Mh. Makala atawaomba radhi wananchi hadi lini?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,585
14,045
Bila kujua dhamira yao huwezi kuwaelewa wanafanya hivyo kwa lengo gani. Wanachochea hasira ya wananchi dhidi ya nani? Panakofuka moshi pana dalili ya kuwepo moto. Je inatosha kwa mh.makala kuwaomba radhi wanachi kwa Yale wanayosema akina Nape, Ng'umbi Na wengine kuhusu ushindi wa ccm kwenye chaguzi? Bado nani ambae hajasema kuwa ccm inatumia mbinu kushinda?
 
Kuna wakati Horace Kolimba aliwahi kusema jambo kuhusu CCM lakini alionekana kama anaropoka, hawa nao je?
 
serikali na CCM wanahujumiwa, ni hujuma hii wawe macho. Hawa wanaoropoka mitandaani kuwa wanafanya hili na lile kushinda kura inawezekana ikawa ni njama kubwa ya kuwachonganisha watanzania na serikali ya chama cha mapinduzi. CCM na serikali hebu fanyeni uchunguzi wa kina kuhusu waropokaji hawa.
 
Back
Top Bottom