Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,432
Serikali imeitaka mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kuacha ujanja ujanja badala yake ijikite kulipa mafao kwa wakati kwa wanachama wao wanaostaafu ama kuachishwa kazi.
Imeitaka mifuko hiyo kutowazungusha na kuwapa usumbufu usiokuwa wa lazima wanachama wanaofuatilia mafao yao.
Vilevile, serikali imewataka wakurugenzi wa mashirika hayo kuchukua hatua na 'kuwatumbua' wafanyakazi wao hususani mameneja wa mikoa kwa kuwa wanafanya kazi kwa mazoea na wamekuwa wazembe kazini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, alitoa maagizo hayo jijini hapa alipofunga semina ya viongozi wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (TSSA).
Mhagama alieleza kushangazwa na kitendo cha wafanyakazi wa mifuko ya hifadhi kuwadai barua za miaka 40 nyuma wanachama wao wanaostaafu kama moja ya vielelezo.
''Mtu ana miaka 60 na amestaafu, leo anakuja kufuatilia mafao yake, mfanyakazi wa mfuko wa hifadhi unamdai barua ya miaka 40 nyuma, sasa ataipata wapi? Matokeo yake mnaanza kuwasumbua tu watu na kuwazungusha,'' alionya.
Mhagama alisema moja ya kazi za mifuko hiyo ni kuweka kumbukumbu za mfanyakazi ambaye ni mwanachama wao kabla ya kufikia umri wa kustaafu, ili ukifika wakati alipwe mafao yake bila usumbufu.
Aliongeza kuwa kazi hiyo inatakiwa kufanywa na maofisa utekelezaji ambao na wanalipwa mishahara, akibainisha kuwa malalamiko ya wanachama katika eneo la mafao yamekuwa mengi.
Kuhusu 'utumbuaji' wa wafanyakazi, Mhagama alisema siku hizi hasikii watu wakiwajibishwa kama ilivyokuwa mwanzo licha ya kuwapo watumishi wazembe wasioendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Akizungumzia suala la uwekezaji kwa mifuko hiyo, waziri huyo aliwataka watendaji wa mifuko hiyo kuwa makini ili wawekeze kwa faida badala ya kuingia mikataba mibovu kama ilivyotokea siku za nyuma.
Aliwataka watendaji na wenyeviti wa bodi za mifuko hiyo kuwa makini na suala hilo ili kusaidia nchi kujenga uchumi na kuinua maisha ya Watanzania.
Mhagama pia aliitaka mifuko hiyo kufanya tathmini ya kina ili kuongeza wanachama kwa kuwa kwa sasa ni asilimia 4.3 pekee ya watumishi ndiyo wanachama wao.
Aliongeza kuwa asilimia 56 ya vijana wote hawako katika mifuko na kwamba kuna haja ya kuongeza nguvu katika upande huo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TSSA, William Erio, akizungumza katika semina hiyo, alisema mifuko hiyo ipo tayari kushirikiana na serikali katika kuwekeza hususani kwenye viwanda.
Alisema mifuko yote imeanza kuchukua hatua na kwamba suala hilo litaleta tija kwa nchi na wanachama wao ambao wanachangia michango yao.