S V Surovikin
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 13,963
- 34,091
Mimea sita yenye sifa za kushangaza zaidi duniani
Mmea huu hutoa harufu ya mzoga
Duniani huwa kuna mimea ya aina nyingi, lakini kunayo baadhi ambayo inashangaza kwa sifa zake za kipekee. Hapa, tutaangazia sita kati ya mimea hiyo na kukueleza ni kwa nini ni ya kushangaza.
Ua la Mauti
Ndio mmea unaochanua maua makubwa zaidi duniani. Kwa kisayansi mmea huo hufahamika kamaUa la Mauti huwa kubwa sana
Rafflesia arnoldii na hukua kwenye misitu yenye mvua nyingi maeneo ya Sumatra na Borneo.
Ukiutazama unaweza kudhani ni mmea kutoka sayari nyingine.
Ua lake linaweza kuwa na upana wa mita moja. Mmea huu huwa hauna majani, miziz au shina. Mmea huu hupata virutubisho na maji kwa kuinyonya mimea mingine.
Ua la mmea huu huvunda sana, hutoa harufu sawa na ya mzoga. Ndio maana huitwa Ua la Mauti.
Mmea huu huvutia wadudu wa kusaidia katika kuchavusha.
Bingwa wa kukua haraka
Panda kwa jina la Meng Meng akila mianzi katika kituo cha kuwatunza wanyama Berlin
Mianzi ndiyo mimea inayokua kwa kasi zaidi duniani. Baadhi ya mianzi inaweza kukua kwa hadi sentimita 91 kwa siku. Hii ni karibu mita moja.
Kwa kulinganisha, mtoto wa miaka minne kwa wastani hukua kwa sentimita 6.5 kila mwaka.
Mmea huu hupendwa sana na wanyama aina ya panda ambao huutumia kama chakula.
Mmea usiohitaji jua
Mmea kwa jina Western Underground Orchid ni miongoni mwa mimea michache sana duniani ambayo huchanua maua yak echini ya ardhi.Mmea huo hukua chini ya ardhi na maua yake ya rangi ya krimu na waridi hukomaa na kuchanua sentimita chache chini ya ardhi.
Ukikasibia sana, mmea huo hufika sentimita mbili chini ya ardhi.
Tofauti na mimea mingine, mmea huu huwa haupati nguvu zake kutoka kwa jua. Badala yake, hutoa virutubisho vyake kutoka kwa kuvu na mimea mingine inayoota karibu. Mmea huu huwa hauna klorofili: kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea ambayo hutumiwa na mimea katika kusanidi nuru na kutengeneza chakula.
Mmea huu huwa adimu sana, na hupatikana maeneo ya Australia Magharibi pekee.
Mmea unaowameza wadudu
Umewahi kusikia kuhusu mmea unaokula nyama? Kuna aina kadha za mimea duniani ambayo huwanasa na kuwala wanyama na wadudu. Moja ni mmea kwa jina Venus Flytrap ambao hupatikana Carolina Kaskazini na Kusini.
Mimea hii huwanasa wadudu na kuwafunikia dani kisha kuwameng'enya.
Majani ya mimea hii hufanya kazi kama mtego kutokana na vinywele ambavyo huwa juu yake. Vinywele zaidi ya viwili kwenye jani vikiguswa kwa pamoja, jani hilo hujifunika ghafla kwa kasi ya chini ya nusu sekunde. Kisha, mmea huo hutoa kemikali za kumeng'enya mdudu polepole kwa siku kumi hivi. Baada ya kumaliza, jani hilo hujifungua tena.
Venus Flytrap hutumia virutubisho kutoka kwa wadudu hao kuongeza kwenye virutubisho ambavyo havipatikana kwenye mchanga. Mmea huu bado huwa na uwezo wa kusanidi nuru kama mimea mingine.
Mimea ina hisia?
Ni kweli mimea ina hisia? Ni vigumu kwani haina mfumo wa neva, lakini utashangaa ukikutana na mmea kwa jina Mimosa pudica, au mmea wa hisia.
Mimea hii ina majani ambayo 'hujikunyata' yanapoguswa, kutokana na kunyimwa maji na mmea wenyewe. Hii huaminika kuwa njia yake ya kujikinga dhidi ya wanyama wala nyasi na majani. Wanyama wakubwa wanaweza pia kutiwa hofu na kujikunyata ghafla kwa majani hayo, huku wadudu hao kukiwa na uwezekano wanaweza kuangushwa jani likijikunja.
Mmea wenye sumu kali
Manchineel
Kuna mimea mingi inayoweza kumdhuru mtu au wanyama wengine, kwa kuwa na sumu. Lakini mmea mmojawapo wa ile hatari zaidi ni manchineel unaopatikana maeneo ya Amerika Kusini na Amerika ya Kati na maeneo ya kusini zaidi ya Marekani.
Mmea huo huwa na majimaji ya rangi ya maziwa ambayo humdhuru mtu akiyagusa. Ukigusa jani lake pia litakuchoma na kukusababishia vidonda, itakuwa ni kama umejimwagilia maji moto.
Watu hushauriwa pia kutojikinga mvua chini ya mimea hiyo kwani maji ya mvua yanaweza kuchanganyikana na majimaji yake na kuwasha sana. Mmea huo ukichomwa, moshi wake unaweza kumpofusha mtu kwa muda na hata kusababisha matatizo ya kupumua.
Tunda la manchineel lina muonekano wa tufaha lakini lina sumu kali. Linaweza kumfanya mtu kukosa maji sana mwilini kiasi cha kufariki na pia kuumwa sana na tumbo.
Imeisha hiyo