Hii wala sikushauri ujaribu hutaweza hii ni level ya juu na practice ya muda mrefu, naweza kukushauri kujaribu kuacha kupumua kwa sekunde 30, ukifanikiwa acha kwa dakika nzima, endelea mpaka uweze dk 5 na kuendelea, yani huvuti pumzi ndani wala kuitoa nje... Hapo ulipo unaweza kujaribu
Hii ndio death meditation, unakuwa na uwezo wa kutopumua kabisa kwa muda fulani, lakini Kiuhalisia sio kwamba hupumui bali huo mchakato unafanyika kupitia matundu mengine ya mwili kama vinyeleo nk, ila inahitaji mazoezi ya muda mrefu sana
Wale wenye uzoefu na hii kitu hupenda kuwashangaza watu kwa kuomba wazikwe kwa masaa kadha huku mkono tu ama mguu tu ukiachwa nje ya jeneza na kisha kaburi
Ni mchakato wa kutisha na kuogofya sana kwakuwa Kama akishindwa manake mna kesi ya kuua bila kukusudia..
Baada ya masaa husika kupita yenye mashaka mengi hatimaye mnamfukua na kumkuta hai bukheri wa afya
Unaposikia ku develop supernatural powers ndio huku uwezo wa kupumua bila kutumia pua wala mdomo
Meditation nyingine inayofanana na hiyo ni ile ya kuwekwa kwenye jeneza na kuachwa pekeyako kwenye chumba cha giza, kama mjuavyo jeneza ni nyumba ya mfu kwahiyo tayari linakuwa na ile roho ya umauti, na hata wewe mwenyewe kihisia utahisi uko kwenye ulimwengu mwingine kabisa
Kuna baadhi waliojaribu hii aina ya pili walishindwa na kupiga kelele huku wakidai kuwa ile hali ya kufungiwa kwenye jeneza ndani ya chumba cha giza totoro na ukimya vimewakutanisha na wafu
All in all hii ni perception tu inakuletea uhalisia wa kile unachowaza, lengo la meditation hii ni kwenda kinyume na perception ya mazingira uliyopo......!!!!