Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali atiwa hatiani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,330
12,950
Mahakama ya Wilaya Mbarali imemhukumu aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Joseph Werema Ndimila adhabu ya kulipa faini ya Tsh. 1,100,000/= au kwenda Jela mwaka mmoja na ameamriwa kurejesha kiasi cha sh. 4,000,000/= alichokifanyia ubadhilifu baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya Kutumia Nyaraka kwa Lengo la Kumdangaya Mwajiri, Kutumia Vibaya Madaraka na kosa la Kufanya ubadhilifu ambayo ni kinyume na vifungu vya 22, 31 na 28 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 R.E 2022].

Hukumu dhidi ya Ndimila imetolewa Julai 26, 2024 kutokana na shauri la Uhujumu Uchumi Na. 18/2023 lililokuwa katika Mahakama ya Wilaya Mbarali mbele ya Hakimu Mkazi Aliko Michael Mwandumbya, shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Sospeter Tyeah.

Ilielezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mashtaka tajwa hapo juu kwa kuandaa nyaraka za uongo za malipo (pay lists) akionesha kuwa aliwalipa watu mbalimbali kwa kukodi kumbi kwa ajili ya kufanya semina katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kulipa Jumla ya sh. 4,000,000/= huku akijua kuwa malipo hayo ni ya uongo na alilenga kumdanganya mwajiri wake na kujipatia kiasi cha sh. 4,000,0000/=

Aidha, Ndimila amelipa faini yote ya sh. 1,100,000/= na amerejesha kiasi chote cha sh. 4,000,000/= alichokifanyia ubadhirifu.
 
Kwanza Mbalali kuna ufisadi wa kutosha.
Kipindi cha kiangazi zinakusanywa pesa, mamilioni ya pesa kwa risiti feki.
Yote hayo yanafanywa yakiongozwa na mkurugenzi wao.
 
Mahakama ya Wilaya Mbarali imemhukumu aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Joseph Werema Ndimila adhabu ya kulipa faini ya Tsh. 1,100,000/= au kwenda Jela mwaka mmoja na ameamriwa kurejesha kiasi cha sh. 4,000,000/= alichokifanyia ubadhilifu baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya Kutumia Nyaraka kwa Lengo la Kumdangaya Mwajiri, Kutumia Vibaya Madaraka na kosa la Kufanya ubadhilifu ambayo ni kinyume na vifungu vya 22, 31 na 28 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 R.E 2022].

Hukumu dhidi ya Ndimila imetolewa Julai 26, 2024 kutokana na shauri la Uhujumu Uchumi Na. 18/2023 lililokuwa katika Mahakama ya Wilaya Mbarali mbele ya Hakimu Mkazi Aliko Michael Mwandumbya, shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Sospeter Tyeah.

Ilielezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mashtaka tajwa hapo juu kwa kuandaa nyaraka za uongo za malipo (pay lists) akionesha kuwa aliwalipa watu mbalimbali kwa kukodi kumbi kwa ajili ya kufanya semina katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kulipa Jumla ya sh. 4,000,000/= huku akijua kuwa malipo hayo ni ya uongo na alilenga kumdanganya mwajiri wake na kujipatia kiasi cha sh. 4,000,0000/=

Aidha, Ndimila amelipa faini yote ya sh. 1,100,000/= na amerejesha kiasi chote cha sh. 4,000,000/= alichokifanyia ubadhirifu.
Kama ameweza kutoa mil.5.1 chaap inamaana alichota zaidi ya hizo, karejesha kiasi kidogo sana cha faida aliyopata.
 
Na wezi wa kuku nao wawe wanaruhusiwa kurejesha kuku walioiba, badala ya kuwahukumu vifungo magerezani.
 
Back
Top Bottom