Mgogoro wa Kenya na Tanzania

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
4,601
NARUDIA TENA :- WATANZANIA WAKENYA WASIWASUMBUE.

Na Thadei Ole Mushi.

Wiki hii toka jumatatu joto la kidiplomasia Kati yetu na Kenya limepanda Kiasi. Joto hili linasababishwa na vurugu za ugonjwa wa Corona. Nimejaribu kwa kiasi kuwaonyesha watanzania sababu za kuendelea kukataa mchezo wa Kenya katika Uchumi wetu. Naelewa Sana umuhimu wa diplomasia yetu na Kenya lakini linapokuja issue ambayo inalihusu Taifa langu lazima tupigane kwa pamoja.

Leo nitawapa kwa kifupi Sana kwa nini Kenya ukiangalia mwelekeo wa nchi yetu kiuchumi wanachanganyikiwa. Nitaongelea Mambo mawili kwa kifupi Sana.

1. Mradi wa SGR.

Kuna watakaojiuliza Reli ya SGR inawahusu nini wakenya? Ni swali zuri Sana na kila anayejiuliza ni haki yake ajiulize.

Kama Kuna kitu kinawasumbua Kenya ni Mradi huu wa SGR. Tukumbuke kuwa issue hapa sio mataruma ya Reli Bali issue kubwa hapa ni bandari zetu Mombasa na Daresalam

Ipo hivi

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

"Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika....

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki Tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Daresalam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Kwa Sasa wanajaribu kutumia Hili la Corona angalau wapige pesa kwenye bandari yao ya Mombasa. Logic ndogo tu ya kujiuliza hakuna mabasi yanayokwenda Kenya? Kama yapo ulishawahi kuona abiria au madereva wa mabasi wakilia Kama wa malori? Unajua ni kwa nn wanakomaa na madereva wa malori? Huhitaji Elimu ya chuo kikuu hapa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC - The East African - Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC

Hili Ni Gazeti la Kenya sio la Tanzania katika Hali Kama hii hawawezi kutufurahia sisi kupaa kiuchumi.

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.

Kenya’s Embattled SGR Suffers Major Setback as Burundi, DRC Opt for Tanzania Route to Port of Dar es Salaam

2. Mradi wa Stiglers Gorge.

Huu ni Mradi wa umeme ambao kufikia 2022 tunatarajia uwe umekamilia kabisa.

Mradi huu utatupatia megawatt 2,100 sawa na bwawa la Aswan la Misri ambalo nalo linatoa megawatt hizo 2,100.

Stiglers itakuwa bwawa Namba Moja Afrika yeye na Aswan kwa pamoja kwa kutoa megawatt nyingi na zinazolingana. Mabwawa Mengine yote yaliyobakia Afrika hayawezi kufikia kiwango hicho Cha Stiglers.

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga.

Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira....

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais wetu. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.

Tanzania to build Stiegler's Gorge dam in a wildlife reserve and Unesco site - LifeGate

Linapokuja suala la kiuchumi kwa Dunia ya Sasa ni Vita. Na Kama hutoruhusu akili yako kufanya kazi Basi utajikuta ukiitikia chorus za nyimbo za mabeberu.

Stiglers itatuondoa kabisa kwenye uhaba wa umeme na kutufikisha kwenye Uchumi wa viwanda. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa Kenya ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda. Hii ni Vita.....hata Panadol hatununui Tena Kenya.

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?.....

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Sisi kujenga Stiglers tu imekuwa kelele kubwa.

Tupunguze kulalamika tuijenge nchi Yetu. Hata Sasa wagonjwa wetu wengi hatupeleki Kenya badala yake wanapelekwa Mloganzila na Muhimbili kwa zile case za kupelekewa Nairobi Kenya.

Vijana wa Kitanzania tufahamu kuwa kwa Sasa tuna jeuri ya kutosha kabisa. Tembeeni kifua mbele, Hawa wachache walioamua kusimika kichwa kwenye mchanga Kama jogoo tuanchane nao. Najua ukiyasema haya watakuambia unatafuta Uteuzi as if kuteuliwa ni jambo baya au yeye hataki kuteuliwa au akiteuliwa atakataa..... Akili za kijinga kabisa hizi.

Unakifikiri wanafurahia.......... Ni baadhi ya watu tu hawaelewi kinachoendelea au kufuatilia Mambo hawawezi. Ndio maana tunawashauri Kama wanaona Kenya ni Bora zaidi wahamie Kenya.... Hakuna aliyenyiwa kufanya hivyo.

Ole Mushi
0712702602

C&P
 
Ww ni mkongwe huku jukwaani, una copy na ku paste hii insha iliyotembea huku mitandaoni toka juzi!?
 
Back
Top Bottom