Salaam wakuu, kila siku huwa napita maeneo haya lakini sijawahi kujiuliza swali hili. Bahati mbaya au nzuri tulipita maeneo haya na mdau mmoja tukapata wazo fulani lililopelekea kujiuliza sehem ya kuanzia. Je sehem hii ya bonde la ufa iko chini ya milki ya nani? TANAPA wanahusika, au mamlaka nyingine, au ni mapori ya wazi tu, au kuna mtu/watu/taasisi inamiliki vipande vya ardhi? Kuna shughuli tunaangalia uwezekano wa kuifanya kwenye maeneo haya ya kuvutia. Pia kwa vile Tanzania ni kubwa naomba mawazo yenu wadau, ni maeneo gani tena yaliyo na milima na mabonde makubwa na yenye kina kikubwa, kukiwa na maporomoko ya maji, mito, au kingo za ziwa/bahari ni nzuri pia.
Natanguliza shukrani.
Au aende Mwanza, town yote ni milima.Pita njia ya iringa mjini kwenda Dodoma kupitia mtera ,utakutana na milima mikali inayoitwa Nyang'oro
Ardhi yote TanZania ni mali ya Serikali na chini ya usimamizi wa Raisi wa JMTZ!
Umeamua kabisa kukandamiza kwa lugha ya kwenu!natamani kwenda mwanza nione hiyo imilima na mawe wanayosema ni ajabu sana
Uongo mtupu
Soma Land Act vizuri
s. 4. All land vested in the President as trustee
(1) All land in Tanzania shall continue to be public land and remain vested in the President
as trustee for and on behalf of all the citizens of Tanzania.
Mzee Tupatupa
Nadhani unahitaji elimu ya uraia ili utambue haki zakoArdhi yote TanZania ni mali ya Serikali na chini ya usimamizi wa Raisi wa JMTZ!