magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 10,318
- 22,611
Ehhh ndio maisha bwana, unashanga kuhusu
jela! Kwa wanaharakati na wanasiasa halisi jela
ndio masikani, huwezi kuwa mdai haki alafu
uogope masikani (jela), kama unaogopa jela
acha siasa, acha uwana harakati, acha kutetea
misingi ya taifa lako, kazi ndogo tu acha kuwa
mzalendo wa nchi na chagua kuwa mzalendo
wa serikali hapo jela itakupita kushoto.
Jifanye unisikii utaambulia uhujumu uchumi na
utakatishaji wa pesa, siunajua kuwa hii haina
dhamani! Haya wewe endelea kubisha, utasema
sikusema.
Ila ukichagua kuwa mzalendo wa taifa,
mwanaharakati wa kweli na mwanasiasa wa
umma jela haiepukiki ndugu, alafu utajiitaje
mtetezi uogope jela bwana? Wazalendo wa nchi
tugonge chairs... Ok tuendelee na sokomoko
letu la wajela jela, hivi unajuwa kuwa Jela Zipo
kuwaficha watetezi wa umma wanao wakela
watawala wasiopenda kukosolewa?
OK iko hivi... Ngoja nikurudishe nyuma
kidogo.....
Mnamo tarehe 20 Aprili, 1964 Nelson Mandela
alituhumiwa kwa kosa la uhaini, akasumbuliwa
na watawala, wakati wote huo akitaabishwa na
dola mahakama ya Afrika kusini haikuwa na
macho, wanasheria husema "Mahakama wakati
huo ilishikwa mikono" alipewa tuhuma ya
kuhujumu utawala wa kikaburi, shitaka lake
ufahamika kama "Rivonia Trial", ni moja ya
kesi maarufu sana Afrika.
Watasha wana msemo usemao "problems plus
problems Is equal to progressive, The Prisoner
today, The President tomorrow, And vice
versus." Ngoja nitie tashititi kidogo "mfungwa
wa leo ndio mtawala wa Kesho"...
Mandele akasimama kizimban mnamo tarehe
20 Aprili, 1964 Nelson Mandela, mshitakiwa
wa kwanza akiwa na wenzake katika ya Kesi ya
Rivonia (Rivonia Trial) walihukumiwa kifungo
cha maisha gerezani, hasa wakina Mandela na
wenzake karibu nusu ya maisha yao yote
waliishi gerezani.
Roben island ikawa sehemu ya maisha yao, kwa
kipindi chote, lakini kwakuwa Mungu ni wa
watu wote, sentensi ya kimombo ndio
inapoingia kuwa "mfungwa wa leo ndio
mtawala wa Kesho"..., miaka 27 baadae mambo
yakabadilika, wale wahain wa nchi wakageuka
maaujaa, ikawa tofauti ya miaka 27 iliyopita
walipoonekana kama magaidi walio hujumu
utawala wa kikaburu.
Unajua sheria kandamizi kwenye tawala za
kifashisti huwa zinapewa nguvu, ni kwasababu
kwao uwahimalishia mamlaka na kuwaweka
sehemu salama, maana watawala kandamizi
huzipenda sheria zenye jicho moja maana
zinawalinda kubakia madarakani.
Kule Harare Agosti 1964 Waziri mkuu mlowezi
alipiga marufuku vyama vyote vya kisiasa,
kikiwemo chama cha ukombozi cha ZANU
kilichoongozwa na Mugabe, kama haitoshi
aliwaweka Mugabe, Nkomo, Sithole na
wanaharakati wengine katika vizuizi bila
hukumu (detention without trial).
Mfano tu ni kwamba Robert Mugabe alitumikia
miaka kumi na moja kama mfungwa wa kisiasa,
akiwa kizuizini kwa kosa la uchochezi, yeye na
wenzake wakituhumiwa na serikali dhalimu ya
walowezi iliyoongozwa na Ian Smith, wakina
Mugabe, Nkomo, Mozorewa na Banana
Sandindo walionwa kama wachochezi na
wavunja sheria kwa hatua yao ya kupinga
ubaguzi wa rangi, unyonyaji, matumizi mbaya
na yasiyo na usawa wa Madaraka, ukandamizaji
wa haki za binadamu na kuwageuza waafrika
wenye aridhi yao watu wa tabaka la chini.
Baada ya kutumikia vifungo gerezani Mungu
akawainua akawabadilishia ile hadithi ya kulala
masikini na kuamka tajiri, siunajua "problems
plus problems Is equal to progressive, The
Prisoner today, The President tomorrow, And
vice versus." Yani "mfungwa wa leo ndio
mtawala wa Kesho" Mugabe akawa mtawala,
wale wakina Smith wakaikimbia nchi, maana
walimjua Mzee Matibili Mugabe asingewaacha
salama.
Mzee akupendaga ujinga, ndio maana mpaka
anakufa alikuwa akimlaumu Mandela kuwa
alikuwa kibaraka wa wazungu ambao yeye
alipenda kuwaita "pig's noise " na kutilia
msumali kwa kusema kuwa "Afadhali Mimi
nimewaachia wananchi wangu ardhi, Mandela
amewaachia wananchi wake mashairi, misemo,
tungo na masanamu yake".
Ndio maana hapa namanisha kwamba "The

mtawala wa Kesho"...
Mwaka 1958 nchini Tanganyika yani Tanzania
ya Sasa Mwalimu Nyerere alipewa Kesi ya
Uchochezi na utawala wa kikoloni, Mwalimu
alishitakiwa kutokana na maneno ya hotuba
yake alipo kuwa akihutubia umma.
Maneno ambayo Nyerere alituhumiwa na
kuitwa kosa nipale alipo waambia hadhira yake
kwamba "Naiomba Serikali ya kibeberu, itamke
wazi kwamba inaishambulia TANU kwa sababu
TANU tumetangaza bila woga kuwa Serikali ya
kimabavu tutaipiga vita. Tutaishambulia bila
kupumua mpaka tumeiangusha. Ndugu
wananchi, jihadharini, adui anashindwa,
anaanguka kwa sababu hana njia za kupinga
kilio chetu. Njia yake ni moja tu nayo ni kutaka
ghasia ili akatumie bunduki. Tusimpe nafasi…
adui atateketea bila shaka". Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, 1958. (Baada ya maneno
hayo na mengine, wakoloni walimkamata
Mwalimu na kumshitaki katika kesi maarufu
ulimwenguni iitwayo kesi ya uchochezi ya
Mwalimu Nyerere.
Katika kesi hiyo Mwalimu alitetewa na mawakili
watatu, Wakili msomi Quincy, Wakili msomi
Pratt na Wakili Msomi Rantancy. Ambapo
tarehe 12/8/1958 mahakama ya hakimu mkazi
ilimtia hatiani na akahukumiwa kwenda jela
miezi sita au kulipa fidia ya pesa taslimu
Shilingi 3,000 za kitanzania ambapo Chama cha
wanachama wa TANU walijichangisha na kulipa
gharama hizo, inamaana zingekosekana
mwalimu angeenda jela.
Miaka mitatu baadae mwalimu akawa kiongozi
wa nchi, hii inatoa maana kwamba gereza ni
moja ya vyumba vya wapambanaji...
Sisemi kuwa gereza zuri, hapana tena
ikiwezekana omba Mungu usikanyage huko
maisha yako yote... Huko ni sehemu mbaya
sana muulize Lissu, Zitto au Kabendera ndio
wanajua dhoruba za gereza..... Mwanangu Tito
Magoti anasota Segerea mpaka leo anasubiri ile
inayoitwa Plea bargain ili aweze kuwa huru...
Usiombe huko babu
Ok ebu tuachane na hilo turudi kwenye story
yetu ya wajela jela....Ndio maana naseama tena
kuwa "The Prisoner today, The President
tomorrow, And vice versus." Yani "mfungwa wa
leo ndio mtawala wa Kesho na kinyume
chake,"... Hapa tuelewane vizuri naposema "
Mfungwa wa leo mtawala wa Kesho na kinyume
chake namanishwa kwamba "Mtawala wa leo ni
mfungwa wa Kesho"
Hivi huamini hii la mkuru wa nchi kuwa
anaweza kulamba kwata segerea au keko?
Ngoja nikupe nyepe za hili, achana na Mzee wa
ilani Kangi, twende zetu mambele uone Marais
walio wahi kufikishwa Mahakamani kwa makosa
mbalimbali,
Huko Bronfotein Afrika kusini walimfungulia
mashitaka wao wa zamani wa Afrika kusini
Jacob Zuma alifikishwa mahakamani kujibu
mashtaka ya ulaji wa rushwa, ufisadi na
matumizi mabaya ya ofisi. Zuma alikabiliwa na
mashtaka taribani 16 aliyo ya tenda kipindi cha
uongozi wake. Hivi mpaka hapa ujaelewa
namanisha nini?
Kule Korea Kusini Park Geuin Hye, raisi wao
mwaka 2018, alipelekwa Mahakamani na
kuhukumiwa kifungo cha miaka 24, baada ya
kupatikana na hatia ya ufisadi, vitisho, na
matumizi mabovu ya madaraka. Hii Tanzania
nchi ya bongo zozo one day yes!! Acha
kushangaa nimesema one day yes...
Kule Chad mpaka Sasa Rais wao wa zamani wa
Chad, Hissene Habre amekuwa akitumikia
kifungo cha nyumbani tangu mwaka wa 2005,
nchini Senegal, ambako alitorokea baada ya
kuondolewa madarakani mwaka 1990. Katika
kipindi cha uongozi wake wa miaka 8 Habre
anadaiwa kuhusika na mauaji na dhuluma dhidi
ya maelfu ya wapinzani wake kisiasa na
kuwaadhibu watu nchini Chad kati ya miaka ya
1982 na 1990.
Sio huko tu hata Rwanda nchi ya Paul Kagame
ilimshikisha adabu mshirika wake wa zamani na
Rais wa zamani wa Rwanda, Pasteur Bizimungu
aliyefungwa jela kwa miaka 15 kwa madai ya
uchochezi.
OK ukiona hivi unapaswa kujisemea kuwa "The

mtawala wa Kesho na kinyume chake,"... OK
Kabendera cool... Piga chairs .... Magoti cool
piga chairs... Lissu cool piga chairs.... Zitto
cool piga chairs....
Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya
acknowledgment.
®Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya
ulimwengu.
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
© Copyrights of this article reserved
®written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
™Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
© Copyright 2020, All Rights Reserved.