TANZIA Mhasibu jiji la Mwanza afariki ajalini akiwahi kwenye mazishi

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,662
8,787
Mhasibu wa Idara ya Mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Amon Joseph (41) amefariki dunia katika ajali ya gari akienda kwenye maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake, yaliyotarajiwa kufanyika leo wilayani Kwimba mkoani hapa.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu Jumanne Juni 4, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kifo cha mhasibu huyo akitaja chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva.

“Ni kweli imetokea ajali hiyo Saa 5:45, maeneo ya Kijiji cha Malembe Kata ya Igongwa Tarafa ya Ngudu Wilaya ya Kwimba kwenye barabara ya vumbi ya Mwabuki kuelekea Jojiro, gari aina ya Toyota Progress lililokuwa likitokea Mwabuki kwenda Ngudu ilimeacha njia na kutumbukia darajani na kusababisha kifo cha dereva (Amon),” amesema Kamanda Mutafungwa.

Awali, Ofisa Mawasiliano wa Halmshauri ya Jiji la Mwanza, Martine Sawema amesema Amon amefariki akiwa safarini kwenda kuhudhuria maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake Ngudu wilayani Kwimba.

Imeandikwa na Mgongo Kaitira
 
Pole yao wafiwa.

Ila watumishi wa umma wakiwa kwenye magari ya Serikali huwa wanakimbia mno huku wakiwa hawazingatia sheria zote za usalama wa barabarani.

Pia inawezekana kuna rafu zimefanyika dhidi yake ili kufunika kombe.

Yote ktk yote RIP
 
Mhasibu wa Idara ya Mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Amon Joseph (41) amefariki dunia katika ajali ya gari akienda kwenye maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake, yaliyotarajiwa kufanyika leo wilayani Kwimba mkoani hapa.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumanne Juni 4, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kifo cha mhasibu huyo akitaja chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva.

“Ni kweli imetokea ajali hiyo Saa 5:45, maeneo ya Kijiji cha Malembe Kata ya Igongwa Tarafa ya Ngudu Wilaya ya Kwimba kwenye barabara ya vumbi ya Mwabuki kuelekea Jojiro, gari aina ya Toyota Progress lililokuwa likitokea Mwabuki kwenda Ngudu ilimeacha njia na kutumbukia darajani na kusababisha kifo cha dereva (Amon),” amesema Kamanda Mutafungwa.

Awali, Ofisa Mawasiliano wa Halmshauri ya Jiji la Mwanza, Martine Sawema amesema Amon amefariki akiwa safarini kwenda kuhudhuria maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake Ngudu wilayani Kwimba.

Imeandikwa na Mgongo Kaitira
Njugu juu ya njugu. Ila hao ni wezi sana wa mali za umma acha afe tu.
 
Pole yao wafiwa.

Ila watumishi wa umma wakiwa kwenye magari ya Serikali huwa wanakimbia mno huku wakiwa hawazingatia sheria zote za usalama wa barabarani.

Pia inawezekana kuna rafu zimefanyika dhidi yake ili kufunika kombe.

Yote ktk yote RIP
Serikali inunue Toyota progress? Tangu lini mhasibu awe dereva Wa Gari la Serikali?! Usijibu Kwa hisia zako kichwani.
 
Back
Top Bottom