Wadau amani iwe kwenu.
Nina dada yangu aliekuwa na mchumba aliepatana nae wakiwa chuo kikuu huko Dar Es Salaam.
Baada ya chuo kila mmoja akaenda njia yake kurudi makwao likizo.
Bahati nzuri wote wakaajiriwa mwaka ule Mhe Magufuli anagombea kwenda Ikulu, mahali patakatifu kabisa.
Baada ya ajira na kujiridhisha kimaisha wakakubaliana kutambulishana rasmi kwa maana ya kijana kupeleka kishika uchumba.
Akafika nyumbani kwa wazazi wa binti na kupokelewa vizuri. Taratibu zikakamilika. Akaja kupewa jibu mahali ya binti ni sh mil 2.5. Kijana akakubali, akarudi kwao huko mkoa wa misitu. Baada ya muda akaleta mahari kama ilivyo kubaliwa.
Tukaja kushtuka mahusiano yao yanadorora sambamba na afya ya binti kudorora kwa sababu ya stress. Kuulizia kulikoni. Kumbe kijana anamfanyia visa mwenzie. Na uchumba wao kwishney. Hatujui sababu ni nini hasa!!!
Tuyaache hayo. Mimi mwenyewe sitaki kabisa kusikia habari za harusi, nimevuta binti awe mke wangu, kama tulivyokubaliana kwamba tukae pamoja angalau mwezi kabla ya kutangaza ndoa rasmi. Hii ni kwa sababu mimi nakaa mbali sana toka mkoa wa nyumbani. Binti mwenyewe ni yatima, hivyo maisha yake ni kutanga tanga tu, Mara akae huku, mara kule.
Sasa sekeseke limeibuka, wazazi walezi wa binti wamesikia binti yao yuko kwa bwana ikyenja. Wameanza kudai pesa ya kujionesha sh laki nne, baadae ndipo nitaambiwa kiasi cha mahari. Mimi nakataa kutoa pesa hiyo maana naiona kama mahari yenyewe, kwa maisha haya ya vijijini ingawa mimi ni mfanyakazi serikalini. Nina maana sinunui mke bali natanua ukoo na kuendeleza undugu, ya nini kusumbuana. Ingawa kwa utamaduni wetu nawajibika kulipa na nitalipa kweli bila kinyongo.
Sasa nataka kuwaambia wazazi wote wenye tabia kama hizi waache maana huwafanya binti zao kukimbiwa.