Mh. Daniel Fred Kidega Spika Mpya wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)

albuluushiy

JF-Expert Member
Oct 2, 2013
1,404
686
B5OFLtHIEAAudie.png:large

Mh. Daniel Fred Kidega Kulia akiwa anaapishwa
B5OKYh5IAAAZYdk.jpg:large

Mh. Daniel Fred Kidega akihutubia Bunge Baada ya kuapishwa

Habari za jioni ndugu wapenzi popote pale mlipo,kwa taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Dan Fred Kidega (NRM) ndiye spika mpya wa bunge la afrika mashariki baada wa yule wa awali kutolewa mapema alhamisi.

Daniel Kidega amepita bila Kupingwa baada ya Chris-Opoka ondoa na kumuunga mkono Kidega wakati mgombea mwingine Suzan Nakawuki hakurudisha fomu.



Dany Kidega awa Spika EALA

MBUNGE wa Chama cha National Resistance Movement (NRM) cha Uganda, Dany Kidega amechaguliwa kuwa Spika mpya wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Kidega anachukua nafasi ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Dk. Margareth Zziwa, aliyeondolewa kutokana na kukabiliwa na kashfa mbalimbali.
Kidega alipata ushindi huo baada ya mbunge mwenzake kutoka Uganda Christopher Okumu (UPC), kujiengua katika kinyang'anyiro hicho muda mchache baada ya kuingia bungeni.

Baada ya Dk. Zziwa kung'olewa katika wadhifa huo, Okumu, alikaimu nafasi hiyo hadi kuibuka kidedea katika uchaguzi wa jana.
EALA juzi lilimuondoa madarakani Dk. Zziwa kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kushindwa kutimiza wajibu na matumizi mabaya ya madaraka.
Kuondolewa kwa Dk. Zziwa kulitokana na wabunge wa EALA kupiga kura na 36 kati ya 39 waliohudhuria kikao cha dharura kilichofanyika juzi chini ya uenyekiti wa Kaimu Spika, Okumu, walipiga kura za ndiyo kukubali hoja ya kumuondoa madarakani.

Wabunge wawili walipiga kura ya hapana, wakati mmoja hakupiga kura hoja hiyo iliyowasilishwa Machi, mwaka huu na Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki na kuibua mvutano miongoni mwa wabunge waliokuwa wakimtetea Dk. Zziwa na wale waliotaka ang'oke.

Uamuzi wa kumng'oa Dk. Zziwa umechukuliwa kwa kuzingatia kifungu cha 53(3) cha Katiba ya kuanzishwa kwa EAC, inayowapa mamlaka wabunge kumwondoa ofisini spika.

Baada ya kung'olewa katika nafasi hiyo baadhi ya wabunge walifurahia na kusema wamefanikisha walichokihitaji kwa muda mrefu.
Dk. Zziwa alisimamishwa wadhifa wake kutokana na hoja iliyopitishwa na wabunge wa EALA Novemba, mwaka huu katika kikao chake cha Mjini Nairobi akizuiwa kutekeleza majukumu yake.

Chanzo:Mtanzania
 
Heading yako na ulichoandika ni vitu viwili tofauti. Watu wanawaza JK kubutubia taifa na wewe unaandika kama una brief za kitakachotokea kumbe ni mambo ya bunge la EA.
 
Heading yako na ulichoandika ni vitu viwili tofauti. Watu wanawaza JK kubutubia taifa na wewe unaandika kama una brief za kitakachotokea kumbe ni mambo ya bunge la EA.

hahahahahaha kaka nlijua tu akili yako itakuwa huko ila na haya mambo tuna haki kuyajua pia
 
Nashangaa mpaka sasa Tanzania tunang'ang'ania nini kwenye huo Muungano.... Hao waachiwe waendelee na mipango yao ya maendeleo! Sisi tuendelee kutembeza bakuli uarabuni hadi china...
 
Back
Top Bottom