Mh. Waziri husika zingatia hili, usalama wa vyuo vikuu na mali zake

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,667
30,581
Kwa ambao hawajui msishangae hata mauaji ya wanafunzi yanayotokea marekani kila siku sio kwamba hawana geti wanazo ila uimara wa ulinzi jambo muhimu kuliko tunavyosubiria majanga nakujirekebisha

Leo nimeona niongelee mazingira ya UDSM na vyuo vingine..kiukweli usalama wa UDSM ule wa miaka ya 1999-2004 sio huu wa leo.

Getini wameandika na bango kubwa watu wasimamishe magari wasachiwe hilo jambo halipotena watu wanajipitia walinzi wamegeuka wasomaji magazeti watu wanatoka na vitu hujui kama vya chuo

Njoo ofisi kuu hapa utawala unapoingia hakuna geti kusema utasachiwa au lah nenda Kule chini COET walinzi wako kama wapiga ramli unapita na kutoka getini unavyotaka

Mizaha hii iliwatesa na inaendelea kuwatesa wamarekani always..tujitahidi kuimarisha ulinzi vyuoni kwa ujumla na sio UDSM tu nimeelezea kama mfano.

Cha kushangaza kibao ambacho mtu anatakiwa kukisoma asimame getini asachiwe nenda geti la upande wa chuo cha ardhi limewekwa chini na maandishi mengine hayasomeki kabisa kuonyesha kutojali nini kinatakiwa
 
Mkuu umeleta ushauri mzuri lakini hadi litokee tukio ndipo utaona ukaguzi,pia inanikumbusha wakati magaidi walipovamia westgate Mall kule kenya pale mlimani City walianzisha utaratibu wa kukagua watu wote wanaoingia mule ndani lakini hivi sasa hamna tena huo utaratibu,ukienda pale unaingia bila hata kukaguliwa ndio maana majambazi yameweka kambi pale
 
Mie naona badala ya kumpapasa mtu wawe na vifaa maalum kama uwanja wa ndege na kwingineko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…