Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Muda huu kuna mhubiri wa Injili, Daudi Mashimo aka Komandoo wa Yesu, anaendelea na mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo akiwataka wanaojiita manabii nchini Tanzania waache mara moja kujiita hivyo kwa sababu unabii unatoka kwa Mungu na kwamba nabii wa kweli atakuja wakati utakapofika.
Amewapa siku 14 watubu, vinginevyo yuko tayari kutoa hadharani siri zao na nguvu wanazozitumia kwa sababu wanachofanya ni utapeli wa kiroho na kuwapotosha watu.
"Watanzania wengi wana hali ngumu kimaisha, sasa hawa matapeli wa kiroho wanatumia fursa hiyo kuwahadaa na kuwapotosha, nawataka waache mara moja vinginevyo baada ya siku 14 nitatoa siri zao na jinsi wanavyotumia nguvu za miujiza za 'Mngindo' ambazo ni za kichawi," anaeleza.
Komandoo sio muharifu, na wala sio muuaji. Ila yote kwa yote wanajiita makomando, wanajifananisha ushupafu ambao makomandoo wanao.Komandoo ni mtu anayefanya kazi za mauaji ya ukatili na uharibifu mkubwa, sasa anapojiita kuwa yeye ni komandoo wa yesu sijui ana maana gani, wote hao ni matapeli tu
.......... kama yule Nabii Bilionea ! Wagalatia mnapenda mzaha ...... mpaka na Mungu !?Maadamu mtumish anahubiri kwa kufuata biblia na anahubiri maneno kutoka kwenye biblia na akanipa unabii na ukawa wa kweli mimi sina shida hapo na huyo nabii.