Mfahamu aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini, Mabior Garang De Mabior

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
13,924
27,997
Sina maelezo lakini nimecheka sana 😂😂😂

===

13174132_1099511190092298_676957432517822589_n.jpg

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini Mh. Mabior Garang De Mabior ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Sudan Kusini na kiongozi wa zamani wa kikundi cha waasi cha SPLA/M cha Sudan Dr. John Garang alikuwa gumzo mitandaoni baada ya picha zake zenye utata kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Mabior Garang ambaye ni mtoto mkubwa wa Marehemu John Garang ambaye aliongoza kikundi cha waasi kwa muda mrefu kabla ya kufariki katika ajali ya Helkopta mwaka 2005 akiwa Rais wa Sudan Kusini, alifukuzwa katika kikao cha Baraza la mawaziri na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi yasiyostahili.

Mwaka 2014, Mabior aliwahi kukamatwa na maafisa usalama wa Ethiopia kwa kile kilichohisiwa kuwa jaribio la kutaka kumuua Rais wa sasa wa Sudan Kusini Salva Kiir baada ya kukamatwa akiwa hotelini na bastola ikiwa na risasi sita. Baada ya kukamatwa na kuhojiwa alisema alitaka kukutana na Rais Kiir kwani ameharibu kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Baba yake John Garang.

Mabior Garang alihudumu katika Serikali ya Umoja kupitia Dr Riek Machar ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini
 
Wakichimba kidogo tu mafuta haya hapa
Ila maji dhiki
Pamoja na hilo wana njaa mbaya na elimu hakuna
Walipopewa Uhuru walikosekana wataalamu ikabidi wasudani watoke majuu kuja kuomba uwaziri na Ukurugenzi
Wako choka mbaya
Ma vita vita yamewaathiri
Ila wengi wametoka na wanasoma nje,na kuna wakati nlipokuwa huko Juba nlikutana jamaa kutoka huko wanajeshi walikuwa wanasoma open University dsm ....
So wanajisukuma,ila napenda mentality yao watu huko siyo wajinga kabisa

Ova
 
Najua mkuu, ni vita ya wao kwa wao
Mara Janjaweed na wengine
Mafuta yao lazima yaende North baharini hapo ndio shida naona
Zamani walielewana ila wakatengana
 
Sina maelezo lakini nimecheka sana 😂😂😂

===

View attachment 3044540
Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini Mh. Mabior Garang De Mabior ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Sudan Kusini na kiongozi wa zamani wa kikundi cha waasi cha SPLA/M cha Sudan Dr. John Garang alikuwa gumzo mitandaoni baada ya picha zake zenye utata kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Mabior Garang ambaye ni mtoto mkubwa wa Marehemu John Garang ambaye aliongoza kikundi cha waasi kwa muda mrefu kabla ya kufariki katika ajali ya Helkopta mwaka 2005 akiwa Rais wa Sudan Kusini, alifukuzwa katika kikao cha Baraza la mawaziri na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi yasiyostahili.

Mwaka 2014, Mabior aliwahi kukamatwa na maafisa usalama wa Ethiopia kwa kile kilichohisiwa kuwa jaribio la kutaka kumuua Rais wa sasa wa Sudan Kusini Salva Kiir baada ya kukamatwa akiwa hotelini na bastola ikiwa na risasi sita. Baada ya kukamatwa na kuhojiwa alisema alitaka kukutana na Rais Kiir kwani ameharibu kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Baba yake John Garang.

Mabior Garang alihudumu katika Serikali ya Umoja kupitia Dr Riek Machar ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini
Huyu ndiye aliyekuwa anapart na yule mtoto wa Odinga ambaye mara baada ya hapo aliporudi home akakutwa na mkewe kafa kitandani. Jamaa hana shida ya fedha hata hapa TZ anatimba mara kwa mara
 
Back
Top Bottom