Alvajumaa
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 4,993
- 6,180
SUPER LEAGUE MFALME WA SOKA ANAEKUJA KWA KASI
ELcapitano Maestro Je umepata kusikia uwepo wa mashindano ya Super League ambayo yatahusisha timu bora barani ULAYA, ambapo humo kutakuwa na timu zipatazo 20, kutakuwa na makundi mawili yaan A na B kila mechi itakuwa ni nyumbani na ugenini.
Kundi A litahusisha timu 10 na Kundi B litahusisha timu 10, kwahiyo hatua ya makundi itahitimishwa kwa kila timu kucheza mechi 18, na baada ya hatua ya makundi kumalizika, kundi A watapita washindi watatu wa juu na kundi B watapita washinda watatu wa juu, piaa nafasi za nne na ya tano kwa kila kundi hapo itachezwa play off ili wawili watakao patikanaa wataungana na timu zile timu 6 zilizopita bila play off kisha kufanyika draw ya kuchezwa Robo Fainali maana hapo kutakuwa na timu 8 tayari, kisha Nusu Fainali na Fainali kupigwa katka kiwanja teule.
Mpaka hivi sasa ni vilabu 12 vya mpira wa miguu vimetangaza kwa pamoja kujiunga na mashindano mapya ya Super League.
AC Milan, Arsenal, Atlético, Chelsea, Barcelona, Internazionale, Juventus, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Real Madrid na Tottenham zote zimejiunga.
Klabu zingine tatu zinatarajiwa kujiunga kama klabu za uanzishaji kabla ya msimu wa uzinduzi, ambao unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo.
Na timu hizo 3 ambazo zitarajiwa kujiunga ni pamoja na Fc Bayern Munich, PSG na Dortmund lakini bado hazijaonesha nia ya kujiunga.
Baada ya Timu hizo 15 kukamilika ndo watakuwa wanachama wa KUDUMU katika kombe hilo, yaani HAKUNA timu itakayo shuka daraja miaka nenda rudi katika hizo timu 15.
ilaa timu 5 zitakazo ongezeka hizo ndo zitakuwa zikishuka daraja kila msimu utapo malizika na wengine wapya watapanda.
Mashindano hayo yatakuwa yanaanza Mwezi wa 8 na kumalizika Mwezi wa 5, na mechi zake zitakuwa zikichezwa katikati ya wiki, hivyo hayata hathiri ligi yoyote ile ya ndani.
Baada ya FIFA na UEFA kupata taarifa hio kuhusu kuja kwa mashindano mapya ya Super League, wamepinga vikali mno kuwepo kwa mashindano hayo na kutoa sheria ngumu kwa wachezaji watakao cheza michuano hio, huku FIFA wakisema mchezaji yeyote atakae cheza ktk mashindano hayo basi hatokuwa na kibali cha kucheza kombe la dunia.
Ila SUPER LEAGUE wao wamesema wanataka wafanye mazungumzo na FIFA pamoja na UEFA ili kuweza kufanya kazi pamoja, haya tuseme kimeumana .
Huu mpango wa Super League haukuanza Leo wala Jana, inaonesha ni mpango wa muda mrefu ambao ulishaandaliwa kuwa ni lazima ufanyike, hivyo lolote litalotokea watakuwa wanajua wanakabiriana nalo vipi, ndomana licha ya Fifa na Uefa kuonesha kupinga mpango wa Super League lakini wao Super League ndo kwanza wanafikiria kufanya kazi pamoja na Fifa & Uefa.
Muundo wa SUPER LEAGUE:
Mwenyekiti: Florentino Perez (Real Madrid)
Makamu mwenyekiti: Andrea Agnelli (Juventus)
Makamu mwenyekiti: Joel Glazer (Man United)
Ikumbukwe Timu zenye mashabiki wengi zaidi DUNIANI ni pamoja na Real Madrid na Man United, na VIONGOZI wa kubwa katika mashindano hayo ya Super League wanatoka katika timu ya Real Madrid na Man United.
NB: Omba Mungu akupe akili ya kutafuta pesa, ila usiombe kupata pesa na ukakosa akili, Uefa Champions League ni kama waliliridhika ila SUPER LEAGUE wanakuja kumwaga pesa ili wapate pesa zaidi.
Kushiriki tu katika Michuano hii ya Super League timu inapata €350 milion na mshindi wa kombe hili anapata €500 milion
Wakati bingwa wa Uefa Champions League anapata €82.4 milion.
Kama timu tu inapewa €350 milion, Je FIFA na UEFA wakikubali kukaa chini kufanya mazungumzo na SUPER LEAGUE wewe unadhani FIFA na UEFA wataweza kutoka katika mitego ya SUPER LEAGUE.
Siku hizi FOOTBALL IS ALL ABOUT MONEY
#Football_Legendary
#Elcapitano_Maestro
Copy & paste