The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,141
- 1,944
Nyakati za usiku ni kama hiyo harufu inafunguliwa maradufu mtu huwezi kupata usingizi ukigeuka kulia, kushoto umelala unavuta harufu ya pombe kali.
Wamiliki wa kiwanda hajali usalama wa wakazi walio karibu na kiwanda kwani yanatiririshwa maji machafu yenye harufu kali ya pombe, ambayo moja ya madhara yaliyosababishwa na maji hayo ni kuuliwa kwa samaki zilizokuwa zikifugwa na mtanzania mmoja baada ya maji hayo kufikia bwawa la samaki.
Maji yanayotiririshwa si salama na hayadhibitiwi inavyotakiwa, liko wapi Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mnafanya kazi gani wakuu tunasikia tu kuwa NEMC walikuja hapo kiwandani lakini hakuna dalili inayoonesha kuwa changamoto hii itatatuliwa karibuni.