Mimi (wewe) ni nani haswa? Majibu yanaweza kufumbua fumbo la mwanadamu ni nani na asili yake pia hatima yake

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,454
34,475
Leo ukisimamishwa ili ujitambulishe kuwa wewe ni nani, kwa vyovyote vile utaanza kutaja majina yako, ukiendelea mbele zaidi unaweza kutambulisha anuani unayotoka ama nasaba yako. Majina uliyonayo ni ya kupewa na wazazi ama jamii yako lakini hayana uhusiano na wewe as mtu.

Lakini, unachokitaja hapo havina uhusiano na wewe kama mtu. Kwa mfano kwenye kutaja viungo vya mwilini utaweza kuorodhesha Mkono wangu, Mguu wangu, Kichwa changu, tumbo langu....... na kadhalika. Lakini ukiulizwa wewe ni nani utataja jina lako ama jinsia.

Je, wewe ni nani haswa? sahau kila kitu chako. Tujadiliane hapa kutafuta majibu. Wewe (mtu) ni nani haswa? Uwepo wako ni upi haswa. Unajitambua ama tufanyeje kujitambua?
 
Umeuliza swali tata sana

BINADAMU ni
Mwili na nafsi
Mwili unabeba nafsi

Mwili ni kama hardware na nafsi ni kama software

MWILI ni jumla ya vitu vyote vilivyo ungana kumtengeneza binadamu kama mikono macho moyo korodani nywele nk nk

NAFSI ni ule utashi wako wa ndani unao utumia kuamua mwili ufanye nini nk nk

Kwahiyo wewe sio single item

Wapo waumini wa IMANI wanakwenda mbali zaidi kwa kusema binadamu ni Mwili nafsi na ROHO
 
Je katika UMiMi (wewe) wangu ni katika umoja au wingi?

Umetoa jibu pana mno ambapo linaibua hoja zaidi
 
Mkuu Mimi nimejaribu kujibu kutokana na utata wa namna ya kujibu swali lako

Ni tata kujibu haswa ulipo maanisha nisitaje majina wala vyeo nk kwasababu havina uhusiano na mimi( which is true kwa kiasi fulani)
Lakini majina na maneno yapo ili kutofautisha vitu kuleta maana

Kujibu swali lako Mimi ni Ujumla (umoja)
 
Mimi mtu ni energy(umeme/wazo).
Sihitaji mwili ili niwepo ila nahitaji mwili ili kuonekana dhahiri(wazo kuwa kitu) na kutimiza kusudi.

Kinachoniunganisha mimi na mwili ni nafsi. Hivyo nafsi hubeba utambulisho wangu.

Natumia nafsi kujidhibiti/ kuconnect kati ya mimi na mwili wangu maana mimi ni spirit/energy tu ila mwili nimuunganiko wa vinasaba( kumbukumbu) zinazoendana na mazingira husika.

Hivyo baada ya muunganiko huo ndio naonekana mimi mtu(wazo) kupitia mwili.

Nikijitambulisha mimi ni nani, ni kuiwakilisha nafsi upande iliyouchagua mfano: wewe(wazo) unataka kutimiza jambo fulani lakini itakuhitaji uvumilivu na muda kutimiza hilo jambo lakini wakati huo huo mwili hautaki shida unahitaji kupata raha, hivyo kutakuwa na vita kati ya wewe na mwili na kitachoamua hatima yako ni nafsi either ichague upande wa mwili au upande wa wewe.

Hapo utajitambulisha mvumilivu au mwenye tamaa kulingana na upande ulivyochagua nafsi yako na inakuwa ni mwendelezo wa tabia yako ama ya utambulisho wako.
 
Kisayansi bao moja lina jumla ya mamilioni kama sio bilions sperms
Na kila sperm ikikutana na yai lililo iva la mwanamke inatunga mimba....... hivi ndio tunavyojua binadamu anavyotengenezeka.

Kwa muktadha wa sperms na yai la mama, nipe darasa hapo mkuu jinsi mimi(energy) ambaye si hitaji mwili kuwepo ninakuwa wapi kabla sijaingia kwenye mwili na jinsi ninavyo kuja kuingia kwenye mwili na kuonekana, na ninakwenda wapi baada ya mwili kufa?
Na uthibitisho wa uwepo wangu kabla ya mwili(kuonekana) na baada ya mwili ni upi?
 
Umeuliza swali tata sana

BINADAMU ni
Mwili na nafsi
Mwili unabeba nafsi

Mwili ni kama hardware na nafsi ni kama software

MWILI ni jumla ya vitu vyote vilivyo ungana kumtengeneza binadamu kama mikono macho moyo korodani nywele nk nk

NAFSI ni ule utashi wako wa ndani unao utumia kuamua mwili ufanye nini nk nk

Kwahiyo wewe sio single item

Wapo waumini wa IMANI wanakwenda mbali zaidi kwa kusema binadamu ni Mwili nafsi na ROHO
Sio waumini, ni watu wote.

Roho ndio chanzo cha nishati ya mwanadamu...energy.

Dini inaelezea kwa undani chanzo cha nishati hii ila sayansi mpaka sasa haijui lolote.

NAFSI ni identity yako tuu, na memory creator, kwenye ulimwengu wa roho.
 
Kisayansi bao moja lina jumla ya mamilioni kama sio bilions sperms
Na kila sperm ikikutana na yai lililo iva la mwanamke inatunga mimba....... hivi ndio tunavyojua binadamu anavyotengenezeka.

Kwa muktadha wa sperms na yai la mama, nipe darasa hapo mkuu jinsi mimi(energy) ambaye si hitaji mwili kuwepo ninakuwa wapi kabla sijaingia kwenye mwili na jinsi ninavyo kuja kuingia kwenye mwili na kuonekana, na ninakwenda wapi baada ya mwili kufa?
Na uthibitisho wa uwepo wangu kabla ya mwili(kuonekana) na baada ya mwili ni upi?
Kwanza kabisa mkuu wewe au mimi kabla ya uhai(life) tulikuwa ni unit of energy zinazo float aimlessly in a state of slumber zikitafuta a new opportunity ku experience life hapa duniani.

Sasa inapotokea mimba inatungwa(yaani sperm na yai kuunganika). Energy inayokuwa interest na hao wazazi ndio inachagua mimba ya kuwa associate nayo(ni kumaanisha wewe ndio unachagua mzazi atayekuzaa ila hauchagui moja kwa moja bali involuntary(yaani kuna Supreme power inayokuchagua wewe kati ya energy nyingi) lakini pia inatokana na karmik circumstance kuwa alike kati yako na wazazi wako. Hapa ni kusema, cause - effect (karma) ya wazazi na wewe ndio itakayovutia uwe associated na hiyo mimba(uingie kama nishati ya uhai).

Baada ya mimba kutungwa some studies zinasema ni baada ya miezi mitatu, zingine zinadai ni after conception energy inakuwa associated na kiumbe kilichopo tumboni na hapo ndipo kinabeba uhai.

Baada ya maisha ya duniani, huyu mtu anatengana na mwili anarudi alipotoka anakuwa katika state ya awali kama alivyokuwa kabla ya kuzaliwa yaani anakuwa na uzima ila hana uhai na anakuwa ni kama mtu anayeota njozi.
Uthibitisho ni mfano ulipokuwa tumboni kwa mama je, unakumbuka chochote? Jibu ni hapana.

Life(uhai) means consciousness, hivyo ili mtu atimize kusudi lake la kuwepo duniani ni lazima awe na chombo(mwili) wa kukuwezesha kufanikisha mambo katika ulimwengu wa physical, astral and mental plane kwa kipindi cha muda maalumu.
 
Mkuu nashukuru umeelezea asili na after life ya duniani.

Tuchukue mfano huu,
Mkono WANGU
Tumbo LANGU
Mguu WANGU......

That Wangu, Yangu, Langu, n.k. unaweza kusema ni MIMI. Swali langi siyo molecules au atoms zinazounda mwili bali Holder wa huo mwili ni nani haswa?

Tutafakari kwa kina labda tunaweza kuambulia kitu
 
Mkuu molecule na atom zinahusika sana katika ufanyikaji wa human body. Kwa kupitia genes za wazazi ndo unapatikana mwili lakini nishati ya mwili haihusiani na wazazi.

Holder(mtu) yeye ni mmiliki wa mwili, hadi kuuchagua ni kumaanisha karma yake na wazazi zimefanana kulingana na kusudi lake.

That’s why mzazi ana uwezo wa kutoa laana na ikampata mtoto vizuri tu maana yeye amehusika katika formation ya mwili wa mtoto kwa kiasi kikubwa.
 
Mkuu nashukuru umeelezea asili na after life ya duniani.

Tuchukue mfano huu,
Mkono WANGU
Tumbo LANGU
Mguu WANGU......

That Wangu, Yangu, Langu, n.k. unaweza kusema ni MIMI. Swali langi siyo molecules au atoms zinazounda mwili bali Holder wa huo mwili ni nani haswa?

Tutafakari kwa kina labda tunaweza kuambulia kitu
Holder wa mwili ni wewe mwenyewe. Ndio maana unasema mwili wangu...

Na mwili wa mtu mwingine utasema mwili wake...

Kuuliza "Holder wa mwili ni nani" tayari swali lako linataka majibu ya mtu fulani au kiumbe fulani kilichopo mahali fulani kinacho hold vitu vyote.

Hapa swali litakuja tena huyo " Holder wa mwili" yeye holder wake ni nani?
 
Leo ukisimamishwa ili ujitambulishe kuwa wewe ni nani, kwa vyovyote vile utaanza kutaja majina yako, ukiendelea mbele zaidi unaweza kutambulisha anuani unayotoka ama nasaba yako. Majina uliyonayo ni ya kupewa na wazazi ama jamii yako lakini hayana uhusiano na wewe as mtu.

Lakini, unachokitaja hapo havina uhusiano na wewe kama mtu. Kwa mfano kwenye kutaja viungo vya mwilini utaweza kuorodhesha Mkono wangu, Mguu wangu, Kichwa changu, tumbo langu....... na kadhalika. Lakini ukiulizwa wewe ni nani utataja jina lako ama jinsia.

Je, wewe ni nani haswa? sahau kila kitu chako. Tujadiliane hapa kutafuta majibu. Wewe (mtu) ni nani haswa? Uwepo wako ni upi haswa. Unajitambua ama tufanyeje kujitambua?
Sisi hatujawai kujiona bali tunacho kiona ni mwili tu ...ambao huo mwili siyo sisi bali sisi ni nafsi ndani ya ubongo wa mwili wa mwanadamu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom