Mimi naamini hakuna mtanzania asiyelipa kodi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Juzi nilisikia kamishna TRA wakidai watanzania milioni 3 kati ya milioni 45 ndio wanaolipa kodi. Ni jambo ambalo halikubaliki tena kauli hii inapotolewa na wataalamu wa kodi inasikitisha maana kauli hii ingetolewa na layman.

kila mtanzania analipa kodi ila kwa viwango tofauti.

kodi nyingi zimewekwa katika bidhaa hivyo kila mtu anaponunua bidhaa hulipa kodi.

sio haki kuwalinganisha watanzania katika PAYE wakati mapato yao ni tofauti.

kila mtu analipa kodi kulingana na anavyopata, hivyo hatua ya kwanza ni kupata kama hatuwezi kusikitika kuwa watanzania wanaopata vipato vinavyowawezesha kulipa kodi ni wachache hatustahili kulalamika kuwa wanaolipa ni wachache.

hivi kiongozi anayesimama kulalamika jambo kama hili kwanza ajiulize analipwa shilingi ngapi? alafu ajiulize ni watanzania wangapi wanaolipwa kiasi hicho anacholipwa yeye?

msingi wa kulipa kodi ni kupata hivyo kujiuliza tunatakiwa tuanzie kwenye vipato ili tuwawezeshe watanzania kupata fedha na ndio hapo wakishapata tujiulize kama wanalipa. hatuwezi kusikitikia kulipa kodi kama hatusikitikii watanzania kupata vipato duni.

wakati awamu ya tano imeingia madarakani kwa viwango vilevile vya kodi kwa kubana mianya ya ukwepaji kodi waliweza kupandisha ukusanyaji mapato kwa zaidi ya asilimia 60. lakini walipotengeneza bajeti walibadilisha viwango vya kodi na kuondoa vyanzo vingi vilivyokuwa vikiingiza mapato kwenye jamii na kuzunguka kutengeneza kodi.

watu wamelalamika lakini badala ya kusikilizwa na kutafakari hatua walizozichukua wao na kuangalia biashara hizi zinazozalisha kodi zimeathirika vipi, wamewajibu wananchi walizoea fedha ya bure. Lakini cha kusikitisha ni pale wanapoonekana kutegemea kukusanya kodi zilezile kwenye biashara chache zinazofanyika.

kugangania kukusanya kiwango cha kodi kilekile ni sawa na kumtwika mgonjwa mzigo bila shaka itakuwa ni kumuongezea machungu.

wataalamu kama hawa walitakiwa wawaambie Serikali ni wapi wamejikwaa na jinsi ya kurekebisha lakini inavyoonekana ni kutafuta mbinu za kulazimisha kufikia malengo ya kodi yaliyowekwa. Hawa wanaanza kudai ni watu wachache wanalipa kodi, na wengine ni kuibuka na maeneo mapya kabisa ya kodi kulazimisha watu walipe.

Serikali itafakari vizuri kama kodi zimepungua wabaini sababu na kuzifanyia kazi na sio kulazimisha kukamua kodi kwa nguvu maana kufanya hivyo wataathiri mzunguko wa fedha zaidi kwenye jamii.

Ni kwa bahati mbaya TRA wao ni wataalamu wa kukusanya kodi, wao wanachotazama ni kuongeza kiwango walichokusanya.

ni vema serikali iwe na taasisi inayoangalia uchumi kwa pamoja na sio kufikiri kukamua kodi tu bila kutizama watu wanapata nini na kwa njia zipi.
 
Walitakiwa kusema ni wawakilishi milioni 3 ndiyo wanaolipa kodi. Wawakilishi ni makampuni, viwanda, taasisi n.k kwani wao ndiyo wakusanyaji kwa walaji wa mwish ambao ndiyo walipakodi
 
Juzi niliweka uzi wa kuhusu jambo hili la Watanzania KUTOLIPA KODI.

Wewe unasema HUAMINI mimi NAAMINI maana kama Watazania WOTE walio na kipato wangelipa KODI zao nchi hii INGEENDELEA sana. Hivyo ni kusema kulingana na kauli ya Kamishna wa TRA ni aslimia 7.5% PEKEE ndo WALIPA kodi. Ndo maana Tanzania HATUENDELEI.

Swali TUTOE maoni TUFANYEJE ili KODI ipatikane? Si kuwaachia TRA peke yao kila mtanzania mwenye UZALENDO ana jukumu la kuchangia mawazo na IDEAS.
 
Watanzania wote wanalipa kodi- Full stop Acheni bla bla bla

Kwa sasa TRA imeshindwa kufikia malengo kwa sababu uchumi umeshuka,..kipato cha mtanznaia kimeshuka...Thamani ya shillingi imeanguka sana,...mfumuko wa bei..ajira hakuna....nchi inayumba

TRA wanabwabwaja ujinga....Watanzania wa leo wameelimika

Wewe Mtanzania,.....unalipa kodi ila hujui unavyolipa

A - Wafanyakazi wote wanalipa kodi kwa PAYE

B - Wafanyabiashara na Makampuni - Kodi ya MAPATO (faida ya kampuni) Corporate tax

C- VAT hiii ni Kodi inayolipwa na Watanzania wote

Sasa hawa TRA Waje watuambie Hii kodi ya VAT tunayolipa kila ukinunua bidhaa inaenda wapi?

Ukinunua Soda, chumvi, sukari, lotion, mkate, diesel, petrol etc tayari umelipa kodi ya VAT

Tunataka fikra chanya jinsi ya kukuza uchumi...acheni siasa na propaganda
 


Kuna siku hata mimi niliwahi uliza swali hili na ilikuwa seminar moja na hawa watu wa mamlaka maana nilikuwa nasikia msururu wa kodi.niligundua kuwa kumbe kodi inategemeana na shuhuli na kipato.nilielekezwa mfanyakazi chini ya laki na sabini kwa mwezi sheria imemsamehe,mfanyabiashara anayezungusha na kupata chini ya milioni 4 kwa mwaka naye kasamehewa.sikuwa nalijua hilo.kumbe hata VAT kuna wafanyabiashara hawalipishi wanadai ni wale mzunguko uliofika milioni mia moja kwa mwaka au kama huyo mfanyabiashara ataweza kufikia kiwango cha milioni hamusini kwa muda wa miezi sita.jumatatu nataka watembelea nijifunze zaidi unajua ukivijua hivi unapiga biashara bila kuwaogopa ni kupiga hesabu tu za manunuzi na matumizi na mauzo.
 

kila bidhaa imewekewa kodi hivyo kila anayetumia bidhaa za kununua analipa kodi kupitia bidhaa hiyo. hebu nieleze hao milioni 42 wanatumia bidhaa gani hizo zisizolipa kodi?

swala la nchi kuendelea ni swala mtambuka kuliweka kwenye kodi ni kufocus pafupi sana.

kila mtanzania analipa kodi na dhana hizi za watu kudhani mataifa yaliyoendelea wameendelea kwa kulipa kodi ni upofu wa hali halisi. hakuna sehemu unaweza kutegemea maskini alipe kodi kama tajiri hivyo matajiri wanalipa kodi kubwa kwa sababu ya vipato vyao vikubwa.

yeyote mwenye mawazo ya kudhani ili tuendelee ni kuwafanya masikini hawa walipe kodi kubwa kama wanazolipa matajiri hawezi kuwakomboa maskini hawa. kinachotakiwa ni mpango wa kuanzia hapo masikini walipo kutumia kodi zao ndogo kuchochea vipato vikikua unapandisha na kodi unachochea tena vipato, hivyo hivyo jamii inatembea taratibu kutoka chini kuelekea juu.

hatuwezi kuangalia maendeleo yetu kwa dhana ya kodi bali mchakato mzima wa tunapanga kufanya nini na fedha zinapatikanaje tukizingatia halihalisi za watu.
 


Hawa jamaa nashindwa kuwaelewa, wamerundika kodi kibao mpaka biashara zinakufa sasa wanawambia watanzania kuwa only 3 millioni out of 45 ndio wanalipa kodi, tafsiri ni yake ni kila anayelipa kodi kujifikiria kuwa yumo ndani ya 3 millioni na wao ndio wanalipa tu while 42 hawalipi unategemea nini? ni kila anayelipa kodi kuona anaonewa kwa nini asiwe mmoja wa wakwepa kodi. Yaani kauli hizi zinahamasisha ukwepaji kodi.

huwezi kuwaambia watu walipe kodi kwa hiari and then kesho unawaambia wanaolipa kodi ni millioni 3 tu na wengine hawalipi alafu watu wajitokeze kulipa kodi.

kwanza wanasema uongo maana hata mtoto mdogo kabisa chekechea akinunua pipi analipa kodi kupitia pipi yake na uongo wao unaweka mawazo hasi kwa wananchi juu ya ulipaji kodi kwa kila anayelipa kujiona anaonewa na kuona kama 42 millioni hawalipi kwa nini na yeye asiweke fedha hiyo mfukoni?
 
Huna ajira, huna hela , unanunua bidhaa gani wkati hata viroba unabomu
 
Kwel mkuu kulipa kodi sio lazim uwe katika sekta rasmi suala la ni hatuna strategic nzur mfano mzur wa kodi za magar ambazo zinavuwa hadi asilimia 100 pia duplicate tax nalo ni tatzo!
 
Mkuu, ninakuelewa sana. Lakini ni lazima tujue kuwa hatuwezi kutenganisha maendeleo na HELA. Hela ikiweko MIPANGO iliyopangwa intimilika. L akini pia NAKUBALIANA nawe kuwa MASKINI hawawezi kuongezwa mzigo mwingine maana HAWANA.

Sasa Ego ikiwa asmilia 7.5 pekee jamani tufanye namna gani ili tutoke hapo?
 


huu ni uongo kusema only 7.5 ndio wanalipa kodi peke yao.

pili wao ndio wanaandaa sekita zipi zitozwe kodi na serikali ndiyo inatakiwa kuweka mifumo ya kuwarahisishia kukusanya kodi.

mpaka leo wakisema kurasimisha sekita zote wao wanawaza fedha kwanza na sio kuwaza kutimiza wajibu ili iwe nafuu kutoa huduma na kukusanya pesa kwa ajili ya kutoa huduma. wakiambiwa kurasimisha wanachukualia simple wanaandaa project za kupiga dili wakiwapa watu utambulisho eti ili walipe kodi katika uholela wao huo na bado inakuwa ngumu kwao kumonitor.
 
Kwel mkuu kulipa kodi sio lazim uwe katika sekta rasmi suala la ni hatuna strategic nzur mfano mzur wa kodi za magar ambazo zinavuwa hadi asilimia 100 pia duplicate tax nalo ni tatzo!

Ukiagiza gari wafwaaa

Maana kuna Kodi kama 4 hivi

A - Kodi ya uchakavu

B- Kodi ya Import duty

C- VAT

D...etc
 
Huna ajira, huna hela , unanunua bidhaa gani wkati hata viroba unabomu

Ajira hakuna....sekta za utalii na bandari zimedumaa

kipato cha mwananchi kimeshuka na purchasing power imepungua...sasa lazima serikali ikose kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…