MiCCM mijitu mihabithi kweli, eti kujengewa vibarabara vibovu na vimeli vya mitumba ndio wanaona maendeleo.
Hakuna hata mzanzibari mmoja anaefurahia visiwa vile vilivyo sasa, kama si punguani wa kisonge huwezi kukubali kuwa zanzibar ina amani na utulivu, wazanzibari wenye akili zilizosalimika wanasikitishwa na aina ya uongozi ambao CCM Dodoma inawaletea kila baada ya miaka kumi.
Zanzibar siasa imeshindwa kuleta maendeleo na mshikamano, wanasiasa sio wa upinzani wala hawa wanaojiita walatawala, wote ni wachumia matumbo yao na kujinufaisha na familia zao.
Mashehe na viongozi wa uamsho wamewekwa ndani, baada ya kudhihirika kuwa wanawaumini wingi wanaowakubali na kuwafuata kuliko siasa na vyama vya siasa vyote, vyama vya siasa ndivyo vinavyoleta mgawanyiko katika jamii ya wazanzibari, na laiti mungewaacha waendelee na shughuli za kufanya mihadhara ya uamsho na kushajihisha kuipigania zanzibar iliyohuru, hakuna hata chama kimoja kingebaki na wanachama wenye msisimko katika kusimamia sera za chama husika.
Wazanzibari wanaijua ajenda wanayoitaka, na popote walipo huwa wanajisikia kuitetea ajenda ya "Zanzibar yenye mamlaka kamili kisiasa, kijamii na hasa kiuchumi", na hii ni baada ya serikali ya kitanganyika kupitia ccm na mawakala wao wenye hisia mbaya za kuiweka zanzibar chini ya mamlaka ya kitanganyika kuzidisha njama na matendo yao ya kuidhalilisha zanzibar kiuchumi kitendo kinachoamsha hisia za kiharakati kwa wazanzibari.
Laanatullah CCM