Media, Tumedhalilishwa!, Tumejidhalilisha!. Ni Matokeo ya Sheria Mbovu, Umasikini, Dawa ni Kuunganisha Habari na UtangazajI, Tulipwe Fungu Nene!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,683
119,318
Wanabodi,

Japo dunia nzima inafahamika nchi kuendeshwa kwa mihilimili mitatu ya The Executives, The Legislature and The Judiciary, si wengi wanaotambua kuwa kuna mhilimili wa nne, The Media. Media ni mhimili, "The Forth Protocol, or The Forth Estate", waandishi wa habari ni mhimili, wanapaswa waheshimiwe, walipwe vizuri kama mihilimili mingine, wasidhauliwe na kutupiwa pesa kama mbwa, na kutokana na njaa, wakazigombea na kujidhalilisha,

Kumetokea tukio la udhalilishaji kwa waandishi wa habari kutupiwa pesa kama mbwa, na wao kuzigombania, kuzichana baadhi, kuharibu vifaa vyao vya kazi na kuonyesha picha mbaya kuwa waandishi wa habari wa Tanzania, ni watu wa hovyo kihivyo na ni watu wenye njaa ya ajabu hadi kuparurana kugombea noti zilizirushwa kwa mtindo wa sadakalawe.

Kabla sijaripoti kilichotokea, naomba kutoa utambulisho wangu mfupi ili haya nitakayo yasema, yatoke kwa mtu ambae ni authority of some sort.

Mimi Pascal Mayalla nilianza kazi ya uandishi Tarehe 02, January, 1990, pale Idara ya Habari Maelezo, wakati huo hapa nchini vyombo vya habari vilikuwa 8 tuu, Magazeti miwili ya Daily News/Sunday News na Uhuru Mzalendo. Gazeti moja la weekly Mfanyakazi. Redio moja ya Taifa, RTD, Redio moja ya dini kule Moshi, Sauti ya Injili, na mashirika miwili ya habari Shihata na Idara ya Habari Maelezo. Tulikuwa na sheria moja ya Habari, The Newspapers Act of 1976. Hatukuwa na sheria ya utangazaji, bali mambo ya habari yalikuwa chini ya Wizara moja ya Habari na Utangazaji. Wakati huo Tanzania tuna vyuo viwili tuu vya habari, TSJ cha Dar na Nyegezi cha Mwanza, hivyo waandishi wote wakongwe, ama wamepitia TSJ ama Nyegezi. Wakati huo ukimaliza tuu chou, unapangiwa ajira direct.

Mimi baada ya kumaliza form six, nilipania kujiunga na chou kikuu cha DSM kusomea sheria, Bahati mbaya baada ya kukosa DV 1 ya form six, huwezi kusoma sheria, hivyo nika opt kusomea uandishi TSJ. Kutoka TSJ nikatua Maelezo, kisha Daily News na kuishia RTD. Tangu hiyo 1990 mpaka leo 2019 ni miaka 29!, hivyo mimi ni authority kwa experience, ya News Agency, Print na Electronics, maoni yangu ni from experienced journalist.

Tulipoleta sheria mbili mpya za habari, mimi kama mwandishi mzoefu nilitoa maoni yangu, both kwa Vipindi vya TV, kuandika kwenye mitandao ya kijamii, na kutoa maoni yangu kwa maandishi kama mdau wa habari.
Nikasema sheria hii mpya ya habari, ni ile ile sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, haiwezi kutusaidia sana katika dunia hii ya utandawazi.

Hiwezekani sekta moja ya habari, yenye vyombo vya habari vya aina tatu, vikaratibiwa na sheria tatu tofauti chini ya wizara mbili tofauti na tukabaki salama.

Sheria ya Habari iko chini chini ya Wizara ya Habari na inaratibu vyombo vya habari vya magazeti, yaani print chini ya Idara ya habari Maelezo. Vtombo vya Utangazaji viko chini ya sheria ya utangazaji inayoratibiwa na TCRA, chini ya wizara ya mawasiliao. Online media inaratibiwa na TCRA chini ya Sheria ya mtandao.
Zamani gazeti ni gazeti tuu kazi yake ni kutoa print out tuu, leo gazeti linafanya utangazaji na kuweka online, huwezi kuwaratibu hawa wote watatu kwa sheria tatu tofauti, mamlaka tofoati chini ya wizara tofauti na mambo yakawa shwari tuu, lazima kutatokea mikanganyika, na mimi katika maoni yangu kwa maandishi nilisema wazi hapa kuna mkanganyiko, hatutaouna mpaka matatizo yaanze kujitokeza ndipo tutafungua macho kuangazia na kuondoa mikanganyiko hii Wito kwa wanahabari: If you can't get what you want, just take what you get!
Sasa soma hiki kisa kilichotokea jana

Tukio hilo humu limeripotiwa na mwana jf huyu Waandishi mmefikia hatua ya kudhalilishwa kiasi hiki?

Kumbe ndio maana tasnia hii inadharaulika kila mahali, sio hapa DSM, Arusha au Mwanza.

Mnafikia mahali mnatupiwa noti kama mbwa anavyotupiwa makombo na mnagombania kiasi cha kuvunjiana kamera zenu na tape recorders?

View attachment 1154274
Mkuu Mkongwe Mzoefu, kwanza asante kutuletea clip hii, hivyo mimi kama mwandishi wa habari, mkwongwe na mzoefu nina haya ya kusema.
  1. Kwanza ni kweli na kiukweli kabisa, waandishi hao habari, wamedhalilishwa kutupiwa fedha kama mbwa, Irene Uwoya amewadhailisha waandishi kuwatunza kwa kuwatupia fedha kama mbwa wanavyotupiwa nyama. Japo Irene Uwoya alifanya kitendo kile cha tunza kwa nia njema, tunza za waandishi zinafanywa kwa heshima maalum ikiwemo kuwawekea hizo tunza kwenye bahasha za khaki na waandishi kukabidhiwa kwa majina na waandishi kusaini. Irene Uwoya ni kiazi, she is imbecile, huwezi kuwatunza kuwatunza watu mtindo wa kuwatunza wasanii on the stage au zile tunza za kitchen party, alifanya vile kutafuta kiki. NB. Nasisitiza Bahasha za waandishi sio rushwa Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa
  2. Waandishi waiokuwepo kwenye tukio hilo pia wamejidhalilisha na kutudhalilisha sisi waandishi wengine wote kuonekana waandishi ndio tuko hivyo kitu ambacho sii kweli. Waandishi wa ukweli tuliopitia mafunzo hatuko hivyo. Kwenye kundi lile naamini kulikuwa na waandishi wa ukweli ambao wao hawakugombea lakini kwa vile lilikuwa zogo, wote wakaonekana waligombea, kwa mtindo wa samaki mmoja akioza, samaki wote wameoza. Haiwezekani mpiga picha mwenye camera ya million 20, agombee elfu 10,000 na kurisk kuharibu kifaa chake cha million 20!.
  3. Kwa jicho la haraka, wengi wa waandishi waiokuwepo pale ni waandishi wa michezo na burudani wakiwemo wale wa online media na ma bloggers. Hawa ni waandishi in a sense ya kuhabarisha jamii kupitia online platforms mbalimbali kama online TVs, blogs, forums, fb, insta, twitter etc. Hawa wanakuwa licenced na TCRA.
  4. Tukio hili ni blessing in disguise kuonyesha jinsi sheria mpya ya habari inavyotuletea majanga!. Kwa mujibu wa sheria, waandishi wa habari wanasajiliwa na Idara ya Habari Maelezo na kupewa Press Cards baada ya kukidhi sifa na vigezo ikiwemo kuwasilisha vyeti vya kitaaluma. Idara hii ya Habari Maelezo iko chini ya Wizara ya Habari, hivyo wanaopata Press Cards za Idara ya Habari Maelezo ni waandishi kweli wenye sifa vigezo na weledi, hawawezi kugombea pesa kama mbwa!.
  5. Wakati Maelezo chini ya Wizara ya Habari wanasajili waandishi wa habari wa ukweli wenye taaluma sifa na vigezo, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, chini ya Wizara ya mawasliano, wao wanasajili ma bloggers na online TV, sifa ya kusajiliwa ni kulipia ada ya usajili ya TZS 1,000,000. Baada ya kulipia ada hiyo, majina yao yanapelekwa Maelezo kuwa issued na Press Cards za Maelezo, hivyo tukikutana kwenye news events wote tunaonekana sawa ni waandishi wa habari wenye Press Cards, mmoja kasomea uandishi kama taaluma, mwingine katokea mtaani hana a wala b kuhusu fani ya habari, matokeo ndio haya sasa ya waandishi kutupiwa fedha kama mbwa na wao kugombea kisha wote kuonekana the same!.
  6. A way Forward. 1. Idara ya Habari isikubali kuletewa makorokocho ya TCRA na kuwapa Press Cards kama za waandishi. Maelezo watenganishe Press Cards kati ya waandishi wa habari wa ukweli waliosomea na hawa ma bloggers na online media ili ikitokea tukio la udhalilishaji wa mwandishi tujue ni mwandishi mweledi wa newsroom au wale wa mitaani wa TCRA. Kinachofanywa na Maelezo kwa sasa ni sawa na madakitari medical doctors kupewa same licenses sawa na waganga wa kienyeji, maana wote wanatibu, mmoja kasomea, mwengine anatumia maruhani and they are the same.
  7. Way Forward 2: Baraza la Idhibati kwa Waandishi wa Habari lianzishwe ili kutuondolea aibu hii na udhalilishwaji huu. Waandishi wajulikane ni waandishi kweli kama ilivyo kwa wanasheria, madakitari na ma engineer, kuwa wakili mtu lazima ahitimu LL.B, chini ya hapo ni paralegal, ili uwe daktari, lazima uhitimu MD, etc, sasa tufike mahali ili kuwa a licensed na accredited journalist lazima uwe na kiwango fulani cha elimu. Wale wasio kidhi vigezo nao watakuwa na utambulisho wao kama ni technical people ma cameraman, ma bloggers, waandishi wa mtaani wa online TV etc.
  8. A Way Forward 3: Turekebishe sheria kuunganisha habari na mawasiloano ambapo mambo yote media yawe chini ya sheria moja. Kwa sasa vyombo vya habari vya print media vinaratibiwa na kudhibitiwa na sheria ya habari chini Wizara ya Habari, na vyombo vyote vya utangazaji vinaratibiwa na sheria ya Utangazaji iko chini ya TCRA, iliyoko chini ya Wizara ya Mawasiliano
  9. A Way Forward 4: Media ni mhimili, waandishi wa habari ni watendakazi wa mhili huu wa nne, nao wanastahili kulipwa malipo mazuri kama kama watu wa mihimili mingine, kama mtu hana uwezo wa kuanzisha media na kuwalipa vuzuri waandishi, basi bora asianzishe, accredited media ziwe na waandishi wasomi, weledi, wanaolipwa vizuri, kama mbwa wa polisi au umbwa wa wazungu, analishwa vizuri na atakula chakula tuu kile alichowekewa na mlishaji wake wa kila siku, siku akitupiwa nyama yanye sumu, hali hata awe na njaa vipi, hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa accredited media, waandishi walipwe vizuri, media ziwe na usafiri wake, waandishi wa accredited media hawahitaji bahasha ya yeyote kwa ajili ya lunch kwa sababu hawana njaa, wala kwa ajili ya usafiri kwa sababu wana unafiri wao, hivyo mtu kichaa kama yule, akiwatupia pesa kama alivyofanya jana, waandishi hao watamwangalia tuu, na pesa zake zitaishia kupeperuka, na kama ni kuokotwa, ziokotwe na wale makanjanja na waandishi wa mitaani wa social media na sio kwa accredited journalists.
  10. Mwsho sisi waandishi wenyewe, tujiheshimu, tuheshimiwe. Ningekuwa ni uwezo wangu, ningewaomba waandishi wote waige mfano wangu, mimi Pascal Mayalla, nikiitwa press conference yoyote, sipokei bahasha yoyote ya mtu yoyote, na hata kwenye events zenye lunch or dinner, mimi na team yangu huwa hatuli lunch ya yeyote wala dinner ya yoyote, hivyo kuendelea kuwa independent, ikiitwa popote, nauliza swali lolote kwa yeyote kwa sababu siwategemei wowote wala yeyote, sipokei bahasha yoyote hivyo kuendelea kuwa an independent journalist.

Paskali
Rejea za Nguli Pasco Kuhusu Tasnia ya Habari Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Na Uchaguzi Mkuu ni Kipindi Cha Neema kwa Media!. Ni Kipindi cha Mavuno!. Jee Bahasha Hizi Ni Halali?!.

Na Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija

Na Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?.
Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer
Wito kwa wanahabari: If you can't get what you want, just take what you get!

Na Magufuli kutawala kurasa za mbele za magazeti, Je anastahili hata kama hazina impact, au wahariri wanajipendekeza?
Na Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?
Na Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya?
Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?. Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?
 
Mkuu uachage kuunganisha ma nyuzi namna hii, unanifanya nisikomenti hapa nikakomenti huko kwenye nyuzi zilizopita, unachokisema ni kweli ila huoni siku hizi wewe mwenyewe unaitwa mzee wa pambio!? Umegeuka msifiaji sana, hii ni baada ya kutoka kuhojiwa na ile kamati uchwara!😬
 
Siku hizi uandishi wa habari umejaa wale watu waliokosa option za maisha...uandishi wa habari na utangazaji umekuwa mbadala wa ualimu.

Cha msingi ni wadau wa sekta hiyo kujitambua na kutoruhusu kufanyiwa haya kwani kilichotokea jana ni matokeo ya uwezo wenu na nafasi mliyowapa hao jamaa kuwatendea vile. Jitambueni na tumieni sana vikundi vyenu vya uanachama kupeana dos and don'ts za habari.

Mkisimama pamoja, hakuna atakaeleta dharau....
 
Hivi sasa wanahabari wamegubikwa na njaa kali iliyojumuika na ukanjanja. Steve Nyerere akiitisha mkutano na waandishi wanajaa waandishi lukuki. Zitto kabwe akiitisha wanaenda waandishi wawili... labda watu watasema waandishi hawana time na siasa... lakini akiitisha bwana Polepole wanajazana kama wamepelekwa na mafuriko

Hakuna tena kubalance stories. Wanaandika zile wanazojua watapewa bahasha na zile Bwana mkubwa atapenda kuzisikia.

What a waste!
 
Hahaha pesa za kuokota nazo hamtaki?! Binadamu hamna shukrani, basi nanyie waandishi waiteni bongo movie muwarushie mapesa kulipizia nao wana njaa sanaaa. Wao wana njaa wanatumiwa na wanasiasa, nao wamempata mnyonge wao. Tusubirie bongo flavor nao watafanyaje.
 
Mkuu Pascal,
Heshima hujengwa na mtu anayetaka kuheshimika/kuheshimiwa. Kama mnataka hiyo heshima tengeneza mazingira ya kuheshimika mtaheshimika.Kama nyie wenyewe manashindwa thamini profession yenu wenyewe hakuna mtu ambaye atawaheshimu.Kama hampati heshima ni kwamba nyie mmeshindwa kujiheshimu na kujithamini wenyewe.

Pia naomba kujua kama waandishi wa habari wana chama chao kama ilivyo kwa Wanasheria ambao wana (TLS). Kama hicho chama kipo inamaana kimeshindwa kutekeleza majuku yao kwa kuwaadhibu/ kuchukua hatua za kinidhamu dhidi waandishi wa habari wanaotenda kinyume na maadili ya waandishi wa habari.
 
Nimekulewa kwenye ulipaji, waandishi waboreshewe maslahi yao. Njaa mbaya sana asee. Hata hivyo ni ngumu kuipangia sekta binafsi (media nyingi ni binafsi) kimo cha chini cha mshahara na kuisimamia, watu kule wanabembeleza kazi na sio kubembelezwa.
 
Hivi kikao chao kilikuwa kimeshaisha? Maana kama kilikuwa bado sidhani kama baada ya pale kiliendelea tena.

Angewapa mmoja mmoja, lakini hiyo ya kuwatupia kila mtu apiganie ni dharau. Hiyo stail inatumika kwa kikundi ambacho wanaaminiana. Wanarushiwa hela baadae zinakusanywa wanagawana. Sasa hiyo ya Irine Duuuh.

Nimesikitika zaidi baada ya kusikia vifaa vya waandishi viliharibika. Nilitegemea aseme ataingia gharama katika matengenezo. Maana kuna ambao hawakuwa na mpango na hizo hela waliendelea kurecord..lakini kilichotokea ni kusukumwa.
 
Mkuu, ujue wandishi wa habari mmejizalilisha wenyewe kwa muda mrefu kwenye matukio mbalimbali.

Iwe vipindi vyenu vya mahojiano unaona kabisa mwandishi ni mjinga wala hana huo weledi ambao kila siku unanasibishwa kuwa ni taaluma na kazi kama kazi zingine.

ni ukweli kuwa sasa kwa tukio hilo ni kuwa mnavuna mlichopanda miaka na mikaka hapa tz. Uwedi mdogo na uwezo mdogo chini juu.

Jana niseme kwa mara ya kwanza niliona Mtozi anajaribu kuja kwenye mstari mahojiano na Sabaya; japo bado halishindwa kusimamia ukweli anaoujua na ukweli mtupu na kumuacha Sabaya akirukaruka hoja na maswali muhimu.

njia yetu kama waandishi wa habari bado ni ndefu mno, tena sana. na hivyo TZ bado itabaki kuwa nchi ya giza

Asanteni

Wanabodi,

Japo dunia nzima inafahamika nchi kuendeshwa kwa mihilimili mitatu ya The Executives, The Legislature and The Judiciary, si wengi wanaotambua kuwa kuna mhilimili wa nne, The Media. Media ni mhimili, "The Forth Protocol, or The Forth Estate", waandishi wa habari ni mhimili, wanapaswa waheshimiwe, walipwe vizuri kama mihilimili mingine, wasidhauliwe na kutupiwa pesa kama mbwa, na kutokana na njaa, wakazigombea na kujidhalilisha,

Kumetokea tukio la udhalilishaji kwa waandishi wa habari kutupiwa pesa kama mbwa, na wao kuzigombania, kuzichana baadhi, kuharibu vifaa vyao vya kazi na kuonyesha picha mbaya kuwa waandishi wa habari wa Tanzania, ni watu wa hovyo kihivyo na ni watu wenye njaa ya ajabu hadi kuparurana kugombea noti zilizirushwa kwa mtindo wa sadakalawe.

Kabla sijaripoti kilichotokea, naomba kutoa utambulisho wangu mfupi ili haya nitakayo yasema, yatoke kwa mtu ambae ni authority of some sort.

Mimi Pascal Mayalla nilianza kazi ya uandishi Tarehe 02, January, 1990, pale Idara ya Habari Maelezo, wakati huo hapa nchini vyombo vya habari vilikuwa 8 tuu, Magazeti miwili ya Daily News/Sunday News na Uhuru Mzalendo. Gazeti moja la weekly Mfanyakazi. Redio moja ya Taifa, RTD, Redio moja ya dini kule Moshi, Sauti ya Injili, na mashirika miwili ya habari Shihata na Idara ya Habari Maelezo. Tulikuwa na sheria moja ya Habari, The Newspapers Act of 1976. Hatukuwa na sheria ya utangazaji, bali mambo ya habari yalikuwa chini ya Wizara moja ya Habari na Utangazaji. Wakati huo Tanzania tuna vyuo viwili tuu vya habari, TSJ cha Dar na Nyegezi cha Mwanza, hivyo waandishi wote wakongwe, ama wamepitia TSJ ama Nyegezi. Wakati huo ukimaliza tuu chou, unapangiwa ajira direct.

Mimi baada ya kumaliza form six, nilipania kujiunga na chou kikuu cha DSM kusomea sheria, Bahati mbaya baada ya kukosa DV 1 ya form six, huwezi kusoma sheria, hivyo nika opt kusomea uandishi TSJ. Kutoka TSJ nikatua Maelezo, kisha Daily News na kuishia RTD. Tangu hiyo 1990 mpaka leo 2019 ni miaka 29!, hivyo mimi ni authority kwa experience, ya News Agency, Print na Electronics, maoni yangu ni from experienced journalist.

Tulipoleta sheria mbili mpya za habari, mimi kama mwandishi mzoefu nilitoa maoni yangu, both kwa Vipindi vya TV, kuandika kwenye mitandao ya kijamii, na kutoa maoni yangu kwa maandishi kama mdau wa habari.
Nikasema sheria hii mpya ya habari, ni ile ile sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, haiwezi kutusaidia sana katika dunia hii ya utandawazi.

Hiwezekani sekta moja ya habari, yenye vyombo vya habari vya aina tatu, vikaratibiwa na sheria tatu tofauti chini ya wizara mbili tofauti na tukabaki salama.

Sheria ya Habari iko chini chini ya Wizara ya Habari na inaratibu vyombo vya habari vya magazeti, yaani print chini ya Idara ya habari Maelezo. Vtombo vya Utangazaji viko chini ya sheria ya utangazaji inayoratibiwa na TCRA, chini ya wizara ya mawasiliao. Online media inaratibiwa na TCRA chini ya Sheria ya mtandao.
Zamani gazeti ni gazeti tuu kazi yake ni kutoa print out tuu, leo gazeti linafanya utangazaji na kuweka online, huwezi kuwaratibu hawa wote watatu kwa sheria tatu tofauti, mamlaka tofoati chini ya wizara tofauti na mambo yakawa shwari tuu, lazima kutatokea mikanganyika, na mimi katika maoni yangu kwa maandishi nilisema wazi hapa kuna mkanganyiko, hatutaouna mpaka matatizo yaanze kujitokeza ndipo tutafungua macho kuangazia na kuondoa mikanganyiko hii.
Sasa soma hiki kisa kilichotokea jana

Tukio hilo humu limeripotiwa na mwana jf huyu

Mkuu Mkongwe Mzoefu, kwanza asante kutuletea clip hii, hivyo mimi kama mwandishi wa habari, mkwongwe na mzoefu nina haya ya kusema.

  1. Kwanza ni kweli na kiukweli kabisa, waandishi hao habari, wamedhalilishwa kutupiwa fedha kama mbwa, Irene Uwoya amewadhailisha waandishi kuwatunza kwa kuwatupia fedha kama mbwa wanavyotupiwa nyama. Japo Irene Uwoya alifanya kitendo kile cha tunza kwa nia njema, tunza za waandishi zinafanywa kwa heshima maalum ikiwemo kuwawekea hizo tunza kwenye bahasha za khaki na waandishi kukabidhiwa kwa majina na waandishi kusaini. Irene Uwoya ni kiazi, she is imbecile, huwezi kuwatunza kuwatunza watu mtindo wa kuwatunza wasanii on the stage au zile tunza za kitchen party, alifanya vile kutafuta kiki. NB. Nasisitiza Bahasha za waandishi sio rushwa.https://www.jamiiforums.com/threads/waandishi-wa-habari-na-bahasha-sio-kila-bahasha-ni-rushwa-pasco-wa-jf.215720/#js-post-3196765
  2. Waandishi waiokuwepo kwenye tukio hilo pia wamejidhalilisha na kutudhalilisha sisi waandishi wengine wote kuonekana waandishi ndio tuko hivyo kitu ambacho sii kweli. Waandishi wa ukweli tuliopitia mafunzo hatuko hivyo. Kwenye kundi lile naamini kulikuwa na waandishi wa ukweli ambao wao hawakugombea lakini kwa vile lilikuwa zogo, wote wakaonekana waligombea, kwa mtindo wa samaki mmoja akioza, samaki wote wameoza. Haiwezekani mpiga picha mwenye camera ya million 20, agombee elfu 10,000 na kurisk kuharibu kifaa chake cha million 20!.
  3. Kwa jicho la haraka, wengi wa waandishi waiokuwepo pale ni waandishi wa michezo na burudani wakiwemo wale wa online media na ma bloggers. Hawa ni waandishi in a sense ya kuhabarisha jamii kupitia online platforms mbalimbali kama online TVs, blogs, forums, fb, insta, twitter etc. Hawa wanakuwa licenced na TCRA.
  4. Tukio hili ni blessing in disguise kuonyesha jinsi sheria mpya ya habari inavyotuetea majanga. Kwa mujibu wa sheria, waandishi wa habari wanasajiliwa na Idara ya Habari Maelezo na kupewa Press Cards baada ya kukidhi sifa na vigezo ikiwemo kuwasilisha vyeti vya kitaaluma. Idara hii ya Habari Maelezo iko chini ya Wizara ya Habari, hivyo wanaopata Press Cards za Idara ya Habari Maelezo ni waandishi kweli wenye sifa vigezo na weledi, hawawezi kugombea pesa kama mbwa.
  5. Wakati Maelezo chini ya Wizara ya Habari wanasajili waandishi wa habari wa ukweli wenye taaluma sifa na vigezo, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, chini ya Wizara ya mawasliano, wao wanasajili ma bloggers na online TV, sifa ya kusajiliwa ni kulipia ada ya usajili ya TZS 1,000,000. Baada ya kulipia ada hiyo, majina yao yanapelekwa Maelezo kuwa issued na Press Cards za Maelezo, hivyo tukikutana kwenye news events wote tunaonekana sawa ni waandishi wa habari wenye Press Cards, mmoja kasomea uandishi kama taaluma, mwengine katokea mtaani hana a wala b kuhusu fani ya habari, matokeo ndio haya sasa ya waandishi kutupiwa fedha kama mbwa na wao kugombea kisha wote kuonekana the same!.
  6. A way Forward. 1. Idara ya Habari isikubali kuletewa makorokocho ya TCRA na kuwapa Press Cards kama za waandishi. Maelezo watenganishe Press Cards kati ya waandishi wa habari wa ukweli waliosomea na hawa ma bloggers na online media ili ikitokea tukio la udhalilishaji wa mwandishi tujue ni mwandishi mweledi wa newsroom au wale wa mitaani wa TCRA. Kinachofanywa na Maelezo kwa sasa ni sawa na madakitari medical doctors kupewa same licenses sawa na waganga wa kienyeji, maana wote wanatibu, mmoja kasomea, mwengine anatumia maruhani and they are the same.
  7. Way Forward 2: Baraza la Idhibati kwa Waandishi wa Habari lianzishwe ili kutuondolea aibu hii na udhalilishwaji huu. Waandishi wajulikane ni waandishi kweli kama ilivyo kwa wanasheria, madakitari na ma engineer, kuwa wakili mtu lazima ahitimu LL.B, chini ya hapo ni paralegal, ili uwe daktari, lazima uhitimu MD, etc, sasa tufike mahali ili kuwa a licensed na accredited journalist lazima uwe na kiwango fulani cha elimu. Wale wasio kidhi vigezo nao watakuwa na utambulisho wao kama ni technical people ma cameraman, ma bloggers, waandishi wa mtaani wa online TV etc.
  8. A Way Forward 3: Turekebishe sheria kuunganisha habari na mawasiloano ambapo mambo yote media yawe chini ya sheria moja. Kwa sasa vyombo vya habari vya print media vinaratibiwa na kudhibitiwa na sheria ya habari chini Wizara ya Habari, na vyombo vyote vya utangazaji vinaratibiwa na sheria ya Utangazaji iko chini ya TCRA, iliyoko chini ya Wizara ya Mawasiliano
Paskali
 
Leo ndiyo mjue kuwa Yule Kenyan Cartoonist nadhani atakuwa ni Gado wa Gazeti la The East African alipochora Waandishi wa Habari wa Tanzania wakiwa wanailamba Miguu ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Kikwete hakuwa na Kosa lolote tena yawezekana alikuwa anataka Kuisaidia Media ya Tanzania ili ijishtukie, ijitathmini na ibadilike upesi lakini bahati mbaya sana kama kawaida yetu Watanzania wote tukaacha Kuupokea Ujumbe wake ule wa Kifalsafa na tukaanza Kumshutumu na hadi Kumtukana. Mabadiliko makubwa yanahitaji katika Media ya Tanzania na ni Jambo ambalo linahitaji Mjadala mrefu na mpana ili Kuiokoa hii Tasnia ambayo kwa ilivyo sasa Mtu akiniomba Ushauri kuwa akaisome Chuo Kikuu sitomshauri akaisome kwani imeshakufa tena Kifo kibaya mno tu.
 
Waandishi wa habari mbona mnapenda kujipa utambulisho wa kipekee?Eti muhimili wa 4,hakuna kitu kama hicho!!!Sasa na walimu wakijiita muhimili wa 5,wauguzi nao wakajiita muhilimili wa 6,wakulima muhimili wa 7 Nk itakuwaje?Hakuna cha muhimili wa nne wala nini,mko kwenye kundi la wafanyakazi,basi hiyo inatosha!!!!!

Back to topic,maslahi duni kwa waandishi wengi wa ngazi za chini ndio imepelekea kudhalilika!
 
Back
Top Bottom