Mfanyabiashara aidai milioni 227 halmashauri ya Monduli kwa miaka 18 ni baada ya kujenga shule ya Sokoine

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
194
467
Mfanyabiashara na mkazi wa jiji la Arusha, Patrick Swai ameangua kilio mbele ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akilalamikia halmashauri ya Monduli kushindwa kumlipa malipo yake ya sh, milioni 227.7 kwa muda wa miaka 18 baada ya kukamilisha ujenzi wa shule.

Akiongea na vyombo vya habari alisema kuwa aliingia makubaliano na halmashauri hiyo kwa nyakati tofauti kujenga shule ya sekondari ya Ole Sokoine iliyopo kata ya Monduli juu pamoja na kusambaza vifaa vya ujenzi .

Alisema katika mikataba walioingia na halmashauri hiyo yenye thamani ya sh,milioni 456.1, mwaka 2007 ilikuwa ni pamoja na kujenga Madarasa, Mabweli na nyumba za walimu.

Alisema 2013 waliingia makubaliano mengine ya ujenzi Maabara, Nyumba ya Mkuu wa shule, Matundu ya vyoo, matenki ya Maji na kukarabati sehemu ya jengo hilo.

Katika kipindi chote cha makubalino, halmashauri hiyo iliweza kumlipa kiasi cha sh. milioni 228.3 tu na kubaki deni la sh, milioni 227.7 ambalo hadi sasa bado anasotea hajaweza kulipwa na kupelekea mfanyabiashara hiyo kuishi maisha ya taabu.

"Wakati wa ujenzi wa mradi huo nilikopa fedha benki kwa ajili ya kukamilisha mradi huo baada ya kuombwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo hayati Edward Lowassa aliyekuwa ameambatana na Laigwanani wa Eneo hilo Meijo Ole Kisongo"

Alisema kutokana na kuchelewa kwa malipo hayo nyumba yangu ya biashara pamoja na mitambo yangu ya ujenzi iliuzwa na benki ili kufidia deni alilokuwa akidaiwa baada ya kushindwa kulipa mkopo kutokana na kucheleweshwa kwa madai yake.

Aliongeza kuwa katika ujenzi wa mradi huo alipoteza gari lake moja baada ya kudumbukia korongoni kwenye kina kirefu wakati akipakia mchanga na mawe kutoka umbali mrefu.

Akiongea kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa mkoa Paulo Makonda wilayani humo, alimweleza jinsi halmashauri hiyo imeshindwa kumlipa fedha zake hatua ambayo imesababisha aishi maisha ya kubangaiza.

Alisema licha ya malalamiko yake kuyapeleka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, na katibu tawala David Lyamongi kuiandikia barua halmashauri hiyo mwaka 2020 ya kuitaka imlipe madai yake mfanyabiashara huyo mwenye kampuni ya ujenzi ya God's enterprise co ltd, lakini bado aliendelea kupigwa danadana na watawala wa halmashauri hiyo.

Swai alimweleza mkuu huyo jinsi anavyopata tabu katika kuendesha maisha yake kwani ameshajaribu kila njia ya kupata msaada wa madai yake lakini amekuwa akiambukia patupu.

Katika Mkutano huo Makonda alimhoji Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Happiness Laizer juu ya madai hayo iwapo anamfahamu mlalamikaji pamoja na madai yake.

Mkurugenzi alijibu kuwa deni hilo halipo kwenye kumbukumbu za halmashauri hiyo na yeye alipata kusikia madai hayo katika juma la haki katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha lililoendeshwa na mkuu huyo wa Mkoa kwa wananchi kutoa malalamiko na kero zao.

Hata hivyo Makonda aliendelea kumng'ang'ania Mkurugenzi huyo kwa kumwamuru kumlipa mfanyabiashara huyo kwakuwa anatambua shule hizo za kata zilijengwa na mfanyabiashara huyo aliyekuwa akisambaza vifaa vya ujenzi.

"Mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa sasa halmashauri haina fedha ila kuna fedha zetu tunatarajia kulipwa na Shirika la umeme Tanesco "alisema Mkurugenzi huyo.

Swai ameiomba serikali kumsaidia kupata fedha zake kwani kipindi hicho alitumia rasilimali zake zote baada ya uongozi wa halmashauri hiyo kumwomba kuwajenga shule hizo za kata baada ya rais wa kipindi hicho Jakaya Kikwete kuagiza ujenzi wa shule za sekondari kata pamoja na maabara.

IMG_20240528_140410_788.jpg
 
sasa mtu anadai hela nyingi hivyo kila akiaambiwa apeleke nyaraka hana. hakuna halamshauri aua serikali inayoweza kulipa hiyo hela kama hana mktaba na nyaraka za kusapoti kweli ali supply hizo mataerial. lowasa alimdanganya mzee wa watu akajaa kwenye mfumo.

Serikali haifanyi kazi kwa mikataba ya Mdomo
 
Kuna wavimba macho wanamlaumu Makonda akiwapiga spana.Hawa wazembe sio wa kuwaonea aibu wala kuwanyenyekea.Wanakula pesa za kodi na wanashindwa hata kulipa pesa walizopata kutoka Serikali Kuu na vyanzo vya ndani.
 
Mfanyabiashara na mkazi wa jiji la Arusha, Patrick Swai ameangua kilio mbele ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akilalamikia halmashauri ya Monduli kushindwa kumlipa malipo yake ya sh, milioni 227.7 kwa muda wa miaka 18 baada ya kukamilisha ujenzi wa shule.

Akiongea na vyombo vya habari alisema kuwa aliingia makubaliano na halmashauri hiyo kwa nyakati tofauti kujenga shule ya sekondari ya Ole Sokoine iliyopo kata ya Monduli juu pamoja na kusambaza vifaa vya ujenzi .

Alisema katika mikataba walioingia na halmashauri hiyo yenye thamani ya sh,milioni 456.1, mwaka 2007 ilikuwa ni pamoja na kujenga Madarasa, Mabweli na nyumba za walimu.

Alisema 2013 waliingia makubaliano mengine ya ujenzi Maabara, Nyumba ya Mkuu wa shule, Matundu ya vyoo, matenki ya Maji na kukarabati sehemu ya jengo hilo.

Katika kipindi chote cha makubalino, halmashauri hiyo iliweza kumlipa kiasi cha sh. milioni 228.3 tu na kubaki deni la sh, milioni 227.7 ambalo hadi sasa bado anasotea hajaweza kulipwa na kupelekea mfanyabiashara hiyo kuishi maisha ya taabu.

"Wakati wa ujenzi wa mradi huo nilikopa fedha benki kwa ajili ya kukamilisha mradi huo baada ya kuombwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo hayati Edward Lowassa aliyekuwa ameambatana na Laigwanani wa Eneo hilo Meijo Ole Kisongo"

Alisema kutokana na kuchelewa kwa malipo hayo nyumba yangu ya biashara pamoja na mitambo yangu ya ujenzi iliuzwa na benki ili kufidia deni alilokuwa akidaiwa baada ya kushindwa kulipa mkopo kutokana na kucheleweshwa kwa madai yake.

Aliongeza kuwa katika ujenzi wa mradi huo alipoteza gari lake moja baada ya kudumbukia korongoni kwenye kina kirefu wakati akipakia mchanga na mawe kutoka umbali mrefu.

Akiongea kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa mkoa Paulo Makonda wilayani humo, alimweleza jinsi halmashauri hiyo imeshindwa kumlipa fedha zake hatua ambayo imesababisha aishi maisha ya kubangaiza.

Alisema licha ya malalamiko yake kuyapeleka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, na katibu tawala David Lyamongi kuiandikia barua halmashauri hiyo mwaka 2020 ya kuitaka imlipe madai yake mfanyabiashara huyo mwenye kampuni ya ujenzi ya God's enterprise co ltd, lakini bado aliendelea kupigwa danadana na watawala wa halmashauri hiyo.

Swai alimweleza mkuu huyo jinsi anavyopata tabu katika kuendesha maisha yake kwani ameshajaribu kila njia ya kupata msaada wa madai yake lakini amekuwa akiambukia patupu.

Katika Mkutano huo Makonda alimhoji Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Happiness Laizer juu ya madai hayo iwapo anamfahamu mlalamikaji pamoja na madai yake.

Mkurugenzi alijibu kuwa deni hilo halipo kwenye kumbukumbu za halmashauri hiyo na yeye alipata kusikia madai hayo katika juma la haki katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha lililoendeshwa na mkuu huyo wa Mkoa kwa wananchi kutoa malalamiko na kero zao.

Hata hivyo Makonda aliendelea kumng'ang'ania Mkurugenzi huyo kwa kumwamuru kumlipa mfanyabiashara huyo kwakuwa anatambua shule hizo za kata zilijengwa na mfanyabiashara huyo aliyekuwa akisambaza vifaa vya ujenzi.

"Mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa sasa halmashauri haina fedha ila kuna fedha zetu tunatarajia kulipwa na Shirika la umeme Tanesco "alisema Mkurugenzi huyo.

Swai ameiomba serikali kumsaidia kupata fedha zake kwani kipindi hicho alitumia rasilimali zake zote baada ya uongozi wa halmashauri hiyo kumwomba kuwajenga shule hizo za kata baada ya rais wa kipindi hicho Jakaya Kikwete kuagiza ujenzi wa shule za sekondari kata pamoja na maabara.

View attachment 3001912
DAH HALMASHAURI N WASHENZI SANA KUMBE MAKONDA WANYOOOSHEE BABAA WAONYESHE WALIPOZIPELEKA
 
Makonda pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu but jamaa Yuko smart sana,watendaji Arusha watanyooshwa vibaya sana
 
Nimesikitika sana, mamlaka zimsaidie huyu baba apate haki yake ikiwemo na fidia ya mali zake zilizouzwa na benki.
 
Ukitaka ufirisike fanya kazi na hizi HALMASHAURI utajuta
Pesa yako unawadai lakini unaonekana msumbufu
Mbaya zaidi huwezi kuwapeleka kokote
Inabaki nenda rudi nenda rudi
Kama uliingia mikataba kihalali unawapeleka mahakamani na unawashinda vzr, sema hayo mambo ya kuombwa na wazee afu ujenge shule ya serikali ndo kimeo...

Wa kwanza kumlaumu ni YEYE
 
NJIA NZURI NA RAHISI YA KUFILISIKA, FANYA BIASHARA NA HALMASHAURI AU MANISPAA.
 
Back
Top Bottom