soka la nchi ya Serbia baina ya Partizan dhidi ya Red Star, timu mbili zenye mafanikio makubwa ndani ya Serbia na zenye mashabiki wengi sana. kitu cha pekee ni mashabiki wake ambao hujipanga vyema sana katika namna ya kuwashangalia wachezaji wao kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya uwanja.

Mashabiki hutumia bendera za timu zao pamoja na nyimbo wakiwa uwanja na kuoneshana nani zaidi kwenye uwezo wa kuwaunga mkono wachezaji wao.
7. Besiktas dhidi ya Fenerbahce
Tutoke Serbia na turejee Uturuki kidogo na kuangalia mechi moja kubwa sana baina ya wababe, Besiktas dhidi ya Fenerbahce, ambapo wana historia ya kukutana zaidi ya miaka 100 huku ikiwa ni moja ya mechi kubwa sana ndani ya Jiji la Istanbul, kwa mara kadhaa timu hizi huchuana kuwa namba moja kwenye misimamo wa ligi kuu ya Uturuku na mara nyingi mechi hizi baina yao ndo huamua ni nani anatakiwa awe juu ya misimamo.

Timu hizi mbili hazina uswahiba hata kidogo, huku mashabiki wake wakichapana ngumi, na kupelekea mpaka majeraha wakati wa kubishana kuhusu uwezo wa timu fulani. Besiktas ilianzishwa na watu waliokuwa wakiishi Uturuki iliyokuwa upande wa Ulaya, wakati Fenerbahce ikianzishwa na watu waliokuwa wakiishi Uturuki upande wa Asia, na hii inatosha kuweka mafuta kwenye makaa ya moto, na kuipatia mechi hii utamu wa ajabu sana.
8. Nacional dhidi ya Penarol
Tuondoke Uturuki na kueleka tena Amerika Kusini mpaka nchi ya Uruguay, maskani ya miamba ya soka la Amerika, Luiz Suarez, Edson Cavani na kadhalika. Basi huko tunakutana na mchezo baina ya Nacional dhidi ya Penarol, timu ambazo zote zinapatikana kwenye jiji la Montevideo, ingawa timu hizi hazina mafanikio makubwa nje ya Amerika Kusini ila zimesaidia sana soka la Amerika Kusini kupita hatua sana, ndani ya Uruguay pamoja na michuano ya Bara la Amerika ya Kusini al maarufu kama Copa Libertadoes. Wajuvi wa mambo wameipatia mechi hii jina la Clasico of Uruguay.

Sasa mechi hii ndo vita halisi kwani sio tu mashabiki bali hata wachezaji wamekuwa wakionesha uvunjifu wa amani na utovu mkubwa wa nidhamu. Tarehe 14 Aprili mwaka 1990 timu hizi mbili zilicheza mchezo wake ambao ulikuwa mgumu kweli na walitoshana nguvu wa magoli sifuri bin sifuri huku wachezaji 22 wakitolewa nje kwa kadi nyekundu, wachezaji wa Nacional 11 walitolewa nje kwa utovu wa nidhamu huku pia wachezaji 11 kutoka timu ya Penarol wakitolewa nje kwa makosa hayo, dakika 85 mchezo huo ulisimama kwa sababu timu zote hazikuwa na wachezaji wa kutosha uwanja, hakuna timu iliyokuwa na wachezaji saba, kwa Kifupi walibakia wachezaji wawili tu.
Mwaka 1991 wakakutana tena na uwanja ambao ulitakiwa wachezaji wacheze soka basi ukabadilika na kuwa ulingo, wachezaji wakabadilishana vitasa kwa kiwango kikubwa sana huku wachezaji 9 na kocha moja wakifungwa jela mwezi mmoja kutokana na kuanzisha ugomvi huo, kutokea mwaka 1800 mpaka sasa timu hizi mbili zimeshakutana zaidi ya mara 520.
9. Chelsea dhidi ya Liverpool
Tuondoke Uruguay na tupae mpaka Uingereza ambapo tunakutana na mechi kali sana baina ya wababe wawili, Chelsea dhidi ya Liverpool, ingawa sio mechi kubwa sana yenye historia ila kukutana kwako kwenye michuano mikubwa kama UEFA pamoja na Kombe la Ligi kumeongeza utamu wa mechi hii.
Namkumbuka John Arne Riise alivyojifunga goli kwenye dakika za majeruhi kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa ya UEFA ya mwaka 2008 na kuifanya Chelsea kuingia fainali.

Lakini sitosahau mwamba, goli kipa bora sana, Mhispania, Pepe Reina alivyoizuia penalty ya Geremi akiwa pale kwenye uwanja wa Majogoo wa Anfield mwaka 2007. Lakini uadui mkubwa ulichochewa na uhamisho wa mchezaji Fernando Torres ambapo Chelsea walivunja kibubu na kutoa paundi milioni 50 ili wamchukue Torres huku Bwana Mkubwa Torres akidai kuwa Chelsea ndo timu kubwa kuliko Liverpool, basi tegemea kukutana na kitu cha moto sana endapo Chelsea akienda Anfield ama Liverpool akienda darajani pale Stamford Bridge.
10. LA Galaxy dhidi ya San Jose Earthquakes
Tutoke Uingereza na twende mpaka Amerika Kaskazini pale kwa Biden ambapo tunakutana na mechi kubwa baina ya LA Galaxy dhidi ya San Jose Earthquakes. Ukipata nafasi ya kuingia kwenye dimba la Buck Shaw Stadium, pale Santa Clara, California basi utaona utamu wa mpira na ufundi mkubwa wa soka la Marekani.
Ingawa soka bado halijanoga sana ndani ya Ardhi ya Marekani kama ilivyo michezo ya Golf, Tennis ama Mbio za Magari ila mechi baina ya LA Galaxy ikichuana na San Jose Earthquakes sio mechi ya kubeza kabsa kwani huvutia watu wengi kwenda kushuhudia ufundi wa soka.

Mtananage huu ni baina ya Kusini wa Jimbo la California dhidi ya Kaskazini mwa Jimbo la California, na wameibatiza mechi hii kwa jina la California Clasico.
Nakumbuka mpira safi sana uliopigwa na San Jose Earthquakes dhidi ya LA Galaxy tarehe 21 Agosti mwaka 2010 kwenye uwanja wa Buck Shaw Stadium uliopo pale Santa Clara, California na San Jose Earthquakes kutoka kifua mbele kwa ushindi wa goli moja kwa sifuri.
Tuungane kwenye sehemu ya pili!!!