OCC Doctors
Senior Member
- Jul 20, 2018
- 110
- 167
Tatizo la miguu kufa ganzi na kuuma linaweza kusababishwa na hali ya kukaa kwa muda mrefu kupelekea kupunguza mtiririko wa damu au kuweka shinikizo kubwa kwenye mishipa.
Kutetemeka na kufa ganzi kwa muda mrefu au isiyoelezeka kwenye miguu (paresthesia) inaweza kuashiria athari katika mfumo mkuu wa neva au ugonjwa wa neva wa pembeni.
Miguu kufa ganzi mara kwa mara kunaweza kuashiria ugonjwa wa kisukari, shida ya kusagika kwa pingili za mgongo, na pia inaweza kuwa ishara ya ujio wa kiharusi.
Dalili ambatana ni pamoja na Maumivu katika mguu ulioathirika, wasiwasi, maumivu ya mgongo, miguu kuwaka moto, kuwashwa, shida ya kukaa sawa au kusimama na udhaifu wa miguu.