Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,705
- 4,702
Kila aliyesikiliza mjadala wa ripoti ya CAG na majawabu ya mawaziri, ameelewa wazi kwamba mawaziri wanahusika na wizi huo. Kama wasingehusika, ingekuwa ni taharuki maana hakuna anayetaka kuibiwa.
Pamoja na kuhusika ktk wizi, yaonekana wapo ktk nafasi kwa urafiki binafsi na rais, na kuna mazungumzo binafsi kati ya rais na wao. Wanafahamiana. Ndiyo maana hawajali malalamiko. Hii ilithibishwa na malalamiko ya mbunge Mulugo; wakati wabunge wanajadili, wao ‘wanachati’. Hizo chati, ninahakika wanatumiana taarifa za mizaha juu ya wizi.
Kuna tukio la Spika kumuhoji waziri wa Elimu, Mkenda. Jambo ambalo lilitokana na hoja ya mbunge kutaka kufahamu maadili ktk shule zetu. Liligeuzwa na spika na kuwa ni kudhibiti madaraka ya waziri na kuanza kumuhoji kama mtu aliyekosea taratibu. Badala ya kuwa azimio la Bunge ilikuwa ni amri ya spika, waalimu warudishwe madarakani.
Hii imeashiria kwamba ndani ya mawaziri, wapo walio na hadhi na heshima, na wengine wapo lakini hawapendwi na spika na rais, ambao wana urafiki wa aina fulani. Sikuona sababu ya kuingilia jambo hili ndani ya bunge, badala ya kumuomba waziri afuatilie. Wakati huo huo kuna mawaziri kama Mwigulu, hutukana bungeni bila hata kuonywa bado wanatukana hata umma wa watanzania kwamba wasiotaka maamuzi ya serikali waende Burundi. Yaonekana akina mwigulu wako kundi la mawaziri marafiki wa uteuzi.
Mwisho kuna tukio la Mbunge wa Ngorongoro akieleza uporaji wa mifugo uliofanyika jimboni kwake na askari wa TANAPA. Ngorongoro tulikoambiwa ni PRIMITIVE kwenye filamu ya rais ya Royal tour. Pamoja na maelezo marefu, waziri Angela alipotoa majawabu ya serikali, hakuonekana kujutia matendo hayo na hasara waliyopata wananchi kwa wizi wa askari wa TANAPA. Badala yake aliisukumia mahakama kana kwamba mahakama hutafuta kesi mitaani.
Mahakama inayofanya madudu kila siku. Inaamua kuuza ng’ombe, kesho yake zinapigwa mnada bila hata muda wa kukata rufaa. Yaani kesi iliendeshwa tayari dalali wa mahakama akiwemo ndani. Waziri hajutii uharifu huo.
Jawabu halikuwa na utu. Nilitegemea Spika aingilie kama alivyoingilia maamuzi ya waziri Mkenda kwa undani huo huo! Lakini ameliweka kama jambo la kawaida sana ambalo halina uzito. Inaonesha pia waziri Angela yuko kundi la marafiki wa rais na Spika, hata kama wanatoa majawabu hovyo.
Mh. Rais tunakuomba ujitambue. Uache urafiki binafsi wa mitaani ktk kuendesha nchi. Hata marafiki kuna kazi huwashinda. Spika naye ameonekana kulewa sifa. Tatizo ni mwanzo wake ambao ulitokana na kubebwa toka chuoni bila sifa akawa naibu na ghafla akawa naibu spika. Tunajua alibebwa na Asha Rose Migiro aliyekuwa akimtumia kama house girl wake tangu askiwa mwanafunzi. Yeye amejiweka kwenye uelewa uliopindukia na amefikia hatua ya kuhutubia na kusikiliza shida za wananchi kama rais wa nchi.
Baya zaidi, wananchi wanasumbuliwa kwa kuwa tu viongozi hawatoki mikoa au wilaya zao. Spika amekuwa makini kufuatilia waalimu walioleta muziki wa hovyo shuleni kwa kuwa tu anatoka sehemu hizo. Lakini anaongoza Bunge linaloletewa taarifa za serikali ikitangaza kuhamisha kijiji kizima kwa kuwa tu viongozi hawatoki huko. Je, leo hii kuna mtu anaweza kutangaza kuhamisha kijiji cha Kizimkazi, Zanzibar? Badala yake kijiji kinatukuzwa na kupeleka tamasha la kitaifa kwa kuwa tu rais alizaliwa hapo! Jiulize Spika huyu angekuwa ni kutoka Ngorongoro hali ingekuwaje?
Tuache ukabila, tuache upendeleo hata kwenye wizi. Rais unawezaje kuruhusu kiongozi aibe kulingana na urefu wa kamba yake. Watu wa Bunda, Ngorongoro, wahamishwe hovyo tu!