DOKEZO Mhe. RAIS, Rudi tena RITA! Ukiritimba wa Huduma ambayo ilipaswa iwe BURE

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
595
Huduma yeyote ile inayoiwezesha jamii husika kupata huduma nyingine, ikicheleweshwa kwa jamii, Maendeleo kwenye nchi huwa yanachelewa au yanaenda Taratibu.

NARUDIA!

"Huduma yeyote ile inayoiwezesha jamii husika kupata huduma nyingine, ikicheleweshwa kwa jamii, Maendeleo kwenye nchi huwa yanachelewa au yanaenda Taratibu".

Jamii ikikaa siku zaidi ya moja kusubiri huduma fulani ifanyike ili waweze kuifikia huduma huduma muhimu wanayohitaji kwa wakati huo, huwa inaleta changamoto na lawama nyingi sana kwa serikali na Wakati mwingine hupelekea hata jamii kutohitaji tena kupata huduma lengwa kwa sababu tu kuna mlolongo unacheleweshwa kwa ajili ya kuifikia huduma nyingine.


Kumekuwa na utaratibu wa kufanya Verification kwenye mfumo wa vyeti vya kuzaliwa vinavyotolewa na RITA lakini verification hizi zinagubikwa na wingu ambalo halieleweki nini sababu ya kufanya verification kila utakapohitaji uhakiki wa cheti chako.

Watu kuverify vyeti vyao ambavyo vimetolewa na RITA kwa sababu tu, wanataka kwenda kupata huduma ambayo inahitaji cheti cha kuzaliwa, tena kula sehemu watakayotaka verification lazima uombe tena, yaani verification namba 1 huwezi itumia sehemu zaidi ya moja..

Kipindi kama hiki wanachuo wengi wanatuma maombi ya bodi ya mikopo, kabla hawajatuma wanatakiwa kufanya Verification RITA ambapo atalipa Tsh 3,000/= kesho akitaka kuomba huduma kwingine atatakiwa tena kufanya verification kwa kulipa gharama zingine tena. Kwa mwaka ukifanya verification mara 10 utakuwa umetumia Tsh 30,000 kuthibitisha nyaraka ambayo wameitoa wao wenyewe. Ni wazi pia zoezi hili linafanyika RITA manually ndio maana watoto wetu wanachelewa kupata Verification Number.

Najiuliza, Kitambulisho cha NIDA na cheti cha kuzaliwa kipi kina nguvu? Mbona NIDA ukishapata tu kitambulisho hakuna gharama zingine?

Rita walipaswa wawe na mfumo ambao mtu ataverify cheti husika kwa kuweka namba ya cheti au entry number na baadhi ya Taarifa kama inavyofanyika NIDA na sio kuweka gharama. Asilimia kubwa ya wanaoumia na hizi gharama ni wanachuo na watoto wa masikini, hata kama ni kiasi kidogo ila kinatengeneza ukiritimba na kuchelewesha watu kupata huduma.

Taasisi kama Rita inatakiwa iwe ya kutoa huduma na Sio biashara, kwa Hili Serikali inafanya Biashara kupitia RITA.

Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom