Mfumo wa udhibiti ubora na ufanisi kazini: Utendaji wa watumishi wa umma wengi ni upuuzi, lazima udhibitiwe

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
342
553
Ģ moningiiii

"Watanzania kila mtu anakwambia ukingiia kwenye system tu bhas muhimu kuingia" kila Mtanzania hasa maskini ndoto zao ni kufanya kazi serikalini si kwasababu ya ubora wa mwajili tu ila ni kwasababu ya udhaifu wa mwajiri, serikalini huko ndo unaweza kuwa mlevi na usifukuzwe kazi ukashushwa vyeo tu lakini pia huko hakuna uangalizi mkubwa sana wa matumizi ya anayeshikilia ofisi mtu kujenga kibanda cha mlinzi kwa 20m ni kawaida na uulizwii.

Wafanyakazi wa baadhi ya mashirika ni pasua kichwa huduma mbovu lakini pia hawajali wanao wapa huduma kabisaa yanii ukiwa mfanyakazi serikalini hata uwe chizi unaweza fanya kazi hadi unastaafu kama meneja na wasikujue.

Wananchi million 60 tunakatwa kodi kusaidia kuendesha shughuli za serikali sisi ndo waajiri wa wao lakini hatuna uwezo wa kuwajibisha kiongozi mmoja mwenye madaraka yote anaweza mlinda yoyote na asisikilize walipa kodi wanaotoa mapato yao ili wao wapate v8 new model kila mwaka kufanya shughuli zao.

Kwa kiasi kikubwa wananchi tunajitaidi kutekeleza wajibu ili serikali iwe na nguvu na watendaji wake wapate ujira kuendelea kuwajibika kwa manufaa yetu sote, lakini ni kama wanajitenga na sisi na kuona sisi si sehemu yao wanafanya majukumu yao si kwa manufaaa yetu sote.

KWANINI SASA TUSIWE NA MFUMO WA DATA UTAKAO PIMA UTENDAJI NA UFANISI WA WATENDAJI WA JUU WA KILA ENEO NA KUTOA RATE YA PERFOMANCE KWA MWAKA NA WANANCHI WAWEZE KUONA PERFORMANCE KWA KILA ENEO KULINGANA NA UBORA WA UFANISI UTAKAO WEKWA.

Yani hapa naamanisha tuwe na kitengo cha ubora chini ya ofisi ya raisi kitakachokuwa kimeandaa mfumo maalumu wa DATA ANALYSIS utakao kuwa umepanga standards , malengo,dira, wajibu na nia za kila nafasi kubwa kama mawaziri, ceo wa mashirika, RC,DC,wakurugenzi, then waweke indicators kupima kila kilichopangwa na standards zake.

Kwa mfano, waziri mkuu awe amewekewa lengo la kugundua matatizo yanayorudisha nyuma ufanisi wa serikali na uondoaji wa tatizo husika na uboreshaji wa shughuli za serikali then tuseme kwa mwaka awe angalau amedetect matatizo 25 na ameyatatua na kutoa njia mpya katika maeneo hayo matatizo yaliyopotokea.

Mfano pia mkuu wa shirika la labda Tanesco awekewe lengo la kuvumbua njia mpya zitakazoweza kuzalisha umeme katika maeneo ya mkoani ili kufanya kila mkoa kuzalisha umeme na kuchangia katika gridi ya taifa na baada ya mwaka awe ameweza kutoa walau njia za uzalishaji katika mikoa 3.

Nb. Hii ni mifano tu ili mnielewe nachojaribu kuwaza ili kuongeza uwajibakaji na ufanisi na kupunguza wazembe

kupitia mifano hiyo kwa kila nafasi kulingana na rasilimali zinavyo ruhusu mwisho wa mwaka tuone performance labda waziri mkuu performance yake ni 60% kwasababu moja mbili tatu na itungwe sheria mfanyakazi asiyefika 50% atakatwa 25% ya mshahara wake kwa mwaka ujao wa fedha, akifanya chini ya 50% kwa miaka miwili mfufulizo atafukuzwa kazi na kutoruhusiwa kuomba kazi yoyote serikalini kwa kipindi cha miaka mitatu.

Na mfumo huu uwe wa wazi online kila mwananchi (waajir) waweze kuona ufanisi wa waliowapa dhamana .

Sijui nmewaza vyema au hangover inanisumbua.
 
Wazo zuri ila rasilimali ndio hamna

Ukisoma miongozo mbalimbali inaonesha Kila sekta na standard ya mwajiriwa na idadi ya watu anaotakiwa kuwahudumia

Mfano, mwalimu mmoja anatakiwa kuwahudumia wanafunzi 45 ndani ya chumba kimoja Cha darasa. Sasa nenda kwenye uhalisia Anza darasa lenyewe kwa odadi ya wanafunzi na baadae walimu idadi yao

Sasa hiyo ipo kwenye kila idara mapungufu ni makubwa kuanzia polisi, manesi, madaktari n.k

Sasa kama huna resources hatuna tunajilizaliza nini sasa?!

Africa sio ulaya tena huku kusini mwa jangwa la Sahara tulia wewe!!
 
Hii ni tabia ya Watanzania na Wala haianzii Serikalini inaanzia huko huko kwenye malezi ya jamii Sasa unatarajia jipya lipi labda?
 
Kazi ipo hii nchi ni bora liende tu,watumishi wa umma wanawahi ofisini kuchati na kutafuta gap wapige dili.
 
Mpaka umefikia kuwaza hivyo nanushaur wako juu ya kusema labda una hangover. Jua mifumo imefanya kaz yake ndio mana ukapata na amani ya kuandika hayo.mipaka ipo shawri,mtaan kwmako kupo sheari jua kaz inafanyika
 
Acha roho mbaya kijana husomi hata maandiko duniani tunapitaaa...
Daaa kwahiyo ni sawa watoto wanazaliwa na shida za moyo na matatizo mengine matibabu ni gharama wanapita mtaani kutuomba maskini wenzao huku kodi zetu zinanunua v8 za kampeni za chama
 
Mpaka umefikia kuwaza hivyo nanushaur wako juu ya kusema labda una hangover. Jua mifumo imefanya kaz yake ndio mana ukapata na amani ya kuandika hayo.mipaka ipo shawri,mtaan kwmako kupo sheari jua kaz inafanyika
Sijakuelewa mkuu
 
Hii ni tabia ya Watanzania na Wala haianzii Serikalini inaanzia huko huko kwenye malezi ya jamii Sasa unatarajia jipya lipi labda?
Sasa tubadilii mifumo aliyelelewa vizuri afiti aliyelelewa vibaya ashindwe kazi, tutaishi hivi mpaka lini lengo la kuondooa matabaka na kuwa Taifa ni kuleta unafuu wa maisha kwa kushughulikia matatizo kwa umoja sasa unafuu uko wapi?
 
Wazo zuri ila rasilimali ndio hamna

Ukisoma miongozo mbalimbali inaonesha Kila sekta na standard ya mwajiriwa na idadi ya watu anaotakiwa kuwahudumia

Mfano, mwalimu mmoja anatakiwa kuwahudumia wanafunzi 45 ndani ya chumba kimoja Cha darasa. Sasa nenda kwenye uhalisia Anza darasa lenyewe kwa odadi ya wanafunzi na baadae walimu idadi yao

Sasa hiyo ipo kwenye kila idara mapungufu ni makubwa kuanzia polisi, manesi, madaktari n.k

Sasa kama huna resources hatuna tunajilizaliza nini sasa?!

Africa sio ulaya tena huku kusini mwa jangwa la Sahara tulia wewe!!
Kwahiyo ulaya wamefika walipo kwa kujikuta tu Wapo hivo walivyo gafla?
 
Umewaza na kunena vyema sana.!Shida ya ngozi yetu nyeusi hata wewe ukiingia kwenye mfumo mawazo yote yanayeyuka.. Viongozi Waajiriwa Kama Hayati Magufuli(R.i.P) ni wa chache sana.!
Kwahiyo amna tunachoweza kufanya kutoka hapa kaka? Au ndo tusubiri yesu arudi tu!
 
Nani wa kuthibiti? Kama anayetakiwa kuthibiti naye ni mpuuzi. Bunge, Baraza la Madiwani na Bodi za mashirika wenye wajibu nao ni walewale tu. Nani?

Niliwahi kumwambia jamaa yangu akimsifia sana Magu, kwamba kama Magu anataka kuisaidia nchi hii basi aimarishe mifumo ya kitaasisi badala ya kujiimarisha yeye. Kwani yeye akifa au kuondoka tutarudi kulekule. Polisi awe na nguvu ya kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria, mahakama ndio usiseme, PCCB, CAG nk.

Tatizo wafanya maamuzi na watunga sera huko juu wameoza sana kiasi kwamba huku chini kila mtu anawaza kupiga sehemu yake. Wachache wenye maono kama ya kwako wanaishia kupuuzwa tu. Nao wanaunga tela wanapiga
 
Back
Top Bottom