Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,663
Kwenye nchi zenye demokrasia iliyostawi , harakati za kuomba kuteuliwa kuwa Rais huanzia ndani ya Chama , ambako wagombea wote wanaotaka kupeperusha bendera huwa na midahalo ya wazi juu ya masuala mbali mbali , na hurushwa LIVE , huu ni ustaarabu mzuri kwakua mgombea atakayepita anakua amepimwa na wanachi hasa wanachama wa chama husika. Midahalo huwa zaidi ya mmoja na inaweza kufanyika kwenye kanda mbali mbali mfano Pwani,Kati,Nyanda za juu etc
Katika ushindani hufikia mahali baadhi ya wagombea wakajitoa na kuamua kumuunga mkono mgombea mmoja , na kufikia mkutano mkuu wa chama husika kila mmoja anakuwa anajua kwa hakika nani atakua mgombe .
Pakiwa na uwazi wa namna hiyo ndani ya chama husika ni rahisi sana na vyama vingine kuiga ustaarbu wa namna hiyo ....pia itapelekea kuwa na mdahalo wa wagombea urais uchaguzi mkuu, Mdahalo ni jambo jema kwani mwaka 1995 Mkapa amekiri hadharani kuwa ule mdahalo ndio uliomsaidia sana kuweza kushinda kwani kabla ya mdahalo akakiri uugwaji wake mkono ulikuwa mdogo hasa dhidi ya Mrema., alijieleza vizuri watu wakamkubali ...huku Mrema aliyekua tishio akishindwa kabisa kuelezea sera zake
Pascal Mayalla kaka yetu anakumbuka sana mambo ya midahalo na kipindi chake cha KITIMOTO pale bilcanas chini ya MASAI STUDIOS
Kwakua tayari Chadema wameonyesha uwazi kwenye utamaduni mzuri wa kutangaza nia tunaomba waende mbele zaidi wafanye midahalo ....na iwe LIVE .
Tunawatakia wagombea wa vyama vyote heri na fanaka kwenye harakati za 2020