Kuelekea 2025 Mikutano ya CCM inayoendelea kufanyika kwenye stendi za mabasi ni kinyume na taratibu. Tusigeuze stendi za mabasi kuwa viwanja vya mikutano ya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
15,380
21,172
Kumezuka mtindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya mikutano ya hadhara kwenye stendi za mikoa za mabasi. Leo katibu mkuu wa CCM ndugu Emmanuel Nchimbi ameongoza mkutano wa hadhara katika stendi ya mabasi mjini Babati mkoani Manyara. Jumatano tarehe 5 CCM wamepanga kufanya mkutano wa hadhara katika stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Sababu hasa za CCM kufanya mikutano yao maeneo ya stendi za mabasi sio utaratibu mzuri kwani wanakwaamisha shughuli za kawaida katika stendi hivyo na kuzuia wasafiri kupata huduma za usafiri kwa utaratibu uliwekwa kisheria na serikali.

Sina uhakika kama vyama vingine vya siasa vinaweza kuruhusiwa kufanya mikutano yao kwenye stendi za mabasi au hata masokoni.

Tunaomba vyombo vya kisheria kukemea utaratibu huu mbovu wa kugeuza stendi za mabasi kuwa viwanja vya kufanyia mikutano ya siasa.
 
Back
Top Bottom