Mhandisi Nyamo-Hanga: Uzalishaji unaendelea vizuri, kuna upungufu wa Megawati 300-350 TANESCO

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,583
13,270
Naibu Waziri Nishati, Judith Salvio Kapinga amefanya ziara katika Kituo kidogo cha Kuzalisha Umeme kwa Gesi Asilia kilichopo Tegeta Jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 2, 2023
IMG-20231002-WA0027.jpg

Akizungumza baada ya kukamilisha ziara hiyo Naibu Waziri amesema Kituo hicho chenye mitambo mitano inayozalisha Megawati 43 ambapo ni Megawati 8.5 kwa kila mtambo.

Amesema mtambo mmoja kati ya mitano upo nje ya kituo kwa ajili ya matengenezo ya lazima ambapo unatarajiwa kurejeshwa hivi karibuni.
IMG-20231002-WA0023.jpg

Amesema “Hali ya uzalishaji inaendelea vizuri, nimewaelekeza TANESCO kuhakikisha matengenezo ya mitambo ya lazima yanafanyika kwa wakati na ndani ya muda mfupi.

“Pamoja na ukaguzi huo, nimewaelekeza kuimarisha huduma kwa wateja, wahakikishe wanatatua changamoto kwa wakati, yaani watoe huduma balimbali kwa wakati pindi kunapotokea hitilafu, wale wenye uhitaji wa kuunganishiwa umeme nao wapewe huduma.

“Kama kuna miundombi stahiki na kuna watu wameombahuduma basi wanatakiwa kupewa.”
IMG-20231002-WA0014.jpg

Kuhusu suala la kurejeshewa umeme kwenye makazi ya watu urudishwe ndani ya muda, pia sehemu zinazohusika na uzalishaji kuwepo na mazungumzo kati ya TANESCO na wawekezaji husika.”

Kuhusu changamoto ya gesi amesema zipo kadhaa na wanapambana nazo, lakini akagusia kuwa uzalishaji wa umeme kwa njia ya maji licha ya kuwa na changamoto kadhaa lakini ni wa bei rahisi ndio maana ni sehemu ya mipango ya kuzalisha umeme.

MKURUGENZI WA TANESCO
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akizungumza wakati wa ziara hiyo kwenye Kituo kidogo cha Kuzalisha Umeme kwa Gesi Asilia.
IMG-20231002-WA0040.jpg

Amesema “Kwa sasa Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) linashirikiana na Wizara ya Nishati tunafanyajitihada kuwa na umeme wa uhakika kwa ajili ya Wananchi kawaida na kwa ajili ya shughuli za uzalishaji pia umeme upatikane kwa gharama nafuu.

“Wiki iliyopita tulisema kwenye Gridi ya Taifa kuna upungufu wa Megawati 400, hizi huwa zinacheza kulingana na mahitaji ya siku husika, juhudi zinaendelea na kupata gesi zaidi kutoka kwenye visima vyetu wakati huohuo kuna matengenezo ya mitambo.

“Ripoti ya kufikia leo upungufu kwenye Gridi ni Megawati 300 hadi 350, pamoja na hivyo kusudio letu ni kuwa hadi kufikia Machi 2024 tusiwe na changamoto ya upungufu.”
IMG-20231002-WA0016.jpg

Alipoulizwa kuhusu Megawati 100 ambazo zipo IPTL, amesema muda wake ukifika litazingatiwa suala hilo.
IMG-20231002-WA0037.jpg
IMG-20231002-WA0035.jpg
IMG-20231002-WA0029.jpg



Takwimu za Uzalishaji wa Umeme Tanzania (2023)

Vyanzo vya Uzalishaji
Gesi Asilia 64.04%
Maji 30.69%
Mafuta 4.71%
Tungamo Taka 0.56%

Jumla: Megawati 1,872.05

Chanzo: TANESCO
 
Lini tutaanza na sisi kuongelea net zero? Tuna jua la kutosha kuweza kutumia umeme wa jua; tuna upepo wa kutosha kutegemea windmills, tuna hydrogen ya kutosha; tungang'ania gesi, gesi, maji, mafuta! Twende na ulimwengu wa kisasa, tungalie miaka 100, 500 ijayo, kwa ajili ya vizazi vijavyo!
 
Lini tutaanza na sisi kuongelea net zero? Tuna jua la kutosha kuweza kutumia umeme wa jua; tuna upepo wa kutosha kutegemea windmills, tuna hydrogen ya kutosha; tungang'ania gesi, gesi, maji, mafuta! Twende na ulimwengu wa kisasa, tungalie miaka 100, 500 ijayo, kwa ajili ya vizazi vijavyo!
Huko walipoendelea bado wanatumia gesi, makaa ya mawe, nyuklia, mafuta
 
Back
Top Bottom