Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima, Martin Malera Ameitwa Polisi kutokana na taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti hilo wakati wa Mo Dewji kutekwa

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,440
32,253
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Martin Malera, ameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusiana na habari ziliozandikwa kwenye gazeti hilo kuhusu tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji. Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Neville Meena, amethibitisha na kusema wanafuatilia kwa karibu. #MtwnzaniaDigital

My take:

Wakuu hivi kumbe gazeti la musiba huwa linaandika mambo ya kweli? Kwa nini huwa hawafanyiwi kazi wale watu ambao linawamulika kwa matendo yao maovu yanayozua taharuki miongoni mwa wanajamii?

Kwa hiyo tumechagua kupuuza taarifa za musiba hazina madhara kwa Taifa?
 
Tumepata taarifa za Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Martin Malera kuitwa Polisi - Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuhusiana na habari ambazo ziliandikwa na gazeti lake wakati wa tukio la kutekwa Mo Dewji. Tunafuatilia kwa karibu!

mwandishi.jpg
 
Tulitegemea polisi watuambie wameshawafikisha watu wangapi mahakamani Mpaka sasa. lakini wanaendelea na maigizo yao.poor government kbs
 
Tumepata taarifa za Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Martin Malera kuitwa Polisi - Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuhusiana na habari ambazo ziliandikwa na gazeti lake wakati wa tukio la kutekwa Mo Dewji. Tunafuatilia kwa karibu!

View attachment 965585
Kama aliandika vitu anavyojua ni vzr ktk uchunguzi mwache aende akasaidie upelelezi sio kosa kuhojiwa mbona zitto aliitwa juzi takukuru.
 
Hii nchi ya ajabu sana, gazeti la Tanzania Daima, ambalo linaandika habari serious na za kiuchunguzi ndilo ambalo kila Siku linapata misukosuko!

Lakini gazeti la Tanzanite ambalo ni bimgwa wa kuandika habari za "uzushi" na porojo llemyewe lipo tu mitaani likiendelea na shighuli zake kama kawaida!
 
ni wajibu wa polisi kufanya kufanya uchunguzi au upelelezi kwa yeyote,....
.popote.
tutiii sheria bila shuruti
 
Back
Top Bottom