Jamani kichwa kinajieleza.
Kwanza ni kweli mende anazalisha maziwa? Mende hawa hawa tunaowaona chooni? Sasa maziwa yenye yanakaa wapi na wanakamuaje? Halafu eti inasemekana maziwa ya mende yanavirutubisho kuliko ya ng'ombe, si makubwa haya!
Mende walivyo wachafu na wanavyoogopesha leo mtu ukanywe sijui ule maziwa yake, yaani sitaki hata kupata picha kwakweli.
Wakuu hili ni kweli?
Kwanza ni kweli mende anazalisha maziwa? Mende hawa hawa tunaowaona chooni? Sasa maziwa yenye yanakaa wapi na wanakamuaje? Halafu eti inasemekana maziwa ya mende yanavirutubisho kuliko ya ng'ombe, si makubwa haya!
Mende walivyo wachafu na wanavyoogopesha leo mtu ukanywe sijui ule maziwa yake, yaani sitaki hata kupata picha kwakweli.
Wakuu hili ni kweli?
- Tunachokijua
- Mende ni wadudu wenye sifa ya kuwa na mwili ulio na umbo bapa, antena ndefu kama uzi, na ngozi inayong'aa ya rangi nyeusi au kahawia.
Muundo wa kichwa chao umeinamishwa kuelekea chini, na sehemu za mdomo zimeelekea nyuma badala ya kwenda mbele au chini kama ilivyo kwa wadudu wengine wengi.
Mende dume huwa na jozi mbili za mbawa, ilhali jike, katika baadhi ya makundi, hawana mabawa au wana mabawa ya nje, pia huwa na sifa ya kutaga mayai kati ya 16-50 kutokana na aina yao.
Mende hupendelea mazingira ya joto, yenye unyevunyevu, na giza na kwa kawaida hupatikana katika hali ya hewa ya kitropiki au nyinginezo.
Aina za Mende
Kuna zaidi ya aina tofauti 4,500 za Mende duniani. Miongoni mwa kundi hili kubwa, ni takriban aina tofauti 30 pekee ndizo huishi kwenye mazingira yanayomzunguka binadamu.
Mfano wa baadhi ya Mende maarufu wanaopatikana kwenye makazi ya watu ni Mende jamii ya Marekani na Mende jamii ya Ujerumani.
Mende kuzalisha Maziwa
Kama tulivyobainisha awali, kuna zaidi ya aina 4,500 za mende duniani.
Miongoni mwa aina hizi yupo mende ambaye kwa lugha ya kisayansi huitwa Diploptera punctata, hufahamika pia kwa jina lingine la utani la Mende wa Pacific.
Tofauti na mende wengine ambao hutaga mayai, aina hii ya mende huzaa watoto walio hai.
Hutengeneza maziwa katika mfumo wa fuwele (crystals) za protini ili kutumika kama chakula cha watoto wao wanaokua.
Virutubisho vya Maziwa haya
Katika miaka ya hivi karibuni, wanasayansi wamegundua kuwa maziwa haya ni lishe na huchukuliwa kuwa chakula kamili, kwani ni chanzo kizuri cha protini, wanga na mafuta.
Zaidi ya hayo, maziwa ya mende huyu ni chanzo kamili cha protini, kwani hutoa asidi zote tisa muhimu za amino zinazotumika kutengeneza protini ambavyo vinaweza kupatikana tu kupitia mlo.
Haya yanathibitishwa na utafiti wa Anna Williford et al. (2004) wenye kichwa cha habari “Evolution of a novel function: nutritive milk in the viviparous cockroach, Diploptera punctata”
Aidha, utafiti mwingine wa Kamal Niaz et al. (2018) wenye kichwa cha habari “Highlight report: Diploptera functata (cockroach) milk as next superfood” unatoa dokezo kuwa maziwa haya ya mende yanaweza kutumika kama chakula cha kutumainiwa kwenye siku za usoni.
Mende wanaopatikana kwenye mazingira yetu wanaweza kuzalisha maziwa?
Hapana, mende wanaopatikana kwenye mazingira yetu hawawezi kuzalisha maziwa.
Mende wenye uwezo wa kuzalisha maziwa hupatikana kwenye maeneo 5 duniani ambayo ni Australia, Myanmar, China, Fiji, Hawaii na India.
Hii inatoa maana kuwa mende wanaopatikana kwenye mazingira yetu sio kundi moja na mende hawa, hawana uwezo wa kuzaa watoto walio hai na hawawezi kuzalisha maziwa.
Ukiachia sifa hii ya kuzaa watoto na kuzalisha maziwa, Diploptera punctata huwa na umbo dogo kuliko mende wengine wa kawaida pia huwa na sifa ya kutoa sumu inayofukuza maadui.
Pamoja na uwepo wa faida nyingi za maziwa haya, aina hii ya mende huzalisha kiasi kidogo sana cha maziwa hivyo inahitajika jitihada kubwa katika kuhakikisha kuwa yanapatikana ya kutosha ikiwa yatatakiwa kutumiwa na binadamu.