SI KWELI Meno ya mtoto yaliyolegea lazima yang’olewe ili kuzuia mengine yasiotee pembeni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hatua za ukuaji wa mtoto huambatana na mabadiliko mengi ya kimwili. Mojawapo ya mabadiliko hayo ni kung’oka kwa meno ya awali na kuota kwa meno ya kudumu.

5B1A035C-14C8-48BC-9241-739CFC3F63C2.jpeg

Mdau wa JamiiForums ametoa hoja kuwa meno ya mtoto mwenye umri kati ya miaka 6-7 yanapotingishika kisha yakaendelea kukaa pasipo kung’olewa husababisha meno mengine kuota kwa pembeni, hivyo ni lazima yang'olewe ili kuepusha kutokea kwa tatizo hili.

Madai haya yana ukweli kiasi gani?
 
Tunachokijua
Wataalam wa afya wanashauri meno ya utotoni yanapofikia muda wa kung’oka yasitikiswe, ili kuepuka madhara mbalimbali ikiwemo kuathiri mishipa ya fahamu ya mtoto. Hii hutokea kwenye umri kati ya miaka 6-12.

Wamesema kimsingi jino la utotoni ambalo kitaalam linaitwa la awali, linapolegea kwa vyovyote lipo lingine jipya linaloota chini yake, linaloitwa la kudumu.

“Kunatokea hali ya kufyonza kwenye jino jipya, ambayo husaga mzizi wa jino la awali na kulifanya lipande juu, hatimaye kung’oka lenyewe,” amesema Mtaalam wa kinywa na meno katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, Dk Casmir Kiloya.

Amesema wakati mwingine kusagika kwa mzizi huenda kusifanyike kwa usahihi, kutokana na umbali uliopo kati ya jino la zamani na jipya, hivyo kusababisha la awali kutolegea.

Matokeo yake la kudumu litachomoza pembeni mwa lile la awali, na kwa hali hiyo mzazi anashauriwa kumpeleka mtoto hospitali, ambapo jino la utotoni litaondolewa kitaalam ili kulipatia nafasi jipya kukaa panapostahili.

Amesistiza jino kutong’olewa kienyeji, kwani madhara yake ni makubwa, ikiwemo uwezekano wa mtoto kuvuja damu nyingi pamoja na kuota uvimbe pale jino lilipotolewa.

Amesema uvimbe nao ukitibiwa kienyeji utasababisha hadi kifo.

“Lakini pia meno yakishakuwa mawili eneo moja mzazi anaweza kuondoa la kudumu na kuacha la awali, hivyo kumsababishia mtoto pengo la maisha kwa sababu hakuna tena uwezekano wa kuota jino lingine” ameongeza Dk Kiloya.
Meno yasipong'olewa hupandiana hili ni dhahiri kabisa, wala haihitajiki sayansi kuuubwa.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom