Asilimia kubwa ya wafungwa wanaomaliza vifungo vyao hasa wafungwa wa vifungo vya zaidi ya miaka miwili wamekuwa wakipata changamoto kuyaanza tena maisha ya uraiani kutokana na kukosa ajira na pesa kama mitaji yakuanzisha biashara na kuendesha shughuli zao na kupelekea wengi wao kujiingiza kwenye wizi na uhalifu mwingine.
Wafungwa wanapomaliza vifungo vyao wamekuwa wakipewa nauli tu ya kurudi makwao lakini upo uwezekano wa kuwapatia kiasi cha fedha cha kuyaanza tena upya maisha yao ya uraiani ili kupunguza vishawishi vya kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.
Ili kuhakikisha hili linatimia ipo miradi inayoweza kuanzishwa na jeshi la magereza na kufanywa na wafungwa kwa kushirikiana na askari magereza hasa wenye taaluma katika miradi husika.
BAADHI YA MIRADI INAYOWEZA KUANZISHWA NA MAGEREZA

- Kushika tenda za ujenzi kutoka kwa watu binafsi makampuni au serekali; jeshi la magereza kwa kushirikiana na serekali lina uwezo wa kuanzisha kampuni ya ujenzi hasa ujenzi wa majengo na kuwatumia wafungwa wenye taaluma za ujenzi pia kuajiri wahandisi wa majengo katika kampuni na kuongeza wigo wa ajira kwa raia na kusaidia wafungwa kupata kipato katika kipindi cha kutumikia adhabu zao.
- Viwanda vidogo vidogo mfano viwanda vya ushonaji wa nguo ambavyo vitasaidia kupunguza uagizwaji wa nguo kutoka nje ya nchi pia vitaongea mapato katika jeshi la magereza. Pia viwanda vya kufyetua matofali ambavyo vitawatumia wafungwa wengi hasa wasio na taaluma yoyote.
- Karakana za ufundi seremala na ufundi wa magari; na kuchukua tenda za utengenezaji wa madawati ya shule za serekali hata vitu vya thamani vya majumbani na maofisini pia magari ya magereza ya watu binafsi na ya serekali.
- Kilimo na ufugaji; uanzishwaji wa mashamba ya ufugaji wa kisasa na kitaalam zaidi na kilimo cha umwagiliaji itasaidia kwanza wafungwa wenyewe kupata chakula bora na cha uhakika pia itaongeza usalama wa chakula katika nchi yetu.
- Kampuni ya huduma za usafi zitakazotoa huduma hizo katika maofisi makubwa ma viwandani mahospitalini na katika taasisi za serekali.