Misiba na mitandao ya kijamii

zwenge ndaba

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
2,037
3,596
Utakuta ndugu wamekuficha kwa muda habari za msiba wa ndugu yako mpaka pale utapofika nyumbani au kwa lengo lingine tu la muhimu lakini ukiingia mitandaoni unakuta tayari umeshaanza kupata pole wakati haujui chochote.

Inauma sana, dawa yake ikiwezekana waliopo karibu waifiche simu yako kwa muda ujue imeibiwa. Utandawazi unakuwa kwa kasi na pia una athari zake nyingi katika jamii.
 
Umesema kweli mkuu, nakumbuka kama miaka miwili iliyopita rafiki yangu mmoja alifiwa na mama yake na baadhi ya marafiki wa karibu tukaambiwa tusimwambie kwa sababu alikuwa na mtihani bahati mbaya kuna ndugu yake akaitupia mtandaoni ilikuwa noma
 
duh.inavuruga kila kitu.alafu ukute umbali ni mrefu mpaka kufika home sasa
 
Kwanini tusiwaambie wafiwa na tuendelee kuwaficha? Kuna tofauti gani akijua sasa na baadae ya huko aendako?
 
Kuna watu wana vimbelembele sn utadhani wanakujali sana mbona hawatangulizi rambirambi wao wanaishia pole tu
 
Wakina mama huwa hawanaga stahmilivu kuvumilia ukishawaambia , ndo mtaa mzima itakuwa makelele, then itategemea na mtu wengine hupandwa na presha nae akaondoka ikawa msiba tena , tuwe tunaangalianga na watu wa kuwaambia
 
sion kama kuana haja ya kumficha mtu apewe tu ukweli
 
hakuna kitu kilichokosa kasoro hapa duniani
intaneti ni nzuri kwa kusomea,mambo ya biashara,kupashana habari lakini hiyo hyo ndio inayotumika katika maswala ya wizi
 
Kwanini tusiwaambie wafiwa na tuendelee kuwaficha? Kuna tofauti gani akijua sasa na baadae ya huko aendako?
inategemea na mazingira mkuu na mtu mnaye mpaka taarifa.nilishashudia mmoja alijirusha kwenye gari wakati akielekea msibani.unaona kama haufiki.hakuna kitu kinauma kama kupoteza mtu wa thamani sana kwako
 
hakuna kitu kilichokosa kasoro hapa duniani
intaneti ni nzuri kwa kusomea,mambo ya biashara,kupashana habari lakini hiyo hyo ndio inayotumika katika maswala ya wizi
ndo maana nikasema japokua ina umuhimu lakini pia madhara yake ni makubwa kama ilivyo faida zake
 
Wakina mama huwa hawanaga stahmilivu kuvumilia ukishawaambia , ndo mtaa mzima itakuwa makelele, then itategemea na mtu wengine hupandwa na presha nae akaondoka ikawa msiba tena , tuwe tunaangalianga na watu wa kuwaambia
ni kweli kabisa
 
Umesema kweli mkuu, nakumbuka kama miaka miwili iliyopita rafiki yangu mmoja alifiwa na mama yake na baadhi ya marafiki wa karibu tukaambiwa tusimwambie kwa sababu alikuwa na mtihani bahati mbaya kuna ndugu yake akaitupia mtandaoni ilikuwa noma
Maobm yote yana faida na hasara pia. Chagua jema upate mema!
 
Kuna watu wana vimbelembele sn utadhani wanakujali sana mbona hawatangulizi rambirambi wao wanaishia pole tu
pole pia inatia faraja mkuu isipokua inatakiwa kuangalia unampa pole kama ata anajua maana kama wakumpa taarifa inatakiwa uwe ndugu zake kwanza
 
Mtu kafiwa saa nne asubuhi af hajui na ana mtihani wa mwisho saa nane mchana sa kwa nini nimwambie sasa....naacha mpaka masaa yapite ya huo mtihani...
 
Kwanini tusiwaambie wafiwa na tuendelee kuwaficha? Kuna tofauti gani akijua sasa na baadae ya huko aendako?
Hujawah kufiwa ndo maana unaropoka lazima aandaliwe mazingira mfano mtu yupo kagera msiba wa mtu muhimu dar unataka aambiwe huko huko je unajua yupo mazingira gani? ?maswali mengine ya kitoto labda kama na wewe ni mtoto sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…