Katika level ipi wanachagua majibu ya hesabu Mkuu..hesabu ni somo Rahisi sana tulipokua tunasoma tuliita somo Mfu halibadiliki na watu walikua wanafaulu sana kwa sasa ivi wanafunzi wenyewe wanatishwa kwanza kuwa somo gumu..watafaulu vipi na walimu wazuri wachache wengi wanalikwepa kusoma na kulifundisha..
Dr. Ndalichako ndiye aliyeanzisha 'chagua jibu sahihi' alipokua katibu mkuu wa baraza la mitihani. Kwa kua kwa sasa ni Prof, ni vyema aliangalie na hilo kwani kipindi analiweka alikua bado ni Dr.
Hata mimi kanikumbisha enzi hizo nikiwa la tano dah nilikuwa najiona msomi mkubwa hasa nikipata vema zote nakumbuka nilikuwa nakumbuka idadi ya vema kwenye daftari langu, nilichukia sana alama ya kosa kwenye daftari langu hata ilipotokea nimekosea nilitamani kuiparua ile alama kwa wembe duh utoto bwana raha sana. Nikapoteza hilo daftari nilikosa amani mwezi mzima hadi leo nalikumbuka zaidi ya miaka 20yrs iliyopita