Mimi ni mwajiri lakini nimekuwa kama mtumwa kwa wajiriwa

osama BLD

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
561
294
Nina kampuni Dar nina wafanyakazi 20 mbao mishahara yao ni kati lak2 na 1.5m.. nilianza 2010 hadi Leo. Ila nina hali mbaya ya uchumi kulingana na ninachokipata lakini mpaka sasa sidaiwi na mfanyakazi yeyote mshara wa mwezi wa 3 wala kodi ya pango nalikuwa nikilipa 6m kwa mwezi Ila kwa sasa nalipa 3m. Ila nishara hiyo na kodi nalipa kwa imani ya mungu.

My point for last 4 years tangu 13,14,15,16,17 ninaishi maisha ya shida yani ninachopata mimi ikizidi Ni hela ya mafuta ya gari na hela ya kula basi au ninywe bia 3 Mara1 kwa wiki .

Kitu ambacho mimi kinanifanya kuona kwamba naishi kwa ajili ya hao wanaonitegemea kumbuka yeye mpaka alipwe mshara wake na rent ilipwe na garama zingine xa serikali na other running cost.

Mwezi makusanyo napata kama 30m lakin cpati chochote wala my family kuenjoy Kuwa baba ana ofc imefikia sehem hata ile kumpa mtu business kadi ilioandikwa director naona aibu naishi bila matumaini ya Kesho naishi ili mfanyakazi aishi.

Ila miaka 3ya mwanzo hali haikuwa mbaya nilichokuwa napata nikawa naimarisha ofc..

Nikisema nifunge ofc wafanyakazi wanikumpatia boss please tusubir huwez kuja ya Kesho Ila akija kudai mshara ndio utamjua na wenye jengo nao hawana maongexi maana ni shirika

Naongea kwa masikitiko maakubwa sana na sina saving yeyote ile ya kuanxisha kampuni nyingine au biashara yeyote ile Ila nafahamu biashara nyingi mpaka sasa...

Naomba ushauri ndugu zangu
 
Pole sana kiongozi, naona namna unavyopambana kusaidia ndugu zako watanzania, nasema huo ndio uzalendo wa kweli ila usifanye kitu kwa manung'uniko utakosa baraka ulizopangiwa na MUNGU
 
Nilichogundua hukua mfanya biashara. U doing for funny
 
mkuu kwani hujui kanuni za kuendesha kampuni? au umeajiri ndugu? kama umeajiri ndugu na washikaji fanya roho ngumu tu .. kampuni yeyote ni after profit making sasa kama wewe unaendesha biashara expenditure inazidi mapato haloo jichunguze upya .. angalia vodacom , tigo na makampuni mengine yanafanyaje? jifunze kwa wenzio
 
Chamsingi inatakiwa ubaject all running costs halafu uone kama production itazidi running costs ,hakuna haja ya kung'ang'ania kuwa na wafanyakaz wengi wakati biashara hairuhusu.
 
Change your strategic plans. Punguza wafanyakazi na working plan ibadilishwe.
 
Pale running cost inapokuwa Higher than a profit made.... iyo ni dalili ya kufilisika mkuu" so kama kuna uwezekano punguza waajiri..ili atleast upate pesa ya bia kila siku
 
Huyu anapata faida ila faida haikidhi matumizi yake baada ya kuwalipa wafanyakaz na rent ya hapo alipo,,,so anabakiwa na kdgo sana,,,ila ndugu ungesema unafanya kitu gan nadhan tungeweza kuona unapokosea ni wapi maana inawezekana mwanzo kuna gharama ambazo ulikua hulipi ila sasa hiv inakulazmu kulipa ili uendelee kuwepo hapo,au kuna kodi ulikua unakwepa na serikali hii imeamua kukomaa so unaona kama hupat chchote....sema usaidiwe
 
Dah.... Ushauri gani Unataka? Kama wewe hujui gharama za uzalishaji/uendeshaji......hujui mauzo..... hujui bajeti yako.... nani atajua? Jaribu kumuona Profesa mshana jr akusaidie kuzindika biashara yako
 
Jipange upya ndugu.

Ni lazima upunguze matumizi yasiyo ya lazima kwanza...kama kuna magari yanaingia road tu pasipo lazima acha na tafuta njia nyingine..kama kukodi gari ni rahisi kuliko kuliendesha basi bora ulikodishe.

Kuwa mkali kwenye kudai wadeni wako..pesa zisilale nje...usikubali mtu aue kampuni yako...bora yake ndo ife..kama unamdai mng'ang'anie hadi alipe.

Wachana na huruma hizo...kama utashindwa zipo kampuni zinazotoa huduma za management...zitafute kuna kampuni nyingi tu za Human Resource Solutions...call them waeleze watakusaidia katika hilo...hilo jambo sio kubwa kwao..

Nikisema huruma namaanisha ni lazima ufanye retrenchment..kama umewaajiri na mikataba tafuta mtaalam wa sheria ya kazi mweleze kuhusu retrenchment yaani kupunguza wafanyakazi kwa kuzingatia sheria ( hapa pesa lakini inahitajika)

Laa sivyo utafunga virago.
 
Ndugu nadhani la msingi unalopaswa kuangalia ni ku adopt mazingira ya biashara kwa sasa.

Fanya kupunguza gharama ikiwezekana kwa kupunguza wafanyakazi na gharama nyingine zinazowezekana kupunguzika.

Vile vile jiweke sawa kwenye records zako ili TRA wajue hali ya biashara yako kuwa unapata hasara maana kodi hautalipa kwa mujibu wa sheria....

Jitahidi usifanye biashara kwa mazoea ya kipindi cha nyuma maana huu ni wakati mwingine na tuko chini ya kiongozi mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…