Miss Rwanda akamatwa na Polisi kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,932
5,256
Polisi nchini Rwanda (RNP) wamemkamata mshindi wa taji la Miss Rwanda 2022, Divine Muheto (21) kwa kurudia "kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi" na kuharibu miundombinu kisha kukimbia eneo la tukio.
1730278503370.png
Mrembo huyo anakabiliwa na mashtaka mengine kadhaa, ikiwemo kuendesha gari bila leseni, polisi walisema. 'Hii si mara ya kwanza kufanya kosa hili' kupitia chapisho X

Vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Muheto vimezua wasiwasi, kwani ukiukwaji wa sheria za barabarani unaorudiwa unaendelea kuhatarisha usalama wa umma. Baada ya kukamatwa kwake, polisi walisema kuwa jalada lake limewasilishwa kwa upande wa mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
1730278572150.png
Muheto alipata umaarufu aliposhinda shindano la urembo la Miss Rwanda 2022, mnamo Machi 19, akimrithi Grace Ingabire kwenye taji hilo, kabla ya serikali kusitisha shindano hilo kwa tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya waandaaji.
 
Back
Top Bottom