Mhe. Magufuli na majipu, wananchi na hali ngumu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Leo ni siku ya 104 ya utendaji kazi wa rais wangu Magufuli (sina namna hata kama sikumchagua). Kazi kubwa aliyoifanya mpaka sasa ni kutumbua majipu tu, mzee kasitisha shughuli zingine zote yeye yuko busy na majipu.

Na watanzania wenzangu walio wengi wamefunga midomo, wanacheka kimoyomoyo rais wao anatumbua majipu. Hii kwao ni burudani tosha.

Na kwa namna nijuavyo mimi Tanzania yangu ina majipu mengi kwelikweli, yaani safari ya siku 104 ya rais wangu ya utumbuaji majipu bado haiwezi kubadilisha chochote na kwa kuwa rais wangu ana nia ya dhati ya kuhakikisha majipu yanatumbuliwa basi inaweza kuchukua zaidi ya miaka yake ya dhamana ya kuongoza aliyopewa ili kumaliza majipu hayo.

Watanzania wanaoishi katika nchi yangu wamesahau kabisa shida zao. Gharama ya sukari, mafuta, pembejeo za ujenzi na kilimo, si hoja tena mbele ya wapumbavu wenzangu wanaoishi katika nchi yangu.

Wako tayari sukari kununua kilo kwa sh 4000, chumvi sh 1000, kilo moja ya nyama sh 12000, mafuta ya taa lita sh 6000 maana rais wao kipenzi yuko busy na majipu. Sisemi haya kwamba ndivyo yalivyo ila nabashiri tu. Pia nalinganisha na uwezo wa kufikiri wa watanzania wenzangu.

Mtaani huko husemi kitu kuhusu rais wangu, utapigwa mawe. Asante rais wangu maana mtego wako umeweka pazuri utavua samaki wengi.

Hata usipofanya kitu nina hakika 2020 watakuchagua kwa kishindo. Watanzania wameridhishwa na kasi yako ya utumbuaji majipu.

By mbunge nje ya bunge (nawaza tu)
 
rais wako lkn hukumchagua!!!! yule uliemchagua hakua rais?
 
Mkuu unakaribia kuminywa nini ss unakuja kutafuta huruma huku JF, nasikitika kukuambia kuwa hakuna lolote tunaloweza kufanya kwa ss.....we tumbuliwa tu.
 
Kama ulitarajia maisha kwa Watanzania yawe rahisi ndani ya siku zake 104 alizokaa madarakani basi huenda ulitarajia utawala wake ungeanza kugawa pesa za makusanyo ya TRA kwa wananchi kila mwezi vinginevyo, manake hata kama angeamua kutulimia mashamba ya mahindi kila mmoja bureee, bado na hayo mahindi yenyewe ingekuwa hatujayavuna!!

Hilo la kushangilia kila kitu hata nami linanikera-- yaani mpuuzi mmoja anayeishi Nambilanje na yeye tayari anajiona ni sehemu ya serikali mwenye wajibu wa kuunga mkono na kushabikia kila kitu huku akisahau alitakiwa kufanya hivyo wakati wa kumwingiza madarakani na hivi sasa kujitenga nae ili umminye vizuri atekeleze yale aliyoahidi lakini kinyume chake; unaweza kudhani wote hawa nao wanaishi Ikulu!
 
Ukishirikisha ubongo ungenielewa
 
rais wako lkn hukumchagua!!!! yule uliemchagua hakua rais?
Kura hazikutosha hivyo kwa mujibu wa katiba hawezi kuapishwa. Ila lazima ujue tunaomuunga mkono tulikua milion 6
 
Dalili ya Mvua ni Mawingu
 
Vitu vimepanda bei mara dufu. Tunaojitegemea tunajua hilo ndio maana inakua ngumu kushangilia maigizo. Wale wa kula kulala ndo wanapenda sinema. Hawajui hata bei ya kiberiti
 
Unataka kuniaminisha kuwa hapa Tanzania kuna ZIKA ya aina yake?!
 
Siku 104 sawa na miezi mitatu na siku 14/15 ni mapema sana. Tusubiri kwani hata hiyo hatua aliyofikia inatia matumaini.
 

Utakuwa umetumwa !
 
Ni mpumbavu pekee anayeweza kuhangaika kuhifadhi chakula stoo kabla ya kuua panya, au kujaza maji kwenye ndoo kabla ya kuziba matundu.

Anachofanya Magufuli kwa sasa ni kuziba matundu!
 
Ni mpumbavu pekee anayeweza kuhangaika kuhifadhi chakula stoo kabla ya kuua panya, au kujaza maji kwenye ndoo kabla ya kuziba matundu.


Anachofanya magufuli kwa sasa ni kuziba matundu.
Na mazingaombwe je ya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…