informer 06
Member
- May 11, 2024
- 51
- 27
Meneja wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) Mhandisi Leonard Ngayungi amesema, kwa sasa kuna miradi mitatu ya BRT ambayo utekelezaji wake unaendelea huku ujenzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili (BRT II) ukifikia asilimia 99 ambapo kwa sasa wako katika hatua ya mwisho ya kuukamilisha mradi huo.
"Tuna miradi mitatu ya ambayo utekelezaji wake unaendelea, ujenzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Kwanza (BRT I) umeshakamilika na unaendelea kutumika huku awamu ya pili ya mradi huo kutoka Mbagala hadi Gerezani ukifikia asilimia 99 na tuko katika hatua ya mwisho ya kufunga taa kwa ajili ya usalama na kuongozea magari" alisema Mhandisi Ngayungi
Ameongeza "Kwa awamu ya tatu ya mradi kutoka katikati ya Jiji kwenda Gongo la Mboto umefikia asilimia 59 licha ya changamoto za mvua kuwepo na kuvuruga kidogo utaratibu, lakini mkandarasi ameshajipanga katika kuhakikisha kwamba mradi unakamilika kwa wakati."
Ameyasema hayo Agosti 23, 2024 ambapo Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Mwanaasha Khamis Juma imetembelea kujionea utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya ya Mabasi yaendayo Haraka (BRT) pamoja na madaraja ya juu (fly over) ambayo inatekelezwa na Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) katika jiji la Dar es Salaam
Akiongea mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Mwanaasha amesema, kwa upande wa Zanzibar wameona haja ya kujenga madaraja ya juu kwa lengo la kuondosha usumbufu wa foleni za magari katika maeneo mbalimbali visiwani humo na kwa hivyo kulazimka kuja kujifunza na kujionea utekelezaji wa miradi hiyo kwa upande wa Tanzania Bara.
Soma Pia:
Pia Mhandisi Mshauri katika mradi wa BRT III kutoka kampuni ya SMEC, Mhandisi Andrew Burnside amesema, mradi huo unaendelea vizuri kwa kuzingatia ubora unaotakiwa huku akidai kuwa hakuna changamoto zozote kwa sasa zinazowakabili, hatua ambayo ameeleza kuwa inawapa matumaini ya kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Aidha awali Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Ephatar Mlavi akiwa katika ofisi za makao makuu ya Wakala ameieleza Kamati hiyo kuwa mradi wa BRT ulibuniwa kwa lengo la kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam,ambapo amedai kuwa umeleta tija.
Imeelezwa kuwa lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujifunza ili maarifa watakayoyapata wakayatumie katika upande wa Tanzania Zanzibar ambapo kwa sasa ujenzi wa madaraja ya juu visiwani humo umeanza.
Ameongeza "Kwa awamu ya tatu ya mradi kutoka katikati ya Jiji kwenda Gongo la Mboto umefikia asilimia 59 licha ya changamoto za mvua kuwepo na kuvuruga kidogo utaratibu, lakini mkandarasi ameshajipanga katika kuhakikisha kwamba mradi unakamilika kwa wakati."
Ameyasema hayo Agosti 23, 2024 ambapo Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Mwanaasha Khamis Juma imetembelea kujionea utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya ya Mabasi yaendayo Haraka (BRT) pamoja na madaraja ya juu (fly over) ambayo inatekelezwa na Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) katika jiji la Dar es Salaam
Akiongea mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Mwanaasha amesema, kwa upande wa Zanzibar wameona haja ya kujenga madaraja ya juu kwa lengo la kuondosha usumbufu wa foleni za magari katika maeneo mbalimbali visiwani humo na kwa hivyo kulazimka kuja kujifunza na kujionea utekelezaji wa miradi hiyo kwa upande wa Tanzania Bara.
Soma Pia:
- Ujenzi wa Miundombinu ya mabasi ya Mwendokasi Awamu ya Nne - Dar unaendelea
- Huduma ya Magari ya Mwendokasi (BRT) Ianze Mbagala