Mh. Rais, Magufuli; pokea zawadi yangu kwa ajili ya mwaka mpya 2017

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
Mkuu, shikamoo! Ukiwa kama moja ya wale niwapendao, sina budi kukupatia zawadi yangu kwa ajili ya mwaka mpya 2017. Sina pesa, sina mali lakini angalau Mwenyezi Mungu kanijaalia kuwa na mawazo ambayo yanaweza kuwa mazuri.

Mh. Rais, suala la kukosolewa “Critism” ni suala ambalo binadamu wote huwa hatulipendi. Hata hivyo, ni suala la kimaumbile kuwa; maadam mtu anaishi, anafanya vitu mbali mbali na anaongea na watu, ni lazima mtu huyo akosolewe tu. Ndio maana hata mwanafalsafa Aristotle katika moja ya maandishi yake akasema “Criticism is something we can avoid easily by saying nothing, doing nothing, and being nothing.” lakini kama mtu anatenda na anaongea, lazima atakosolewa tu, hayo ndio maumbile ya binadamu. Suala linalobakia nia amma apende au asipende kukosolewa lakini bado watu watakuwa wakikosoa ama kwa siri au dhahiri.

Mh. Rais wetu mpendwa; pamoja na kuwa kukosolewa daima kunakera; lakini kukosolewa ni kitu kizuri sana kwa anayekosolewa kuliko kwa anayekosoa kwani anayekosolewa huongeza maarifa lakini anayekosoa hakuna kipya anachojifunza.

Mh. Rais, mtu afanyapo jambo lolote lile; kupata mrejesho toka kwa jamii ni muhimu pengine kuliko kitu kingine chochote. Hebu jiulize kwa mfano unasema au unafanya kitu halafu jamii haitoi feed back!!? (au inatoa feedback ya kuigiza)!. Sasa feedback ndio inakuja kwa njia ya kushangiliwa, kukosolewa au kubaki kimya. Hata hivyo, wale wanaounga mkono, tayari wanakuwa washakubali kwa hiyo hamna wanachoweza kuongeza kwenye lile lililofanyika ili kuboresha na wanaokuwa kimya wanakuwa hawakotayari kuwajibika, bali wale wanaokosoa ndio wanaweza kuwa na maboresho.

Mh. Rais, Ukosoaji “Criticism” ni kama kioo. Ni vigumu sana mkuu, kwa mtu mwenyewe kujitathmini na kujua alivyo bali wale wanaomwangalia ndio wanaoweza kujua zaidi alivyo. Hii si kwangu au kwako tu mheshimiwa, lakini hebu kila mtu na ajiulize; ni mara ngapi ashawahi kufanya vitu akidhani yuko sahihi ila baada ya muda akabaini kuwa hayuko sahihi kutokana na “Criticism” za hadhira?. Pengine ndio maana mwandishi Frank A. Clark akasema “Criticism, like rain, should be gentle enough to nourish a man’s growth without destroying his roots.”

Mh. Rais, “Criticism” ni njia ya taarifa/ feedback pekee ambayo wanaoitoa huitoa kutoka kwenye nafsi zao bila unafiki. Kwa mantiki hiyo, inaweza kuwa ndio njia inayoweza kumpa mtu taarifa sahihi juu ya alivyo au alichokifanya kuliko njia nyingine yeyote.

Mh. Rais, “criticism” ni kitu kizuri kwa sababu humfanya mkosolewaji kudurusu yale anayoyafanya kila mara na kuona namna ya kufanya vizuri zaidi.

Mh. Rais wangu, mtu anayekosoa mwingine; haimaanishi kuwa anamchukia yule anayemkosoa bali anapenda afanye vizuri zaidi.

Kwa mantiki hiyo hapo juu, nakuomba Mh.Rais wangu mpendwa; wakati uingiapo mwaka 2017 uangalie kama ukiona inafaa na itakupendeza uwafanye wakosoaji wako kuwa “fans” wako na kutoka kwao, durusu yale wanayokueleza na chukua yale ambayo ni “constructive” na kuyafanyia kazi na utaona mrejesho wake utakavyokuwa wakupendeza kwa watu wengi.

Mh. Rais, hii ndio zawadi yangu kwako, nakuomba uipokee na kama utaipokea, naamini ni zawadi ambayo italeta matokeo makubwa sana kwenye uongozi wako na watanzania kwa ujumla kwenye mwaka 2017 na kuendelea.


Kwa heshma kubwa naomba kukukabidhi;-
 
Wakati tunaelekea 2017 , kwa wale wakosoaji nao wajitahidi kuwa na "Constructive Criticism" na hiyo inaweza kusaidia sana kwenye mambo ya msingi kwenye maendeleo yetu.
 
Ukitaka kuwa kiongozi bora, lazima ukubali constructive criticism.

Unapotokea kiongozi ambaye kila anayekukosoa unamuona kama mchochezi, basi hapo panaacha maswali mengi yanayokosa majibu kuwa ni kwanini kiongozi ukatae kabisa kusahihishwa pale inapoonekana umekosea.

Inapotokea kiongozi ambaye yeyote anayemkosoa anajibu kwa kupiga 'mkwara' kuwa yeye hajaribiwi.....

Hapo kunakuwa na maswali mengi yanayokosa majibu kuwa kiongozi wa aina hiyo asiyetaka kukosolewa, je yeye anajitoa kwenye ubinadamu wa kawaida?

Kwa kuwa vitabu vyote vya dini vinabainisha kuwa hakuna binadamu ambaye yupo 100% perfect.

Ambaye yuko 100% perfect ni Mungu peke yake.
 
Kwa kuwa vitabu vyote vya dini vinabainisha kuwa hakuna binadamu ambaye yupo 100% perfect.

Ambaye yuko 100% perfect ni Mungu peke yake.
mkuu kukosea sio kitu cha ajabu wala cha kudhalilisha bali ni sehemu ya ubinadamu wetu. Hata mitume wa zamani walikuwa wakikosea. Kwa mfano kwa waislaam wanazisoma habari za nabii Yunus na alivyokuwa amekusea lakini baadaye akajisahihisha. Wakriso wanamtambua kama nabii yona.
 
Labda wewe unachanganya vitu kati ya kukosoa na kutukana au kutenda jinai...
Hivi ni lini na ni wapi Magufuli alikataa kukosolewa?
Wale wapinzani bungeni mbona huwa wanamkosaoa na hajawafanya lolote?
Mbona humu mnamkosoa na hajwafanya lolote?
Yani hata sijui kwanini mnaandika vitu visivyo kuwepo? Hivi kweli Magufuli angekuwa hataki kukosolewa hata wewe ungepata wasaha wakuandika huu uzi?
 
Hivi ni lini na ni wapi Magufuli alikataa kukosolewa?
Hivi kweli Magufuli angekuwa hataki kukosolewa hata wewe ungepata wasaha wakuandika huu uzi?
Mkuu, sijasema hataki kukosolewa, usinilishe maneno, nimesema inafaa zaidi kuwapenda wakosoaji wake na kuwafanya kuwa "Fans" wake. Yaani anapenda kukosolewa na anawapenda wanaompa " constructive criticism " ila itakuwa vyema kama atawapenda zaidi maana wanampa mbinu za kuboresha mambo kuliko wale wanaomshangilia kwa kila kitu au kukaa kimya bila kutoa mrejesho wa chochote wakati wote..

umeelewa sasa?
 
Hii ni shida tu kwa kiongozi wanamna hiyo lakini kwa kuwa tulichagua wenyewe wachatukome
Mkuu, uwapo katika mazingira yoyote wakati wowote, fikiria ni kwa namna gani unaweza kuifanya kesho yako na ya wenzako kuwa bora kuliko leo na jana bila kujali ni wapi ulikosea au nani alikosea nini. Ukifanya hivyo, mara nyingi utajikuta ukiwa na mchango chanya kwenye maisha yako na jamaa zako, na hivyo kuwa mtu muhimu duniani na kuwa na sababu ya msingi ya kuendelea kuishi.
 
Wale wapinzani bungeni mbona huwa wanamkosaoa na hajawafanya lolote?
Amefanya jambo zuri na ni bila shaka atafanya vizuri zaidi na ndicho kinachozungumziwa hicho sema tu sijui kwa nini hukuelewa, labda lugha!
 
Hii ni shida tu kwa kiongozi wanamna hiyo lakini kwa kuwa tulichagua wenyewe wachatukome

Lakini pia jambo la msingi ni kuhamasishana kote mjini,vijijini,kwenye mikusanyiko ya watu ili kwa pamoja tutwae mageuzi ya kiutawala.Kosa lisirudiwe 2020.
CCM ni kupe.ktk taaluma ya mashairi ya kiswahili kupe kitaswira huwa na maana ya mnyonyaji,hivyo kwa pamoja tuwakatae na tuwapige teke.
 
Mafisadi mtanyooka tu, na bado miaka 9 mbele.

Wapuuzi wakubwa nyinyi, mligeuza nchi shamba la bibi
 
Wewe tahira kweli unataka sasa kuleta wehu wako kwa kuzidisha unafiki na uzambiki shut ua bowl if u don't have a single point since u was born.
Hii ni shida tu kwa kiongozi wanamna hiyo lakini kwa kuwa tulichagua wenyewe wachatukome

 
Umati wa watu utakaojitokeza kesho utapeleka kilio kwa mafisadi.

Wananchi wako tayari kubadili katiba na kumruhusu magufuli awe rais wa milele ili kuyaangamiza kabisa mafisadi wa ufipa.
 
Umati wa watu utakaojitokeza kesho utapeleka kilio kwa mafisadi.

Wananchi wako tayari kubadili katiba na kumruhusu magufuli awe rais wa milele ili kuyaangamiza kabisa mafisadi wa ufipa.
Kunguru mdandia ata cost ukidhan inakusaidia !aibu nanisifa mbaya kuona mchangiaj mwenye akil za funza kama ww hasara kuwa bado unaishi!
 
Vp mbowe ana kubali kukosolewa HUKO CDM????
 
Umati wa watu utakaojitokeza kesho utapeleka kilio kwa mafisadi.

Wananchi wako tayari kubadili katiba na kumruhusu magufuli awe rais wa milele ili kuyaangamiza kabisa mafisadi wa ufipa.
Umesoma kabla ya kuchangia, au ndo unawahi mwaka mpya?
 
Umati wa watu utakaojitokeza kesho utapeleka kilio kwa mafisadi.

Wananchi wako tayari kubadili katiba na kumruhusu magufuli awe rais wa milele ili kuyaangamiza kabisa mafisadi wa ufipa.

Mkuu hii ya kubadili katiba unaongea kwa niaba yako mwenyewe au Watanzania. Iwe iwavyo adui namba moja ya Watanzania ni mafisadi na ufisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…