Mdororo wa uchumi Duniani na mikakati ya viongozi wa Afrika kuuza rasilimali kwa siri kwa lengo la kuendesha serikali zao; nini mtizamo wako?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,037
4,752
Kuanguka kwa uchumi wa Dunia kutokana na COVid 19 kumepelekea Mataifa makubwa kuyumba na hivyo kushindwa kusupport mashirika ya Kimataifa na nchi masikini kama ilivyokuwa awali.

Vita vinavyoendelea Dunia kati ya Russia Ukrain, Israel na ukanda wa ghaza kwa ujumla vimepelekea rasilimali nyingi kuwekezwa kwenye vita kuliko miradi ya maendeleo.

Kwa Afrika sauti ya Umoja wa Afrika imefifia kwa sababu hakuna financial capability yakutetea rasilimali za Afrika badala yake AU imebaki kuwa chombo cha kukemea mapinduzi.

Jumuia za kikanda kama SADC na EAC hazina nguvu, kila nchi inapambana kivyake kisiasa na kiuchumi. Miradi mingi ya EAC inafadhiliwa na Mataifa ya Ulaya na Asia. Mdororo wa uchumi umepelekea kusua sua kwa miradi ya kikanda ikiwemo Bararaba na vituo vya huduma za pamoja mipakani wanaita OSBP.

Kukosekana kwa ajira kunakotokana na kushuka kwa uwekezaji na rushwa kumewafanya vijana kutamani kufa kuliko kuendelea kuishi. Vijana wasio na uwezo wa mlo mmoja kwa siku wanaposikia bunge linapitisha bilioni 500 kuzipeleka Japan zikanunue magari wanasikitika. Wanaposikia msafara wa viongozi una magari zaidi ya mia huku ukipita kwenye kaya maskini wanachukizwa nakuona bora waache kuishi.

Kwa upande mwingine viongozi wa kisiasa wanachofanya nikuuza madini, misitu na rasilimali nyingine wakibadilisha na mikopo ya riba nafuu. Wale wanaohoji wananyamazishwa kwa gharama yoyote kuzima jamii kupata elimu. Siasa imekuwa ikitumika kuwaaminisha wenye njaa kwamba wameshiba na kwamba lazima wakiri wameshiba.

Tunapotazama miaka ishirini mbele tunaamini tutaweza kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo yetu? Endapo rasilimali zote zitakuwa zinamilikiwa na wageni je wazawa wataweza kuishi kwenye sovereign state au watakuwa watumwa kwenye ardhi yao.

After COVID na uuzaji wa rasilimali za nchi kuendesha nchi kunakupa taswira gani miaka ishirini mbele?
 
Rais ni uvivu wake tu wa kufikiri, maana kwa wingi wa rasilimali za nchi anayoiongoza kulikuwa hakuna haja ya kuuza hata kuku ili kupata fedha za kuendesha serikali.
 
Back
Top Bottom