Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 334
- 691
Manzese
Picha ikionyesha baadhi ya maduka eneo la Manzese Tiptop, jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumatano Juni 26, 2024 yakiwa yamefungwa kutokana na mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea katika baadhi ya mikoa nchini.
Madai ya wafanyabiashara ni pamoja na utitiri wa kodi unaotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kariakoo
Wafanyabiashara wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam wameingia katika siku ya tatu mgomo wa kufungua maduka waliouanza Jumatatu ya Juni 24, 2024 wakipinga tozo na kamatakamata inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hadi saa 3:30 asubuhi ya leo Jumatano, Juni 26, 2024, baadhi ya maduka hayajafunguliwa kama ilivyokuwa juzi na jana. Baadhi ya wafanyabiashara waliofungua maduka ni wale wanaouza vipodozi, simu na dawa.
Baada kuanza kwa mgomo huo, Serikali ilifanya kikao na viongozi wa wafanyabiashara hao na kutangaza kusitisha kwa muda ukaguzi wa risiti za kielektroniki za EFD inayofanywa na TRA, lakini wafanyabiashara wameendelea na mgomo
Mbeya
Mgomo wa wafanyabiashara wa maduka jijini Mbeya umeendelea leo Jumatano, Juni 26, 2024 ikiwa ni siku ya pili, huku baadhi ya maduka ya pembeni yakifunguliwa.
Wafanyabiashara hao wameanza kugoma jana JUni 25, wakishinikiza Serikali kuondoa utitiri wa kodi na tozo mbalimbali ambazo si rafiki kwa wafanyabiashara.
Mwananchi Digital ambayo ipo maeneo ya Soko la Sido, Mwanjelwa na Kabwe imeshuhudiwa maduka makubwa yakiwa yamefungwa, huku madogo ya pembeni yakiwa wazi yakitoa huduma.
Pia wafanyabiashara wanauza bidhaa zao nje, wanaendelea, ingawa ni kwa kificho.
Hata hivyo, hakuna mfanyabiashara aliyeeleza kuhusu hatima ya mgomo huo, iwapo utaendelea au kusitishwa kwa kipindi hiki.
Mwanza
Wakati mgomo wa wafanyabiashara jijini Mwanza ukiingia siku ya pili, maofisa wa Jeshi la Polisi wanaotembea na waliopo kwenye magari wameonekana wakipita katika mitaa mbalimbali ya jijini hilo, huku maduka yakiwa hayajafunguliwa.
Kamera ya Mwananchi Digital iliyoko mtaani kuanzia saa 12:30 hadi saa 3:00 asubuhi ya leo Jumatano Juni 26, 2024, imeshuhudia magari yaliyojaa askari wa Jeshi la Polisi yakikatiza, huku baadhi ya askari polisi wakitembea kwa miguu kuzunguka mitaa ya jiji hilo.
Alipoulizwa kuhusu askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuwasambaza askari katika mitaa ya jiji hilo, huku akidokeza kuwa jukumu lao ni kuimarisha ulinzi kwa wafanyabiashara watakaofungua maduka, ili wasifanyiwe fujo na waliogoma.
Kamanda Mutafungwa amesema ulinzi na doria hizo zitakuwa endelevu hadi hali itakaporejea katika utimamu, huku akionya watakaojaribu kuwafanyia vurugu wafanyabiashara walioridhia kufungua maduka yao.
Dodoma
Picha ikionyesha baadhi ya maduka katika Mtaa wa One way, leo Jumatano Juni 26, 2024 jijini Dodoma ambapo wafanyabiashara wamefunga maduka yao, ikiwa ni siku ya pili ya mgomo.
Madai ya wafanyabiashara ni pamoja na utitiri wa kodi unaotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mtwara
Wafanyabiashara katika soko kuu lililopo Karibu na Stendi ya zamani mkoani Mtwara wamefunga maduka yao leo Jumatano, Juni 26, 2024.
Tunduma
Maduka katika soko kuu la Manzese, Halmashauri ya mji wa Tunduma mkoani Songwe yakiwa yamefungwa.
Wafanyabiashara hao wamefunga maduka kushinikiza kupunguzwa kwa utitiri wa kodi wanaotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Arusha
Maduka mkoani Arusha yakiwa yamefungwa leo Alhamisi Juni 26, 2024, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara, kushinikiza kupunguzwa kwa utitiri wa kodi wanazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia soma: