Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 46,618
- 66,801
Nikirejea namna vyama vikubwa viwili Tanzania vinavyoteua wagombea wake wa nafasi za uchaguzi hasa za Urais ni wazi vigogo wachache wa vyama wamehodhi mchakato wa kupitisha wagombea wao badala ya wanachama.
Utaratibu sahihi wa uteuzi katika demokrasia halisi na zilizokamaa ni chaguzi za wagombea kupitia wanachama wote au wajumbe walio wengi.
Kinachofanyika ndani ya CCM na CHADEMA cha zinazoitwa kamati za maadili na kamati kuu kuchuja wagombea kabla hawajapigwa kura na wanachama au wajumbe walio wengi mfano katika mkutano mkuu au Halmashauri kuu ni sawa na kutanguliza mkokoteni mbele ya Punda anayeuvuta au kuanza kuweka unga kwenye sufuria kisha maji ya kusonga ugali baadaye, kitakachopatikana hapo kitakuwa ni kituko tu.
Haya mambo ndio yaliyosababisha Lowassa kuwa muathirika mara kadhaa ndani ya chama chake akinyimwa fursa ya kuchaguliwa bila kupewa sababu, Mwenyekiti na kamati yake ya maadili hawapaswi kuwa na nguvu kubwa kiasi hicho cha kuamua nani atapata fursa ya kupigiwa au kutokupigiwa kura na wajumbe.
Pia hili jambo ndilo lililoivuruga CHADEMA wakati Lowassa alipohamia huko. Kama Lowassa angeshindanishwa kwa kura za wanachama wote au wajumbe walio wengi kwanza dhidi ya wagombea wote akiwemo Slaa CHADEMA ingeenda katika uchaguzi kikiwa chama tulivu kwa sababu mchakato unegeonekana huru bila vigogo wa chama kumbeba mtu.