Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 23,800
- 43,477
Hili sakata linaloendelea la Rais Donald Trump kutishia kufuta misaada iliyokuwa inatolewa kwa Nchi Maskini hasa afrika imezua kasheshe.
Hata hivyo wananchi ktk mataifa mbali mbali yaliyoko kwenye orodha inayotishiwa wamekuwa na hisia na mawazo tofauti juu ya kadhia hiyo.
Wengine wanasema mataifa hayo yataathrika kwa sehemu kubwa hasa ktk nyanja za miradi ya elimu, afya na shughuli za kiuchumi kama kilimo, ufugaji, barabara na biashara pia.
Hata hivyo kundi lingine linadai kwa nuda wa miaka mingi tangu uhuru serikali za Afrika zimepokea matrilioni ya fedha za misaada.
Soma Pia: Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika
Na kinachoonekana kama matokeo ya misaada ni kidogo sana. Wengine wakidai wanufaika wa pesa za wa hisani ni watu wachache tu wenye mamlaka kutokana na kukithiri kwa Ufisadi, ufujaji wa mali za umma, rushwa, kukosekana kwa misingi ya utawala bora kama uwazi na uwajibikaji.
Hali hiyo imepelekea Raia wa Nchi hizo kudhani kwamba misaada inaishia mikononi ai mifukoni mwa Watawala wa Nchi zao.
Ndio maana Raia wengi wanaonekana kufurahia agizo la Rais Trump kusitisha misaada kwa miezi mitatu.
Mpaka sasa Mashirika ya Misaada ya Marekani kama USAID wameanza utekelezaji mara moja tangu Tamko hilo Jan 20, 2025.
Kwa Upande wa Tanzania hatua hiyo inaweza kuwa na madhara kadhaa ikiwemo watu kukosa ajira, miradi mbali mbali ya afya na elimu yaweza kuathirika kwa kiasi fulani.
Hata hivyo tunatumaini kupata ripoti ya uchambuzi kutoka kwa wataalam wa uchumi watueleze ni kwa namna gani tunaweza kuathiriwa na uamzi huo ikiwemo mbinu za muda mfupi na muda mrefu za kukabiliana.