Mganga wa kienyeji ahukumiwa miaka 20 jela na viboko 12 kwa kosa la kufuga fisi

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,512
3,991
Nani anaikumbuka hii kesi ya mganga wa kienyeji aliyekamatwa na fisi? amehukumiwa leo.

IMG_2994.jpeg


Mahakama ya Wilaya Bariadi mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kuchapwa viboko 12 Emmanuel John (31), maarufu kama Chief wa Kilulu, kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali aina ya fisi akiwa hai na akiishi naye nyumbani kwake.

Mshtakiwa huyo, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kilulu kilichopo kata ya Bunhamala, wilayani Bariadi, na mganga wa kienyeji, alipewa adhabu hiyo katika kesi namba 2458/2025 iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama hiyo.

Awali, akisoma kosa la mshtakiwa, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mashtaka Mkoa, Lupiana Mahenge, alieleza mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa na nyara ya serikali, fisi akiwa hai, akimfuga nyumbani kwake kinyume cha sheria.

Mtuhumiwa aliishi na fisi huyo kama mnyama wa kufuga kinyume na kifungu cha 86 (1) na kifungu kidogo cha (2)(C)(III) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori sura ya 283, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliomba mahakama imsamehe kwa kuwa anategemewa na familia ya watoto wanne, wakiwemo mapacha, ndipo hakimu akatoa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela na viboko 12 ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.
 
Adhabu kubwa kuliko kosa, angemuua angeitwa muwindaji haramu, angalau inge make sense, ila kumfuga tu pasipo kumdhuru sioni kama anastahili adhabu kubwa kiasi hicho, mbona kuna hawa wanaotembea na mijoka mikubwa kwenye maonyesho yao hawakamatwi?
Labda ni wakati muafaka hizi sheria zifanyiwe mabadiliko ili kuendana na mazingira ya sasa.
Nakubaliana na wewe, miaka 20 ni mingi sana.
 
Hivi kwa nini sheria za Tanzania ni za uonevu sana. Yaani kufuga fisi miaka ishirini jela?

Hizi sheria lengo lake ni kufundisha au kukomoana?
Mpaka huruma kwa kweli..SEMA USIMUACHE MCHAWI AKAISHI..

KAMA VIPI MGANGA AJIOKOE MWENYEWE KWA TUNGURI ZAKE PIA INGEFAA AKASIKILIZWA MAANA ANA MAARIFA YA KUWEZA KUFUGA MNYAMA KAMA FISI SIO JAMBO DOGO KUFUGA FISI ( HYENA)

Fisi ni mnyama mlafi na akiwa na NJAA anaweza kumgeuka hata boss wake..ingekua nchi zilizo ENDELEA MGANGA angepelekwa kwenye wizara ya maliasili na utalii aende kusaidia huko kukuza utalii na wanyamapori
 
Back
Top Bottom