Meya wa Arusha azindua mitambo yenye thamani ya Tsh 1.7 Bilioni ili kujenga barabara. Hizi ni sarakasi za Uchaguzi?

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,712
4,448
Wakuu,

Hivi karibuni nimeona miradi mingi ya barabara inazinduliwa kwenye sehemu mbalimbali za Tanzania. Kila kitu cha habari ni wabunge na Mameya wa CCM wakizindua miradi mbalimbali ya barabara.

Walikuwa wapi miaka 4 iliyopita au ndo fedha zimepatikana sasa hivi?

==================================================================
Halmashauri ya Jiji la Arusha imenunua mitambo mipya mitatu yenye thamani ya Sh1.7 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa barabara za ndani.

Mitambo hiyo iliyozinduliwa Januari 29,2025 na Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranghe ni greda aina ya Catapiler -Model 140GC pamoja na malori mawili (SINOTRUK-ModI HOWO) yaliyonunuliwa kwa fedha ya mapato ya ndani ya mwaka wa fedha 2024/25.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mitambo hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo amesema inakwenda kujibu kilio cha muda mrefu cha wananchi ikiwamo changamoto ya barabara korofi hasa zinazoharibiwa na mvua.

Amesema halmashauri hiyo ilitenga Sh2 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na malori.

 
Nawapongeza kwa hatua hii nzuri..nashauri waanze na hizi barabara
1.Kona ya Kuingia PPF Kijenge -- Moshono Kituo cha Afya - Moshono
2.Kijenge Mwanama- Viwandani- Engutoto
3.Njiro - City College of Health
4.Moshono -- Sorenyi Baraa -- Moshi Arusha road
5.Barabara za Kata ya Muriet...ni MAJANGA
 
Back
Top Bottom