Mheshimiwa Rais, nakukumbusha ahadi yako ya kushusha bei ya vifaa vya ujenzi!

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Nakukumbusha mh rais, moja ya ahadi zako kubwa ulizotoa wakati wa kampeni ni kutupunguzia bei ya vifaa vya ujenzi ili sisi masikini tunaoishi kama mashetani tuweze kujitengenezea vibanda vyetu vyenye utu kidogo vya kuishi.

Ni muda sasa sijasikia sio waziri wako wala wewe ukizungumzia mikakati ya kutekeleza hilo. Bajeti ya wizara ya ujenzi na pia ile ya viwanda zimepita bila kulizungumzia hili.

Tunaomba Rais utuambie hii ahadi utaitekeleza lini ili na sisi wanyonge tuweze kuishi kama binadamu, kwa kuachana na maisha ya kijima ya kuishi kwenye nyumba za tembe?!

Ni mimi mpiga kura wako ninayekupenda sana na kukufagilia sana kwa utendaji wako!
 
Hizo ahadi nyingi zilitolewa kama sehemu ya kuwin kura kwani aliogopa wapinzani wangeweza kuitumia ahadi hiyo na kukipunguzia chama chake kura. Hizo zinaitwa ni ahadi za kwenye majukwaa ya siasa, huwa hazina nguvu sana.
 
Nahisi wanaanza na viwanja vya bei elekezi
Naomba usiishie kama ada elekezi ya shule
 
Angalau akili zinakurudia,Magufuli ndiye Raisi.
 
Angalau akili zinakurudia,Magufuli ndiye Raisi.
Mimi particle ndogo tu, nina ubavu gani wa kukataa urais wa Magufuli hata km alipewa na tume na vyombo vya dola? Si katiba inasema akishatangazwa hakuna mtu snaweza kuhoji duniani na mbinguni?. I love my beautiful country, Tanzania_!
 


Apunguze bei ya sukari kwanza. Sukari mtaani inazidi kupanda bei alafu mnatuletea story nyingine.

Asije akatoa bei ekelekezi huku tena alfu bei ikapanda mara dufu.
 
Tutafika tu huko kwenye simenti bado tunamalizia kushughulikia sakata la sukari.Tunaomba muwe na subira wananchi.
 
Mhhh!Ukweli mcfm40 hautopita bila nami kukuunga mkono kwenye hili!Bahati mbaya sisi wengine hatuna uwezo wa kuanzisha thread zetu tangu walipoanzisha huu mfumo mpya wa jf,sijui yatokana vimeo!?Tumebaki kuwa wachangiaji wa hoja tu.Mh:Magu hata kama unayonia njema,elewa ya kwamba tangu uingie madarakani hakuna cha unafuu wa bei za bidhaa za viwandani bali vimepaa kwa bei maradufu unafuu upo kwenye mafuta ya vyombo vya moto tu!Nipo kanda ya ziwa na ni mwenyeji sana na maeneo unayotoka, hali huku ni mbaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…